Kama Lissu Anakubalika CHADEMA Kwanini Sasa Wafuasi Wake Wanalialia Na kupiga Mayowe Baada ya Mwamba Mbowe kutangaza Kugombea?

Mnafiki tu we jamaa!


 
Lucas..huwa nakupinga vitu vyako vingi..lkn kwa hili..na mimi nimewashangaa hawa CHADEMA.
1.Walipiga kampeni nyingi za mtandaoni kumsema vibaya mwenyekiti wao ili asichukue form Lissu apite.
2.Nimesikitishwa CDM haiamini katika sanduku la kura....Wanalalamika hovyohovyo badala ya kuweka mkazo kwenye upigaji kura.
3.Lissu ni makamu mwenyekiti - lakini anaongea utafikiri yeye hahusiki kabisa na yaliyoendelea CDM..(Hakuna Collective Accountability)
Tutaamini vipi kama ametumia nafasi yake kupata taarifa nyingi, kugundua vitu vingi bila kuvifanyia marekebisho ili kutumia nafasi hiyo kumshambulia mwenyekiti wake.
4.CDM hawaamini katika taasisi wanaamini katika mtu.Ilikua Mbowe sasa baadhi wanataka Lissu....wanaongelea ukomo wa madaraka utafikiri hilo ndo issue pekee inayoisumbua CDM..Lissu mfano akiingia kwa katiba ya sasa na yeye akakataa kubadirisha, wataliamsha tena watafute mwingine.
Kama ni suala la mabadiliko why lisiwe collective na sio point moja tu ya mwenyekiti wao kugombea..mengine hakuna?? Au ni kikundi cha wachache wanataka kutumia mapungufu ya chama kumweka mtu wao.
5.CDM wanahisi Lissu ni kama nabii vile...labda pia wanahisi ataleta siasa za migomo..Je! Imeitishwa migomo mara ngapi watu hawatokei au ghafla Lissu akiwa M/kiti ndo watapata ujasiri wa kuandamana??

Kama chama kikuu cha upinzani ni vizuri wajikite katika kutii katiba yao ya sasa [ ndo mfano bora], sio watu wanataka kufanya mapinduzi ya kikatiba kisa wanamtaka mtu mwingine.
Mbowe asigombee kwa sababu katiba imemtaka au yeye hana utayari na sio shinikizo la watu wa mitandaoni.
Kila mtu awe na haki ya kuchukua form..afanye kampeni - atakayeshinda hata kama wengine hawa mpendi ndo awe kiongozi.

Sasa hivyo kila mtu anatoa matamko tu.
 
Acha kudandia gari moshi kwa mbele hali likiwa katika mwendo. Tunaitambua hofu ya CCM juu ya matokeo ya uchaguz huu ujao wa CDM., na ni si nyingine bali ni kiti hiki nyeti cha M/Taifa kukaliwa na mpambanaji Tundu Antipasi.

That's where this fear of unknown comes from! 🥺

Zimwi likujualo halikuli ukaisha. Serikari ya CCM inautambua vyema mziki wa kianauharakati wa Lissu. Aidha, wanatambua kwa muda mrefu jinsi zilivyo "conventional politics" za Mbowe.

Kwa hiyo kuja mageuzi ya aina ya uongozi wa Tundu inawafanya machawa aina yako wewe Lucas chupi kuwabana na kusahau hata sehemu ya kujisaidia ilipo. Kaa kwa kutulia huku ukisubiri matokeo ya uchaguzi yatakavyo kuwa.

Ni wajumbe wa mkutano mkuu tu ndiyo watakao amua, ama kuzidi kwenda na siasa zilezile za miaka nenda rudi walizozizoea chini ya uongozi wa Freeman licha ya kufanyiwa udhalimu na mabaya mengi na mahasimu wao wa CCM, ama watahitaji siasa mpya za kumperamera zikishadadiwa na uanauharakati mwingi ndani yake za Tundu.

Acha kurukia mambo ambayo kwa undani hata huyajui. CDM haina mila ya utoaji wa fomu moja tu ili kumkwepesha MTaifa asishindanishwe na makada wengine katika uchaguzi.

Nakutakia maisha mema ya uchawa tunapozidi kukaribia kuufunga mwaka huu wa 2024.
 
Mbowe ni kada wa CCM anayejua kuishi na chama kimaslahi Lissu yupo huru sana kwenye maongezi yake na anaonekana kuwa mkweli kwa upinzani. Ana ile intellectual superiority complex na hatawaliki kwa mipango ya muda mrefu ya CCM.
 
kwasababu hawana kura, wanapuuzwa sana na hawana wafuasi wengi wenye midomo na tamaa kama zao pia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…