Kuna tetesi kuwa Maboresho yatakayofanyika katika reli ya TAZARA yanahusisha kuifanya reli hiyo kutumia treni ya dizeli kama Kenya.
Kama huu ndo ukweli napenda kuzishauri mamlaka za Tanzania kuukataa huu mradi.
Kama tumeweza kujenga reli yetu ya kati kwa kiwango cha SGR tena umeme itakuwa ni aibu na fedheha kuu tukijengewa kwa mkopo reli ya TAZARA iliyo na kiwango cha kutumia dizeli.
Mchina asitupande kichwani. Kama Zambia hawawezi kuwa na treni ya Umeme tumwambie kwa kujiamini kuwa kipande cha reli hii kwa upande wa Tanzania lazima kiwe na viwango vya kutumia umeme.
Akibisha tuachane nae tufanye kama Magufuli alivyoachana nao na kwenda kwa Waturuki kwenye SGR Reli ya Kati
Dogo kama hujui ni hivi hiyo rail ya tazara inapojengwa mwaka 1970 hadi 1975 hamkoa hata mia zaidi ya kupokea hela hiyo reli walichina walitoa dola 400 milliona kama dola 3 billionn tatu za sasa kujenga hiyo reli kama msaada wa bure kabisa
Malengo yalikuwa haya
1 .kupinga na wazungu wa south africa makaburi
Makaburu walikuwa wanazengua sana copper ya zambia ikipita kule so zambia ikawa inakosa mapato so moja ya solution wakaomba msaada china pia nyerere akaenda china kuona na mao akakubali
2.biashara ya copper
China walijua wakijenga reli hiyo wa zambia itawauzia copper kumbuka china ilikuwa ndo inaanza kujenga viwanda vya electrons na copper ni muhimu so waliona mbali so wazambia mteja wao mkuu wa copper ni wa china
3 .kuonesha nguvu ya DRAGON
huo mradi hadi leo hii ni mmoja wa mradi wa kihistoria yaaani wanausoma darasani kama sisi tunavyosoma uhuru sijui maji maji yaaani ni mradi wachina walijitoa wakiwa maskini kabisa kusaidia africa na wao kufaidika na copper kidogo ....
Lakini huo mradi walitaka kuonesha nguvu ya china katika siasa za dunia yaani kuwa china ni taifa lenye nguvu linaweza saidia pia ila kiukweli kwa wakati ule walikuwa kajamba nani tu nao ila walionesha nguvu ya dragon yaani nembo ya china
Tukirudi mwaka huu hiyo reli tanzania na zambia imewashinda kuendesha toka siku nyingi inaendeshwa kwa mikopo ya ulaya mara marekani
Sasa wachina wamesikia uchungu kuona kitu waligharamia kwa moyo mkunjufu kuona kina kufa sasa kupita kampuni yao ya serikali CCECC ya ujenzi wamesema wanataka kuboresha kwenda SGR na nyie watanzania kama ww uliyeandika hiiyo comment kama mna hela mtaweka umeme
LA MWISHO HIYO RELI HAMKUTOA HATA MIA WALA KUDAIWA CHOCHOTE KILE MLIKUWA MMETO MACHO KUPOKEA MSAADA KWA HILI WACHINA NILIWAPA HONGERA ENZI HIYO WACHNA WAJAMAAA KWELI KWELI WANAKUPA HELA KIROHOO SAFI
SASA HIVI WAKIREPAIR HIYO RELI ITAENDESHWA KIBEBARI SIKU HIZI UJAMAA HAWANA