Mganguzi
JF-Expert Member
- Aug 3, 2022
- 1,604
- 3,715
Ninamashaka makubwa na sera za polisi hapa Venezuela hasa kutoka makao makuu ya jeshi Hilo hapa mjini Colombo kama linalinda raia na mali zao ama lipo kupambana na wanasiasa ! Polisi hapa mjini Colombo kwa sasa linapambana na kauli za mapambano ya wanasiasa hasa kipindi hiki ambacho mabondia wakisiasa wanatambiana ! Polisi wanaingilia kauli zinazotolewa na wapinzani lakini hawafuatilii kauli zinazotolewa na viongozi wa chama tawala ! Leo hata mtu akiamua kutoa malalamiko au kero zake kwa serikali ni jinai ! Waalimu wasio na ajira wamejaribu kutoa kero zao wameishia kunigwa roba na sasa tunasikia wako mahabusu ! Kuna mtu analipeleka jeshi hili mahali pabaya Sana! Kuna mtu anatufanya wanavenezuela tuliona jeshi kama kikwazo na sio usalama Tena ! Mbinu za ukamataji nazo pia zimebadilika ,polisi wanamkamata mtu kwa magari binafsi na kupambana nae kama jambazi katikati ya makutano ya watu ! Polisi wa sasa wamefuga Rasta na wananyoosha bastola hadharani ! Kama Kuna siku nchi ya vene itaingia kwenye vurugu na haitatawalika Tena basi chanzo litakuwa ni jeshi la polisi ! Venezuela sio sehemu salama