Mwakilishi
JF-Expert Member
- Jan 31, 2007
- 483
- 34
Dala dala zilianza zenyewe mwaka 1983 kutokana na UDA kutotosheleza mahitaji, na zikawa zikikamua watu TShs. 5 au dala kama ilivyokuwa inaitwa mitaani. Hilo la Sokoine kuzisimamia sijui umelitoa wapi maana kama angefanya hivyo, hii industry ingeendelea siku nyingi sana. Badala yake wakati wake iliendelea kuwa biashara haramu hadi Mzee Mwinyi alipotangazia umma rukhsa ya kufanya biashara. Sokoine alishindwa kutofautisha entrepreneurship na uhujumu wa uchumi na kuhangaisha sana wafanyabiashara.
Mwakilishi Re: Kama Mama Malecela hafai, huyu je anafaa?
Ok kwani Hitler ndo kafanya nini tena?!
Pia sikufahamu kwamba ni Sokoine ndio alituletea Dala Dala. Ni kitendo cha kijasiri mno kuruhusu ubinafsishaji wa nyanja za Uchumi za Usafirishaji wakati wa Nyerere. Ni kama vile alimwambia Nyerere, Mzee haya makampuni yako ya Ujamaa na Kujitegemea ya UDA na KAMATA yanafeli. Ruhusu watu wamiliki vyombo vya uchumi. Alichapa kibao kwenye uso wa Nyerere, na Azimio la Arusha.
Hata hivyo, kama ambavyo tunaungana mkono pale tukikubaliana, tukikosea pia tutakosoana.
Uchambuzi wako wa Adolf Hitler una mushkeli. Hakuna wachambuzi wanaoheshimika wanaosema Ujerumani ya leo ni kazi ya Hitler. Hitler aliua wasomi, isipokuwa watengeneza mabomu. Mabomu yakazaa vita, vita vyenyewe wakashindwa, na li nchi likabomolewa na washindi wa vita. Wasomi wa Kiyahudi wakaanza mbele. Ujerumani ikaanza kujengwa upya baada ya Hitler kuondoka.
Ujerumani ilijengwa tena na mifumo mipya ya Ujamaa wa Masoko ya Kiuchumi (Social Market Economy) kuanzia katikati miaka ya 40 mpaka mwishoni wa miaka ya 50. Tofauti na mifumo ya Kidekta chini ya mawazo ya Hitler, mifumo hii mipya ilihurisha uchumi wa Ujerumani, ikiwa ni pamoja na kufungua milango ya mashindano, kuruhusu masoko huria, pamoja na biashara ya nje. Hilter hasifiki kwa hayo. Kile anachosifika kwa kukijenga wakati wa utawala wake alikivunja kwa mawazo na mwamko wake wa kivita vita.
Ahsante.
1.
Mkuu Mwakilishi, yaani tayari umesahau hii chini wakati umeandika mwenyewe kubadili subject ili unikosose na kuonekana umeshinda hoja, sasa umesahau tayari?
Ndio tutakupatia majibu chini haya hebu soma tena mkuu uone hoja inavyojibiwa kwa hoja, naona sasa unataka dala dala, haya turudi kwenye Dala Dala nako huna facts, aibu tupu mwaka wa hasara bwana!
Hivi kuwepo mjini na kujua daladala zimeanza lini vina uhusiano?
Are you sure ni mimi nimeandika hayo maneno unayodai? Kwa kukusaidia kuondoa paranoia yako, I repeat I am not who you think I am, vipi wewe mbona unanilazimishia tu?
Sio lazima viwe na uhusiano, ila kuna watu kuingia mjini kwao ni kama ushujaa na wana-reminisce kila wakipata mwanya. Wanasahau kuwa kuna wazee kama Maggid Mjengwa ambaye hawezi kuzungumzia siku aliyoingia mjini kwa sababu tangu anapata fahamu yuko town!
Ni wewe mwenyewe ndiye unayejilazimisha, anyways back to the ishu bro tuendelee kukata ishu hapa taifa liko njia panda!
Kumbuka pia kuna wengine hapohapo mjini walikuwa wanapelekwa kila mahali na dreva, hawakuwa wanapanda UDA
Ahsante mkuu, lakini mimi nilizaliwa Ocean Road na kukulia hapo hapo karibu sio mbali sana, na Mjengwa kwangu ni kijana mdogo bado sio level yangu, kwa hiyo sidhani kama nina-fit huu mfano, labda Kubwajinga na Mwakilishi!
Mkuu kweli unaamini kuwa unalijua hili la kupelekwa na Dereva shuleni na kila mahali kuliko mimi? Kweli uaaamini hilo kuwa ni fact?
Itakuwa ni jambo la ajabu sana kwetu, ambapo tuna wasomi kwenye kila chama, kurudi kwenye kibatali au kandili. Ni vema tukabadilisha ile karabai isiyofanya kazi vema kwa kuweka karabai nyingine ili tuendelee kuwa na mwanga wa kutosha, badala ya kukimbilia kibatali ambacho tunajua kabisa kuwa mwanga wake hautoshi.
Unachotakiwa kuweka wazi hapa ni vipi viongozi wenye elimu kubwa bongo ambavyo wameweza kutusaidia na ufisadi na vipi viongozi wasiokuwa na elimu kama kina Sokoine na Mrema waliweza kutusaidia kuondoa ufisadi, tumejaribu waliosoma na hakuna faida yoyote tuliyopata, sasa ni lazima tuywe open kwa kiongozi yoyote mwenye kuonyehsa uwezo, kwa sababu hata akili ya kujua viongozi gani wanotufaa hilo wananchi imetushinda, Mwalimu angekuwa anajua umuhimu wa elimu kama unavyosema basi asingempiga vita msomi Kambona na kumpa Kawawa uongozi wa juu, mkuu bado unahangaika tu aktika kujaribu kui-elimisha chuki yako na Mbowe so far sioni hoja ya msingi!
FMES,Nyerere alisema unapoelimika, yale unayokuwa unayafahamu ni sawa sawa na mduara wa mwangaza unaotengenezwa na taa za kibatali, kandili au karabai. Halafu Giza linalopakana na huo mduara wa mwanga, linakuwa ni yale unayofahamu kuwa huyafahamu na unahitaji msaada.
- Akasema, elimu ya msingi ni sawa na mwangaza wa kibatali. Unasaidia kuona lakini hauoni mbali. Mduara wake wa mwangaza ni mdogo lakini pia mpaka wake na giza ni mdogo vile vile. Kwa hiyo mtu wa kiwango cha elimu hii ya awali, huwa anakua na ufahamu kiasi lakini kibaya kwake ni kuwa, huyu pia huwa anakuwa na ufahamu mdogo sana wa yale asiyojua. Anapovurunda, anavurunda hata yale ambayo mtu mwingine hushangaa kwa nini alifanya hivyo.