Kama Mama Malecela hafai, je Mbowe anafaa?

Kama Mama Malecela hafai, je Mbowe anafaa?

Kwenye hiyo pointi ya daladala nakumbuka circa 1983 kulikuwa na ki-van fulani hivi pale Posta mpya kilikuwa kinajibanza pale kituoni karibu na Agip gas station kinategeshea wateja, nauli ilikua dala(shilingi 5 enzi zile kulikuwa na ile ya coin, sijui ilikuwa sawa na USD 1 au la?), kilikuwa kinakwenda Kinondoni-posta mpya wakati huo na teksi bubu ndio nazo zinaibukia.
 
Dala dala zilianza zenyewe mwaka 1983 kutokana na UDA kutotosheleza mahitaji, na zikawa zikikamua watu TShs. 5 au dala kama ilivyokuwa inaitwa mitaani. Hilo la Sokoine kuzisimamia sijui umelitoa wapi maana kama angefanya hivyo, hii industry ingeendelea siku nyingi sana. Badala yake wakati wake iliendelea kuwa biashara haramu hadi Mzee Mwinyi alipotangazia umma rukhsa ya kufanya biashara. Sokoine alishindwa kutofautisha entrepreneurship na uhujumu wa uchumi na kuhangaisha sana wafanyabiashara.

Mkuu unaendelea kujiabisha tu afadhali unyamaze, kubali tu kuwa hukuwepo mjini, na hujui haya ya Dala Dala maana ungejua vizuri, basi basi la kwanza serious la Dala Dala baada ya kupewa ruhusa na Sokoine, lilikuwa linaitwa "THe Jaws" kutoka kwa bwana mdogo mmoja wa Magomeni, ambaye tulikuwa na naye Ummangani ambaye alikuwa ni mdogo wa Mkulu Wangu Abdul Masudi Jalewa, aliyekuwa Katibu Mwenenzi wa Yanga, na mtangazaji wa Redio Tanzania Michezo,

From there on the message was clear kwa mabaharia wote kuwa Mmasai ameruhusu Dala Dala na Pick up, kwa wasela wote wakaanza kujimwaga Jap na kumwaga vi-Dala Dala recondition kibao bongo, kwa sababu nusu ya Dala Dala zote za mwanzo zilikuwa owned na mabaharia mkuu, ndio na timu ya Simba nao wakakishusha kile ki-Dala Dala like,

By the time Mwinyi anashika urais wa-Tanzania tulikuwa tumeipita mbali sana hiyo ishu ya usafiri mjini, kwanza tulikuwa tumesahau kabisaa, kwa maneno yako ni clear kabisa kuwa hukuwepo mjini, halafu ninashukuru kwamba hatimaye mmeamua kurudi tena kwenye hii ishu baada ya brief ya Hitler!masikini ya Mungu!
 
1.
Mwakilishi Re: Kama Mama Malecela hafai, huyu je anafaa?

Ok kwani Hitler ndo kafanya nini tena?!


Mkuu Mwakilishi, yaani tayari umesahau hii chini wakati umeandika mwenyewe kubadili subject ili unikosose na kuonekana umeshinda hoja, sasa umesahau tayari?

Pia sikufahamu kwamba ni Sokoine ndio alituletea Dala Dala. Ni kitendo cha kijasiri mno kuruhusu ubinafsishaji wa nyanja za Uchumi za Usafirishaji wakati wa Nyerere. Ni kama vile alimwambia Nyerere, Mzee haya makampuni yako ya Ujamaa na Kujitegemea ya UDA na KAMATA yanafeli. Ruhusu watu wamiliki vyombo vya uchumi. Alichapa kibao kwenye uso wa Nyerere, na Azimio la Arusha.

Hata hivyo, kama ambavyo tunaungana mkono pale tukikubaliana, tukikosea pia tutakosoana.

Uchambuzi wako wa Adolf Hitler una mushkeli. Hakuna wachambuzi wanaoheshimika wanaosema Ujerumani ya leo ni kazi ya Hitler. Hitler aliua wasomi, isipokuwa watengeneza mabomu. Mabomu yakazaa vita, vita vyenyewe wakashindwa, na li nchi likabomolewa na washindi wa vita. Wasomi wa Kiyahudi wakaanza mbele. Ujerumani ikaanza kujengwa upya baada ya Hitler kuondoka.

Ujerumani ilijengwa tena na mifumo mipya ya Ujamaa wa Masoko ya Kiuchumi (Social Market Economy) kuanzia katikati miaka ya 40 mpaka mwishoni wa miaka ya 50. Tofauti na mifumo ya Kidekta chini ya mawazo ya Hitler, mifumo hii mipya ilihurisha uchumi wa Ujerumani, ikiwa ni pamoja na kufungua milango ya mashindano, kuruhusu masoko huria, pamoja na biashara ya nje. Hilter hasifiki kwa hayo. Kile anachosifika kwa kukijenga wakati wa utawala wake alikivunja kwa mawazo na mwamko wake wa kivita vita.

Ahsante.

Ndio tutakupatia majibu chini haya hebu soma tena mkuu uone hoja inavyojibiwa kwa hoja, naona sasa unataka dala dala, haya turudi kwenye Dala Dala nako huna facts, aibu tupu mwaka wa hasara bwana!
 
Outside of Hitler's birthplace in Braunau am Inn, Austria is a stone marker engraved with the following message:

Für Frieden Freiheit ,Und Demokratie ,Nie wieder Faschismus ,Millionen Tote mahnen ,Loosely translated, it reads: "For Peace, Freedom and Democracy - Never Again Fascism - Remember the Millions Dead."

However some people have referred to Hitler's legacy in neutral or favourable terms.

1. Former Egyptian President Anwar Sadat spoke of his 'admiration' of Hitler in 1953, when he was a young man, though it is possible he was speaking in the context of a rebellion against the British Empire.

2. [83] Louis Farrakhan has referred to him as a "very great man".

3. [84] Bal Thackeray, leader of the right-wing Hindu Shiv Sena party in the Indian state of the Maharashtra, declared in 1995 that he was an admirer of Hitler.

4. [85] Friedrich Meinecke, the German historian quotes of Hitler, "It is one of the great examples of the singular and incalculable
 
1.


Mkuu Mwakilishi, yaani tayari umesahau hii chini wakati umeandika mwenyewe kubadili subject ili unikosose na kuonekana umeshinda hoja, sasa umesahau tayari?



Ndio tutakupatia majibu chini haya hebu soma tena mkuu uone hoja inavyojibiwa kwa hoja, naona sasa unataka dala dala, haya turudi kwenye Dala Dala nako huna facts, aibu tupu mwaka wa hasara bwana!

Are you sure ni mimi nimeandika hayo maneno unayodai? Kwa kukusaidia kuondoa paranoia yako, I repeat I am not who you think I am, vipi wewe mbona unanilazimishia tu?
 
Kwa sababu wale wote tuliokuwepo mjini Dar tunaelewa matatizo ya usafiri wa UDA na suluhisho lilipokuja, pamoja UDA kujaribu kuleta Ikarus Kumba Kumba toka Hungary, lakini haikusaidia kitu haya hayako kwenye any history ya taifa letu, kwa hiyo ilikuwa ni kuwepo mjini tu sio anything else!
 
Hivi kuwepo mjini na kujua daladala zimeanza lini vina uhusiano?

Sio lazima viwe na uhusiano, ila kuna watu kuingia mjini kwao ni kama ushujaa na wana-reminisce kila wakipata mwanya. Wanasahau kuwa kuna wazee kama Maggid Mjengwa ambaye hawezi kuzungumzia siku aliyoingia mjini kwa sababu tangu anapata fahamu yuko town!

Ni sawa na jinsi wabongo wakikutana US wanavyosimuliana story za jinsi walivyopata Visa ubalozi wa Marekani.Especially wale wabongo waliolazimika kwenda kuchukulia Visa Zimbabwe baada ya ubalozi kulipiliwa.
 
Are you sure ni mimi nimeandika hayo maneno unayodai? Kwa kukusaidia kuondoa paranoia yako, I repeat I am not who you think I am, vipi wewe mbona unanilazimishia tu?

Ni wewe mwenyewe ndiye unayejilazimisha, anyways back to the ishu bro tuendelee kukata ishu hapa taifa liko njia panda!
 
Kumbuka pia kuna wengine hapohapo mjini walikuwa wanapelekwa kila mahali na dreva, hawakuwa wanapanda UDA
 
Sio lazima viwe na uhusiano, ila kuna watu kuingia mjini kwao ni kama ushujaa na wana-reminisce kila wakipata mwanya. Wanasahau kuwa kuna wazee kama Maggid Mjengwa ambaye hawezi kuzungumzia siku aliyoingia mjini kwa sababu tangu anapata fahamu yuko town!

Ahsante mkuu, lakini mimi nilizaliwa Ocean Road na kukulia hapo hapo karibu sio mbali sana, na Mjengwa kwangu ni kijana mdogo bado sio level yangu, kwa hiyo sidhani kama nina-fit huu mfano, labda Kubwajinga na Mwakilishi!
 
Ni wewe mwenyewe ndiye unayejilazimisha, anyways back to the ishu bro tuendelee kukata ishu hapa taifa liko njia panda!

Wewe ndio unalazimisha mtu akikuswalisha tu basi ohh majina yenu mengi mimi langu moja blah blah blah lakini ukiungwa mkono aah hayo ya majina mengi husemi... tell you what for the last time I am Mwakilishi na sina jina jingine humu, get it?!
 
Kumbuka pia kuna wengine hapohapo mjini walikuwa wanapelekwa kila mahali na dreva, hawakuwa wanapanda UDA

Mkuu kweli unaamini kuwa unalijua hili la kupelekwa na Dereva shuleni na kila mahali kuliko mimi? Kweli uaaamini hilo kuwa ni fact?
 
Ahsante mkuu, lakini mimi nilizaliwa Ocean Road na kukulia hapo hapo karibu sio mbali sana, na Mjengwa kwangu ni kijana mdogo bado sio level yangu, kwa hiyo sidhani kama nina-fit huu mfano, labda Kubwajinga na Mwakilishi!

Ok sina nia ya kukukatisha tamaa lakini kwa taarifa yako tu mimi nimezaliwa Aga Khan na kukulia hapohapo mjini!
 
sasa tumwamini nani maana wengine tulizaliwa mwamashele!i love JF maana nacheka sana hadi mbavu zinakaribia kuvunjika!
 
Quote:
Itakuwa ni jambo la ajabu sana kwetu, ambapo tuna wasomi kwenye kila chama, kurudi kwenye kibatali au kandili. Ni vema tukabadilisha ile karabai isiyofanya kazi vema kwa kuweka karabai nyingine ili tuendelee kuwa na mwanga wa kutosha, badala ya kukimbilia kibatali ambacho tunajua kabisa kuwa mwanga wake hautoshi.

Unachotakiwa kuweka wazi hapa ni vipi viongozi wenye elimu kubwa bongo ambavyo wameweza kutusaidia na ufisadi na vipi viongozi wasiokuwa na elimu kama kina Sokoine na Mrema waliweza kutusaidia kuondoa ufisadi, tumejaribu waliosoma na hakuna faida yoyote tuliyopata, sasa ni lazima tuywe open kwa kiongozi yoyote mwenye kuonyehsa uwezo, kwa sababu hata akili ya kujua viongozi gani wanotufaa hilo wananchi imetushinda, Mwalimu angekuwa anajua umuhimu wa elimu kama unavyosema basi asingempiga vita msomi Kambona na kumpa Kawawa uongozi wa juu, mkuu bado unahangaika tu aktika kujaribu kui-elimisha chuki yako na Mbowe so far sioni hoja ya msingi!

FMES,
Kwanza naomba ninukuu post ya awali:


Nyerere alisema unapoelimika, yale unayokuwa unayafahamu ni sawa sawa na mduara wa mwangaza unaotengenezwa na taa za kibatali, kandili au karabai. Halafu Giza linalopakana na huo mduara wa mwanga, linakuwa ni yale unayofahamu kuwa huyafahamu na unahitaji msaada.
  1. Akasema, elimu ya msingi ni sawa na mwangaza wa kibatali. Unasaidia kuona lakini hauoni mbali. Mduara wake wa mwangaza ni mdogo lakini pia mpaka wake na giza ni mdogo vile vile. Kwa hiyo mtu wa kiwango cha elimu hii ya awali, huwa anakua na ufahamu kiasi lakini kibaya kwake ni kuwa, huyu pia huwa anakuwa na ufahamu mdogo sana wa yale asiyojua. Anapovurunda, anavurunda hata yale ambayo mtu mwingine hushangaa kwa nini alifanya hivyo.
FMES,
Huu mfano unachotueleza ni kuwa, asiye na shule ya kutosha anaweza pia akafanya mazuri, lakini upeo wake unakoma mapema na huwa hajui wapi aombe msaada. Ndio maana Mrema alikuwa naibu waziri mkuu na pia askari kanzu aliyeenda kukamata wahujumu kule airport badala ya kuwatumia walio chini yake. Vivo hivyo Sokoine, ingawa alikuwa na elimu kuliko Mbowe na Mrema, naye pia alivurunda pale alipowaburuza watu kwa kuwa tu na TV zaidi ya moja nyumbani kwao. Kawawa naye kuboronga kwake tunakufahamu.

Shule ni muhimu kwa viongozi utake au usitake, unless kuwe hakuna alternative kama ilivyo Zimbabwe ambapo wasomi hawana umaarufu zaidi ya Tsvangirai. Watu kama Mrema, Mbowe n.k., kwa mazingira ya sasa TZ wanafaa kuwa katika nafasi zisizozidi ukuu wa wilaya au kusimamia kamati za chama. Zaidi ya hapo labda wawe ndio pekee wanaofaa.

Lakini kwenye chama kama Chadema chenye akina Zitto, Dr. Slaa n.k., inashangaza kuona kikiongozwa na form six aliyefeli, licha ya kuwa priviledged kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na waTZ wengine wakati akisoma. Sijui kama asingekua mkwe wa mmiliki wa chama kama angekuwa na hayo madaraka.


Tatizo la Mwalimu ni kuwa alipinga chalenge na sio wasomi. Hakushaurika kirahisi awali mpaka alipokuwa too poweful to access. Lau kama angetumia mawazo ya wasomi wote tuliokuwa nao hapo awali na kuacha kuwatumia tu akina mzee Kawawa, Sokoine n.k, ambao uwezo wao wa kupembua ulikuwa ni mdogo kama wa Mbowe hivi sasa, pengine uchumi wetu usingeharibika.
 
Hollo,
Unajua nini, tukianza kukosa ustaarabu wa kujibu hoja na kuanza kushambuliana kwa vigezo vya nani kawahi mjini basi ndio tunapogeuka vituko.
 
Naona kuna ka-strategy ka kutaka kugeuza topic na mjadala, sasa wakuu maana huwezi kukulia mjini ukashindwa kujua ishu ya Dala Dala na Pickup, anyways wakuu heshima mbele naona kazi yangu imeisha hapa, lakini ikibidi nitarudi tena ila kwa sasa naomba ku-retire maana unajua tena jina langu ni moja tu sina mengi kama wenzetu nafikiri mwenye macho hawezi ambiwa ona wanavyojiabisha!

Mkuu Mwakilishi mimi sitegemei kusfiwa, mimi ni mamen ninasimama mwenye we kwa miguu yangu miwili na kujibu mapigo, pound for pound mpaka mwisho!

Anyways Later.....! Mkuu KJ nimeona hoja hapo juu nitarudi baadaye, I love it
 
Back
Top Bottom