Mkuu mimi ni CCM damu, lakini pia ninachelea sana maendeleo ya taifa letu, la Tanzania ambalo ndilo linalopaswa kuwa mbele kabla ya sifa za wagombea na vyama vyao, meaning kwamba ni lazima kwanza qualifications ziambatane na mahitaji ya nchi yetu na wakati wake,
So far binafsi ninaamini kuwa ni marais wetu wawili tu waliopita waliowahi ku-fit kwenye hili, yaani Mwalimu kututoa chini ya wakoloni na kutuweka to the next level, halafu Mwinyi, kutupeleka kwenye demokrasia inagawa ya kiduchu, lakini si haba sasa tuna uhuru wa kusema, Mkapa alikuwa na all the pontetials kuuurekebisha uchumi, lakini kwa bahati mbaya ni kuwa aliutengeneza uchumi kwa faida ya familia yake na marafiki zake, badala ya taifa,
Mwenyekiti wa Chadema wa sasa, ameipokea Chadema ikiwa almost dead, kama sio kuelekea kufa, ameweza kuipa meno mpaka imeweza kuwavuta viongozi imara wa taifa sasa kama kina Zitto, Dr. Slaaa, Wangwe na wengineo kama kina Mnyika, ambao giveni a choice between CCM, NCCR na TLP, au CUF, waliamua kuwa Chadema under Mbowe ndio inayofaa wao kuwemo, ninaamini kuwa anazo qualifications zote zinazotakiwa na Chadema kuwa mgombea wao wa urais, mimi ningeheshimu hoja zako kama zingekuwa zina-base na katiba ya Chadema kutokuwa fullfilled, au za taifa letu, lakini kama anaridhisha katiba za Chadema na Taifa, which ninaamini he does, sielewi the base hasa ya your argument kuanzia kisiasa na kisheria,
Binafsi ninaamini kuwa anao uwezo wa kuwa rais wa Tanzania, hasa kwa wakati huu ambao tuna matatizo ya Respect kwa Rule of Law, tunahitaji kiongozi imara anayeweza ku-up hold sheria zetu, mafanikio ya binafsi kibiashara ya Mbowe ni mfano wa kuigwa na wabongo wote, I mean sio form six wote Tanzania wanamiliki Casino ya kimataifa kama anavyofanya, na sio Fom Six wote wanaoweza kusimama mbele ya Conventional ya Republicans kule USA na kuongea mpaka wakaeleweka na kupewa heshima ya wajumbe wote kusimama kwa dakika tano wakimshangilia, na sio viongozi wote wa Tanzania walioweza kualikwa kwenye kitu kama kile,
Ninaomba uiweke hiii argument yako in mfumo unaoweza kukubalika na wananchi wengi hapa walioenda shule, kuwa Mbowe hafai kuwa rais kwa sababu hatimizi masharti ya katiba ya Chadema, nayo ni one, two, three na pia hatimizi masharti ya katiba ya taifa, one, two, three, otherwise una-make a lot of sense na the Yanga na Simba's like arguments, ila una-fall mbali sana na serious debate far as our national politics is concerned,
Vipi ukirekebisha hilo mkuu!