Kama Mama Malecela hafai, je Mbowe anafaa?

Kama Mama Malecela hafai, je Mbowe anafaa?

CV ya Mbowe

http://www.parliament.go.tz/bunge/Mp_Cv3.asp?PTerm=2000-2005&fpkey=261&vusername=GUEST")

  1. Jamani hivi kweli hii CV ya Mbowe inafaa kuwa kiongozi nchi au wa chama au hivi vyeo tunapeana tu?
  2. Licha ya elimu ndogo, form six, experience aliyonayo ni ya ukarani tu, BOT. Je hivi vinatosha kuongoza nchi au hata chama cha siasa?
  3. Hivi akina Dr. Slaa, Zitto n.k. wamekubali vipi au wanajisikiaje kuongozwa na mtu wa elimu ya form six?
  4. Je elimu ndogo na uwezo mdogo wa Mbowe ni kikwazo kwa Chadema katika kuwabana vihiyo ndani ya CCM?
Jamani! CV by itself is not conclusive proof kuwa s/he can or cannot deliver... you need to look at cv +other parameters......wangapi wana macv ya kutisha lakini uzoefu ukawa nil?!Tuwe objective na si kuweka chuki binafsi..kama zipo...
 
1
. Kama Mama Malecela hafai, huyu je anafaa?

Kuna wana JF waliosikiliza majadiliano kati ya Mzee Mwanakijiji na Mama Anna Kilango Malecela wakavutiwa kuangalia profile ya Mama Malecela kwenye tovuti ya Bunge. Kwa bahati mbaya kuna waliomdisqualify mbunge huyu aliyeonyesha ujasiri baada ya kusoma profile yake.

2.
Originally Posted by Field Marshall ES
Mama Anne Kilango Malecela, Mbunge,

kwanza Mwalimu wa Sekondari ya Kisutu, huku akiwa mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Kionondoni, akawa Accountant ATC, akawa Senior Accountant Gulf Air, huku akiwa mmoja wa Directors wa Casino pale Sea View, akawa mbunge wa kuteuliwa na rais, baadaye akaw mbunge wa kuchaguliw na wananchi hadi sasa, pia ni mfanya biashara maarufu wa bidahaa mbali mbali toka USA na Europe, akimiliki maduka makubwa ya bidhaa hizo kati ya Dar, Dodoma, na Same, sasa hivi pia ni makamu mwenyekiti kamati ya bunge ya Miundo Mbinu, na pia mwenyekiti wa kamati ya maadili ya viongozi ya bunge,

Toka awe mbunge wa kuchaguliwa amekuwa kiongozi hodari wa kukataa ufisadi, ndiye aliyeongoza mapambano ya kumuondoa madarakani aliyekuwa Waziri Mkuu wa zamani Lowassa, baada ya hapo ndiye aliyepigana sana mpaka kuufuta mkatba wa kifisadi ulikouwepo bandarini kwa miaka kumi na ulikuwa uwepo kwa miaka 15 zaidi, akiwa kama mwenyekiti wa muda wa kamati ya Miundo Mbinu ya bunge kutokana na mwenyekiti wa kamati Ndugu Misanga, kutoweza kushiriki kikamilifu kwenye kamati hiyo kutokana na kuumwa sana ugonjwa wa kisukari, Mama mbunge pia kwa sasa yupo Chuo Kikuu Huria akimalizia Degree ya Uchumi.

Sasa mnyonge mnyongeni lakini haki apewe, ningeomba mtoa mada hii atuwekee qualifications za hao anaosema kuwa wameangalia CV ya huyu mbunge wetu wa taifa na kuona hafai, maana nina wasi wasi kuwa sio rahisi mwananchi mwenye CV ya wasi wasi kuweza kuielewa CV inayofaa au isiyofaa, au kuelewa kuwa ni kiongozi yupi anafaa na yupi hafai, halafu ikiwezekana atupe historia ya hao wanachi jinsi ambavyo wamewahi kulisaidia taifa letu na hizi hukumu, ambazo pia watuambie wamezi-base on CV za viongozi wapi hao wa taifa letu wanaofaaa!

Ninasema kuwa Mama Anne Kilango Malecela, anazo qualifications zote anazozihitaji kuwa na nafasi aliyonayo sasa, yaani mbunge wa kuchaguliwa na kuwawakilisha wananchi bungeni.

2.
Quote:- Kubwajinga

Mama Malecela ana sifa zote za kuwa kiongozi wa ngazi yoyote nchini. Lakini nafikiri nchi yetu inao wazalendo wengine wengi wenye sifa bora zaidi kwa nafasi ya uraisi.

Mkuu Kubwajinga,

Mimi ninafikiri kwa maneno yako mengi humu ndani unaonekana una shule angalua kidogo sio sana, lakini jaribu kujifunza ku-stick na topic at hand, mtoa mada hii hakusema mahali popote kuwa Mama Kilango hafai au anafaa kuwa rais, alichosema ni kuwa hafai kutokana na profile yake, sasa wewe naona umerukia urais,

On that, pamoja na kwamba sio the ishu hapa, ninasema hivi Mbunge Mama Kilango, ana haki zote kama nilizonazo mimi na raia wengine wa Tanzania, kugombea urais at any of her time, as long as anatimiza sharti kubwa la kugombea on CCM's side, ambalo ni kuwa na angalau First Degree, ila cha muhimu kuliko yote awe raia wa Tanzania,

Pia niwakumbushe wale wasiokuwa raia wa Tanzania, kuwa hata kama ulizaliwa bongo, lakini ukienda nje na kubadili passport na kuikana pass yetu ya bongo, mbele ya Mungu, wewe sasa sio raia tena wa nchi yetu, sasa sheria ziko very clear kuwa as a foreigner as you are, hutakiwi kujiingiza na siasa zetu za Tanzania, yaani local politics, ni sawa kabisa ukipigia kelele zako huko kwenye "nchi" yako mpya, lakini sio katika ardhi yetu sisi wa-Tanzania, ambao tumeamua kuwa tutakufa na ubongo wetu liwalo na liwe lakini hatutauza utu wetu.

Mama Kilango anazo qualifications zote na za kutosha kuwa kwenye nafasi aliyonayo sasa, yaani ya kuwawakilisha wananchi wa jimbo la Same East, bungeni.

Ahsante Wakuu!
 
kubwa jinga kwa faida ya mjadala rejea post ya mwisho ya nyama hatari, na fanya kama anavyofanya fmes, no wonder unapata majibu ya chooni, unahoji cv ya mbowe naamini na wewe cv yako imetulia ndo maana una ballz za kuhoji za wenzako, tumia basi kidogo hiyo elimu yako kuuliza maswali vizuri yaliyoenda shule, kama sivyo basi majibu mwafrika wa kike yanakutosha.

It doesn't take a rocket scientist to figure out that the type of "questions" you've posited earlier are what are known as "loaded" questions in the sense that these presuppose that Mr.Mbowe has insufficient and/or inferior credentials to qualify as Party Chairman and potential candidate for presidency of the Republic.

Like I said above, what appears to be much more harder for you to accomplish in this case is to lay down your argumentation(s), point-by-point, as to why Mr. Mbowe is (as you try to insinuate through your questioning here), "unqualified" and/or "unfit" to maintain his formal position as current Party Chairman or to vie for candidacy as president of the Republic in future presidential elections.

NyamaH & MaP,
What needs no rocket scientist or neural surgeon to understand 'wasiofaa kuongoza nchi' is this;

  1. If we can not allow a form six certificate holder to teach our sec school children, or be a Diocese Bishop in RC or Luth Churches, or be our embasador even in Burundi or even nowadays be an army officer because of their inferior academic knowhow, especially those who failed to get good grades to proceed to tertiary education, why should we entrust one, with similar credentials, to lead a nation??
  2. Why should a BoT clerk be given such a high leadership position by his party if it is not reasons known to the party insiders alone??
  3. Why the likes of Dr. Slaa and Zitto and many others in CHADEMA are swallowing this without even questioning?? Are they just complying in order to retain their positions or this form six stuff makes no sence to them??
Let's be honest, Mbowe is not a presidential material.
 
Let's be honest, Mbowe is not a presidential material.

Mkuu comment kubwa namna hii ni lazima iwe na side mbili accademically, au politically,

sasa vipi ukienda zaidi kama inavyotakiwa na kanuni za elimu kwa kusema as opposed to whom?
 
Mkuu Kubwajinga,

Mimi ninafikiri kwa maneno yako mengi humu ndani unaonekana una shule angalua kidogo sio sana, lakini jaribu kujifunza ku-stick na topic at hand, mtoa mada hii kausema mahlai popote kuwa Mama Kilango hafai au anafaa kuwa rais, alichosema ni kuwa hafai kutokana na profile yake, sasa wewe naona umerukia urais,

On that, pamoja na kwamba sio the ishu hapa, ninasema hivi Mbunge Mama Kilango, ana haki zote kama nilizonazo mimi na raia wengine wa Tanzania, kugombea urais at any of her time, as long as anatimiza sharti kubwa la kugombea on CCM's side, ambalo ni kuwa na angalau First Degree, ila cha muhimu kuliko yote awe raia wa Tanzania,

Pia niwakumbushe wale wasiokuwa raia wa Tanzania, kuwa hata kama ulizaliwa bongo, lakini ukienda nje na kubadili passport na kuikana pass yetu ya bongo, mbele ya Mungu, wewe sasa sio raia tena wa nchi yetu, sasa sheria ziko very clear kuwa as a foreigner as you are, hutakiwi kujiingiza na siasa zetu za Tanzania, yaani local politics, ni sawa kabisa ukipigia kelele zako huko kwenye "nchi" yako mpya, lakini sio katika ardhi yetu sisi wa-Tanzania, ambao tumeamua kuwa tutakufa na ubongo wetu liwalo na liwe lakini hatutauza utu wetu.

Mama Kilango anazo qualifications zote na za kutosha kuwa kwenye nafasi aliyonayo sasa, yaani ya kuwawakilisha wananchi wa jimbo la Same East, bungeni.

Ahsante Wakuu!

Mkuu FMES,
Hii thread nafikiri ilitokana na ile ya KLH Exclusive:Mhe Anne Kilango Malecela Alonga! ambapo suala la mama Malecela kugombea liliibuka. Kwa mfano angalia hizi links;
mvumilivu
FMES
FMES
zemarcopolo
Mzee Mwanakijiji

Kwa hiyo ni vema tukaweka mjadala in full perspective. Ndio maana nilipoona umeweka sifa zake ikabidi na mimi nitoe mawazo yangu; kuwa ni kweli ana-qualify kuwa hata raisi lakini nafikiri tunao wagombea wazuri zaidi yake humo humo ndani ya CCM na labda hata nje ya CCM.
 
Mkuu comment kubwa namna hii ni lazima iwe na side mbili accademically, au politically,

sasa vipi ukienda zaidi kama inavyotakiwa na kanuni za elimu kwa kusema as opposed to whom?

Mkuu FMES,
Kama nimekuelewa vizuri, ni kuwa, Mbowe hana qualifications zozote za kuwa kiongozi wa nchi yoyote period. Sio tu TZ bali hata zile za Kufikirika au ile ya Wagagagigikoko. Ukweli ni kuwa Mbowe hana elimu inayofaa kuongoza hata wizara au na hana hata uzoefu wowote wa ku-substitute hiyo elimu yake ndogo kama ilivyo kwa Mrema. Kwa hiyo inanishangaza sana kuona kwa nini alikodishiwa helicopter na Chadema kuzunguka nchi nzima kama mgombea uraisi wakati ni wazi kuwa hakuwa na sifa za kufanya hivyo.
 
Mkuu bado hujajibu swali langu la msingi, Mwenyekiti wa Chadema hana qualifications za urais as opposed to whom? Yaani ukimlinganisha na kiongozi yupi mwingine aliyegombea na anayetaka kugombea urais wetu?
 
Mkuu FMES,
Kama nimekuelewa vizuri, ni kuwa, Mbowe hana qualifications zozote za kuwa kiongozi wa nchi yoyote period. Sio tu TZ bali hata zile za Kufikirika au ile ya Wagagagigikoko. Ukweli ni kuwa Mbowe hana elimu inayofaa kuongoza hata wizara au na hana hata uzoefu wowote wa ku-substitute hiyo elimu yake ndogo kama ilivyo kwa Mrema. Kwa hiyo inanishangaza sana kuona kwa nini alikodishiwa helicopter na Chadema kuzunguka nchi nzima kama mgombea uraisi wakati ni wazi kuwa hakuwa na sifa za kufanya hivyo.

kwa watu wenye chuki za kikabila na kidini kama wewe, Mbowe hana sifa za kuongoza kwa vile wewe unaangalia kabila na dini ili kuchagua viongozi. Chini ya Mbowe chadema imeipiku nccr, tlp na hata cuf kwa umaarufu Tanzania bara na idadi ya wabunge huko bara. Uongozi unapimwa kwa vitendo na sio dini na kabila kama wewe unavyofanya kila mara.

Hayo ya elimu, nitakukumbusha tu kuwa sio elimu pekee inayozaa kiongozi mzuri kwani kuna msemo kuwa viongozi wengi hawatengenezwi bali huzaliwa (most leaders are not made, they are born).
 
Shule nimemaliza,Elimu nimeipata,
Jambo moja latatiza,Maisha takayopata,
Mimi ni Kijana hasa,Maisha natapatapa,
Lakini Kilimo sitaki,Hiyo kazi ya kishamba.

Shughuli zimejazana,Siasa ndiyo kazi,
Mimi naepukana,kuona kilimo kazi
Hiyo kazi ya watwana,na tena hawajiwezi
Washamba na walime,Na mimi nilime,hata?

Siasa na ikigoma,naanza kazi si adili
Hii haina huruma,hiyo kazi si adili
Kwa baba au mama,ukimbana hana akili.
Lazima niwe fisadi,maana huu unalipa.

"Watanzania wengi mabuku wamebukua lakini kwa nini leo tupo hapa tulipo?
Hizi elimu zetu kwenye siasa za TZ haziwezi kuzaa matunda bila kurekebisha au kuondoa mfumo wa umangimeza ambao unawapeleka viongozi magogoni.
"Hivi ndivyo katiba isemavyo,sasa hapo sijui wenye mashahada ya uzamili na uzamivu sifa zao ziwekwe fungu gani?
39.-(1) Mtu hatastahili kuchaguliwa kushika kiti cha Rais wa
Jamhuri ya Muungano isipokuwa tu kama-
(a) ni raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano kwa
mujibu wa Sheria ya Uraia.
(b) ametimiza umri wa miaka arobaini;
(c) ni mwanachama, na mgombea aliyependekezwa na
chama cha siasa;
(d) anazo sifa za kumwezesha kuwa Mbunge au Mjumbe
wa Baraza la Wawakilishi,
(e) katika kipindi cha miaka mitano kabla ya tarehe ya
Uchaguzi Mkuu hajawahi kutiwa hatiani katika
Mahakama yoyote kwa kosa lolote la kukwepa kulipa
kodi yoyote ya Serikali.

_________________________________________________________________
33
(2) Bila ya kuingilia haki na uhuru wa mtu kuwa na maoni
yake, kuamini dini atakayo, kushirikiana na wengine na kushiriki
shughuli za umma kwa mujibu wa sheria za nchi, mtu yeyote
hatakuwa na sifa za kuchaguliwa kushika kiti cha Rais wa
Jamhuri ya Muungano kama si mwananchama na mgombea
aliyependekezwa na chama cha siasa.
[/COLOR]
 
Kama nimekuelewa vizuri, ni kuwa, Mbowe hana qualifications zozote za kuwa kiongozi wa nchi yoyote period.

Mkuu mimi ni CCM damu, lakini pia ninachelea sana maendeleo ya taifa letu, la Tanzania ambalo ndilo linalopaswa kuwa mbele kabla ya sifa za wagombea na vyama vyao, meaning kwamba ni lazima kwanza qualifications ziambatane na mahitaji ya nchi yetu na wakati wake,

So far binafsi ninaamini kuwa ni marais wetu wawili tu waliopita waliowahi ku-fit kwenye hili, yaani Mwalimu kututoa chini ya wakoloni na kutuweka to the next level, halafu Mwinyi, kutupeleka kwenye demokrasia inagawa ya kiduchu, lakini si haba sasa tuna uhuru wa kusema, Mkapa alikuwa na all the pontetials kuuurekebisha uchumi, lakini kwa bahati mbaya ni kuwa aliutengeneza uchumi kwa faida ya familia yake na marafiki zake, badala ya taifa,

Mwenyekiti wa Chadema wa sasa, ameipokea Chadema ikiwa almost dead, kama sio kuelekea kufa, ameweza kuipa meno mpaka imeweza kuwavuta viongozi imara wa taifa sasa kama kina Zitto, Dr. Slaaa, Wangwe na wengineo kama kina Mnyika, ambao giveni a choice between CCM, NCCR na TLP, au CUF, waliamua kuwa Chadema under Mbowe ndio inayofaa wao kuwemo, ninaamini kuwa anazo qualifications zote zinazotakiwa na Chadema kuwa mgombea wao wa urais, mimi ningeheshimu hoja zako kama zingekuwa zina-base na katiba ya Chadema kutokuwa fullfilled, au za taifa letu, lakini kama anaridhisha katiba za Chadema na Taifa, which ninaamini he does, sielewi the base hasa ya your argument kuanzia kisiasa na kisheria,

Binafsi ninaamini kuwa anao uwezo wa kuwa rais wa Tanzania, hasa kwa wakati huu ambao tuna matatizo ya Respect kwa Rule of Law, tunahitaji kiongozi imara anayeweza ku-up hold sheria zetu, mafanikio ya binafsi kibiashara ya Mbowe ni mfano wa kuigwa na wabongo wote, I mean sio form six wote Tanzania wanamiliki Casino ya kimataifa kama anavyofanya, na sio Fom Six wote wanaoweza kusimama mbele ya Conventional ya Republicans kule USA na kuongea mpaka wakaeleweka na kupewa heshima ya wajumbe wote kusimama kwa dakika tano wakimshangilia, na sio viongozi wote wa Tanzania walioweza kualikwa kwenye kitu kama kile,

Ninaomba uiweke hiii argument yako in mfumo unaoweza kukubalika na wananchi wengi hapa walioenda shule, kuwa Mbowe hafai kuwa rais kwa sababu hatimizi masharti ya katiba ya Chadema, nayo ni one, two, three na pia hatimizi masharti ya katiba ya taifa, one, two, three, otherwise una-make a lot of sense na the Yanga na Simba's like arguments, ila una-fall mbali sana na serious debate far as our national politics is concerned,

Vipi ukirekebisha hilo mkuu!
 
39.-(1) Mtu hatastahili kuchaguliwa kushika kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano isipokuwa tu kama-

(e) katika kipindi cha miaka mitano kabla ya tarehe ya Uchaguzi Mkuu hajawahi kutiwa hatiani katika Mahakama yoyote kwa kosa lolote la kukwepa kulipa kodi yoyote ya Serikali.

Hilo ndilo kosa kubwa kuliko yote unaloweza kuitendea Serikali?
 
39.-(1) Mtu hatastahili kuchaguliwa kushika kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano isipokuwa tu kama-

(e) katika kipindi cha miaka mitano kabla ya tarehe ya Uchaguzi Mkuu hajawahi kutiwa hatiani katika Mahakama yoyote kwa kosa lolote la kukwepa kulipa kodi yoyote ya Serikali.

Je Mwenyekiti wa Chadema wa sasa, ambaye ndiye aliyekuwa mgombea wao wa urais, anahusika in anyway na hii article hapo juu? au?
 
Je Mwenyekiti wa Chadema wa sasa, ambaye ndiye aliyekuwa mgombea wao wa urais, anahusika in anyway na hii article hapo juu? au?

Hapana. Hili halikuhusiana sana na mada ya Mbowe, bali masharti ya kugombea Urais kwa ujumla. Samahani.

Huwa sielewi hicho kipengele kina umuhimu gani, kwa sababu Katiba inasema kuna makosa mengine makubwa kuliko kutolipa kodi.

Kwa mtaji wa kipengele hicho, mtu akifanya Uhaini -ambalo ndilo kosa kubwa kuliko yote kikatiba - lakini kalipa kodi, basi anaweza kuwa Rais. Haileti mantiki.

Samahani tena.
 
kazi nzuri wazee, elimu ya chuo kikuu inahitajika sana kwa mtu anayetaka kuwa raisi. Inabidi watanzania waachane na watu ambao hawajasoma kama hawa.

Elimu ni muhimu kuliko mengine yoyote yale.

kwanza mara zote huwa nashikwa na mshangao kuhusu tafsiri ya kikasuku ya watu wengi kuhusu elimu. Elimu siyo kujua kiingereza au kuwa na shahada ya chuo kikuu. Elimu ni mtaji wa kifalsafa alionao mtu katika kupambanua mambo na kutafsiri hali ya mambo katika mazingira yake na kutafuta ufumbuzi kwa yale mambo yenye utata kwa njia mjarabu!

Lakini kwa taratibu za dunia wakati fulani ukawekwa utaratibu wa kupima ufahamu wa watu ili kuwa kigezo cha watu hao kuajiriwa na watu wengine,na mwanzoni kabisa waliowathibitisha hawakuwa ni waalimu waliotambuliwa na jamii nzima,na hapo ndipo usomi ulipoanza

wale wenye maarifa kama kina Plato na wenzie walitumia njia maalum ya kupenyeza maarifa yao kwa watu wengine na wala kwa mastaajabu siyo wao wasomi na wanafalsafa wakubwa waliogundua sanaa ya uandishi,wagunduzi wa sanaa hii ya uandishi ni watu wa kawaida kabisa ambao kwa leo hii tungewaita "hakusoma!

Nakubalina na kwamba Mbowe inawezekana si msomi lakini kusema hana elimu si kweli kwa sababu unaposema mtu hana elimu ni mawanda mapana sana. Hana elimu ya nini? Nafikiri tunaweza kusema kwamba Mbowe hakusoma mpaka kupewa shahada ya chuo kikuu katika fani yoyote ile!

Maana usomi una mikogo lakini elimu hutambuliwa na jamii. Kama mtu ni msomi wa uchumi hiyo siyo sifa pekee ya kuwa rais anayefaa kuongoza nchi. Huyu msomi wa uchumi inawezekana kabisa kwamba hana alijualo kuhusu mahusiano ya kimataifa sasa tutamfanyaje?

Nafikiri elimu yetu isiwe kwa vigezo vya kisomi bali viwe kwa jinsi ya mtu anavyoweza kuchambua mambo. Mpaka sasa kuna watu wako vyuo vikuu mbalimbali wanasoma kuhusu Shaaban Robert au Chalie Chaplin, hawa wawili walikuwa na digrii ngapi? na Jee Jacob Zuma anayetarajiwa kuwa Rais wa Afrika kusini amesoma kwa kiwango gani?

Sitetei ujinga bali naamini kwamba usomi siyo kigezo cha kuwa na elimu na siyo wasiosoma hawana elimu. nina mifano lukuki ya watu wenye Phd ambao ukikaa nao au ukisoma tafakuri zao kuhusu ulimwengu wetu utakuta "madudu" matupu!
 
Mkuu mimi ni CCM damu, lakini pia ninachelea sana maendeleo ya taifa letu, la Tanzania ambalo ndilo linalopaswa kuwa mbele kabla ya sifa za wagombea na vyama vyao, meaning kwamba ni lazima kwanza qualifications ziambatane na mahitaji ya nchi yetu na wakati wake,

So far binafsi ninaamini kuwa ni marais wetu wawili tu waliopita waliowahi ku-fit kwenye hili, yaani Mwalimu kututoa chini ya wakoloni na kutuweka to the next level, halafu Mwinyi, kutupeleka kwenye demokrasia inagawa ya kiduchu, lakini si haba sasa tuna uhuru wa kusema, Mkapa alikuwa na all the pontetials kuuurekebisha uchumi, lakini kwa bahati mbaya ni kuwa aliutengeneza uchumi kwa faida ya familia yake na marafiki zake, badala ya taifa,

Mwenyekiti wa Chadema wa sasa, ameipokea Chadema ikiwa almost dead, kama sio kuelekea kufa, ameweza kuipa meno mpaka imeweza kuwavuta viongozi imara wa taifa sasa kama kina Zitto, Dr. Slaaa, Wangwe na wengineo kama kina Mnyika, ambao giveni a choice between CCM, NCCR na TLP, au CUF, waliamua kuwa Chadema under Mbowe ndio inayofaa wao kuwemo, ninaamini kuwa anazo qualifications zote zinazotakiwa na Chadema kuwa mgombea wao wa urais, mimi ningeheshimu hoja zako kama zingekuwa zina-base na katiba ya Chadema kutokuwa fullfilled, au za taifa letu, lakini kama anaridhisha katiba za Chadema na Taifa, which ninaamini he does, sielewi the base hasa ya your argument kuanzia kisiasa na kisheria,

Binafsi ninaamini kuwa anao uwezo wa kuwa rais wa Tanzania, hasa kwa wakati huu ambao tuna matatizo ya Respect kwa Rule of Law, tunahitaji kiongozi imara anayeweza ku-up hold sheria zetu, mafanikio ya binafsi kibiashara ya Mbowe ni mfano wa kuigwa na wabongo wote, I mean sio form six wote Tanzania wanamiliki Casino ya kimataifa kama anavyofanya, na sio Fom Six wote wanaoweza kusimama mbele ya Conventional ya Republicans kule USA na kuongea mpaka wakaeleweka na kupewa heshima ya wajumbe wote kusimama kwa dakika tano wakimshangilia, na sio viongozi wote wa Tanzania walioweza kualikwa kwenye kitu kama kile,

Ninaomba uiweke hiii argument yako in mfumo unaoweza kukubalika na wananchi wengi hapa walioenda shule, kuwa Mbowe hafai kuwa rais kwa sababu hatimizi masharti ya katiba ya Chadema, nayo ni one, two, three na pia hatimizi masharti ya katiba ya taifa, one, two, three, otherwise una-make a lot of sense na the Yanga na Simba's like arguments, ila una-fall mbali sana na serious debate far as our national politics is concerned,

Vipi ukirekebisha hilo mkuu!

Mkuu FMES,
Uwezo wa kumvuta Zitto kwenye Chadema n.k., sio dalili ya mtu kuwa na ubavu wa kuwa raisi. Uraisi unahitaji kusoma ripoti mbalimbali na kupitisha maamuzi makubwa ya kitaifa na kimataifa. Sasa kama shule ndogo ya digirii ya kwanza imemshinda Mbowe kule UK na wala sio UDSM, ataweza vipi kuiendesha serikali ngumu ya TZ?

Kama ni kuiongoza Chadema kwa sasa hivi, hiyo haina tofauti na ukiranja mkuu, maana bado Chadema ni kundi dogo linalotegemea familia fulani-fulani, hasa baba mkwe wake Mbowe na rafiki yake Ndesamburo. Na ndio maana labda hiyo form six yake inafaa katika uongozi wa Chadema. Lakini sifa zake hazifai kabisa kuibeba nchi yenye watu wanaojua mambo 10 times ya yeye. Hata akiiba si atasema katapeliwa kwa kuwa elimu yake ni ndogo??
 
kwanza mara zote huwa nashikwa na mshangao kuhusu tafsiri ya kikasuku ya watu wengi kuhusu elimu. Elimu siyo kujua kiingereza au kuwa na shahada ya chuo kikuu. Elimu ni mtaji wa kifalsafa alionao mtu katika kupambanua mambo na kutafsiri hali ya mambo katika mazingira yake na kutafuta ufumbuzi kwa yale mambo yenye utata kwa njia mjarabu!

Lakini kwa taratibu za dunia wakati fulani ukawekwa utaratibu wa kupima ufahamu wa watu ili kuwa kigezo cha watu hao kuajiriwa na watu wengine,na mwanzoni kabisa waliowathibitisha hawakuwa ni waalimu waliotambuliwa na jamii nzima,na hapo ndipo usomi ulipoanza

wale wenye maarifa kama kina Plato na wenzie walitumia njia maalum ya kupenyeza maarifa yao kwa watu wengine na wala kwa mastaajabu siyo wao wasomi na wanafalsafa wakubwa waliogundua sanaa ya uandishi,wagunduzi wa sanaa hii ya uandishi ni watu wa kawaida kabisa ambao kwa leo hii tungewaita "hakusoma!

Nakubalina na kwamba Mbowe inawezekana si msomi lakini kusema hana elimu si kweli kwa sababu unaposema mtu hana elimu ni mawanda mapana sana. Hana elimu ya nini? Nafikiri tunaweza kusema kwamba Mbowe hakusoma mpaka kupewa shahada ya chuo kikuu katika fani yoyote ile!

Maana usomi una mikogo lakini elimu hutambuliwa na jamii. Kama mtu ni msomi wa uchumi hiyo siyo sifa pekee ya kuwa rais anayefaa kuongoza nchi. Huyu msomi wa uchumi inawezekana kabisa kwamba hana alijualo kuhusu mahusiano ya kimataifa sasa tutamfanyaje?

Nafikiri elimu yetu isiwe kwa vigezo vya kisomi bali viwe kwa jinsi ya mtu anavyoweza kuchambua mambo. Mpaka sasa kuna watu wako vyuo vikuu mbalimbali wanasoma kuhusu Shaaban Robert au Chalie Chaplin, hawa wawili walikuwa na digrii ngapi? na Jee Jacob Zuma anayetarajiwa kuwa Rais wa Afrika kusini amesoma kwa kiwango gani?

Sitetei ujinga bali naamini kwamba usomi siyo kigezo cha kuwa na elimu na siyo wasiosoma hawana elimu. nina mifano lukuki ya watu wenye Phd ambao ukikaa nao au ukisoma tafakuri zao kuhusu ulimwengu wetu utakuta "madudu" matupu!

Mkuu Kiga,
Hapa naona umetetea ujinga. Ni vema ukaelewa tofauti ya kuelimika, uwezo wa kujieleza na mtu kuwa na busara. Ukiwa na vyote vitatu unakuwa Clinton, Obama, Nyerere n.k., Ukiwa na busara na elimu kiasi unakuwa Mzee Rukhsa, Kenyata, n.k., ukiwa na elimu tu unakuwa kama Prof. Sarungi, ukiwa na mdomo mkubwa tu unaweza ukawa kama Mrema, Samuel Doe, Iddi Amin n.k.

Mdomo mkubwa utakuwezesha ku-mobilize watu lakini inapokuja masuala yanayohitaji kusoma ripoti na kutoa maamuzi, unakimbia kama alivyofanya Mbowe kule chuo UK.
 
Mdomo mkubwa utakuwezesha ku-mobilize watu lakini inapokuja masuala yanayohitaji kusoma ripoti na kutoa maamuzi, unakimbia kama alivyofanya Mbowe kule chuo UK.

say whaaat ???? yakhe naona hapo umebonyeza kisawasawa ! maana hakuna chembe ya uongo hata kidogo yakhe !
Kama mbowe kakimbia shule, kuongoza watanzania ataweza vipi ?
 
say whaaat ???? yakhe naona hapo umebonyeza kisawasawa ! maana hakuna chembe ya uongo hata kidogo yakhe !
Kama mbowe kakimbia shule, kuongoza watanzania ataweza vipi ?

Yakhe Kada,
Umesema sawia kabisa kuwa ukweli inabidi tuuongee. Uwezo wa kubwabwaja sio ubora wa uongozi. Kama mtu alikimbia umande ni vema akakabiliana na matokeo yake na sio kutumia wakwe zake ili kujipatia madaraka asiyoyaweza. Nilishasema hapo awali kuwa Mbowe anafaa sana kuwa mpiga debe wa wagombea wengine, kama akina Slaa, Zitto, Lipumba n.k., lakini sio yeye kutaka asiyoyaweza. Mbowe anatakiwa atambuelimit ya uwezo wake kiuongozi kutokana na uwezo wake mdogo kielimu na uzoefu.
 
Baada ya mjadala huu kuendelea kwa muda mrefu naomba nitoe tamko la mwisho baada ya kupima maoni ya wana JF.

Mbowe hafai kuongoza nchi ya Tanzania, ujumbe kwake ni kwamba asijitokeze tena katika uchaguzi mkuu ujao kama mgombea. Kwa vile amejaliwa kipaji cha kuongea basi ni vyema akitumie kipaji hicho kuwanadi wagombea wengine wa Chama chake au wa upinzani kwa ujumla.

Mama Malecela anafaa kuwa kiongozi wa nafasi aliyo nayo sasa ya ubunge. Iwapo ana mikakati ya kugombea urais ni vyema atumie muda huu kujiimarisha kielimu na kisiasa.

Mods, mjadala unaweza kufungwa.
 
Back
Top Bottom