Membe S K
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 1,389
- 1,253
Uwezo wa kubwabwaja sio ubora wa uongozi.
Hii quote nimeipenda,
Mimi nadhani Mbowe ni kiongozi mzuri ila mapungufu ya kielimu ni drawback kubwa ingawa wengi wetu tutaikataa. Nadhani Mbowe anahitaji elimu zaidi kuliko urais.
Lazima tukubali kwamba elimu ni muhimu kwa viongozi wa karne hii. Ila nimeona wachangiaji wengi wakichanganya mapera na maembe hapa. Elimu sio sawa na maadili ya uongozi, ni bora hili likaeleweka. Kiongozi anaweza akaelimika na kukosa maadili, au akawa hana elimu ila akawa na maadili. kiongozi bora ni yule mwenye yote mawili (elimu na maadili), kama kimoja kinakosekana basi huyo "hafai" miongoni mwa walio na vitu hivyo viwili. Na ndio maana hata founder wa politics Pilato, anakubali kwamba 'kings should be philosophers and philosophers should be kings', akiwa na maana kwamba viongozi (kings) lazima waelimike na walio elimika (philosophers) ndio wafanywe kuwa viongozi.
Kwa mantiki hii, umuhimu wa elimu kwa viongozi ni sawa na umuhimu wa maadili ya uongozi. Swali linakuja katika kiwango cha elimu vs kiwango cha maadili. Kama jamii inakubali kiwango cha form six kuwa ni kiwango sahihi kwa kiongozi basi Mbowe ana qualify, la sivyo ipo haja ya Mbowe kuongeza elimu.