Kama Mama Malecela hafai, je Mbowe anafaa?

Kama Mama Malecela hafai, je Mbowe anafaa?

Hiyo form six kwanza ya division ngapi?
Mbowe kwa kupigia debe daladala pale kariakoo ahha apo anafaa.
Huyu opportunist, tapeli mkubwa, leo anajifanya anauchungu na nchi.

Nadhani hapa mkuu umevuka mpaka. Ni bora tukajadiri elimu ya Mbowe na suitability ya kuwa rais wetu....kuitana majina na kejeli hakujengi hoja badala yake kunabomoa hata zile hoja mzuri.
 
Hiyo big Casino unayoizungumzia iko wapi?, au unamanisha ukumbi wa musiki billicanas. Je unajua ameupataje ? kama ni urithi au utapeli je?

Unajua kwa kawaida huwa sipendi debate na mtu kama wewe, kwa sababu nyingi sana ambazo sitazisema, lakini kwa leo nitakujibu, maana sasa unatoka kwenye elimu na kukimbilia kwenye Casino, okay:-

1. Anayoimiliki Mbowe ni Casino, tena ya kimataifa sio tu Club peke yake, halafu uende hazina, uwaulize taifa letu linapata kodi kiasi gani pale yaani Bilicanas, ningekuelewa kama wewe ungekuwa nazo kama kumi zile Bilicanas, na kwamba wabongo wote waliomaliza Form Six wanazo hizo Bilicanas type of Casinos,

2. Mkuu I grew up with the guy, nimemuona akisoma Ihungo, akipanda treni kwenda shule, wakati huo Mbowe Hotels ikiendeshwa na kaka yake Marx, baadaye ilikuwa under Sudi Space 19000, ndipo Freeman aliporudi kutoka shule na kuanza kufanya kazi BOT, huku akijishughulisha na Hotel ikiwa ni pamoja na kusafirisha Mananasi kupeleka Uarabuni, haikupita muda mkuu akaenda Uk na kununua vyombo vyake vya kisasa vya Disco, kabla hajarudi mjini Sudi na kundi lake wakaahamia Margott, na Freeman akafungua rasmi Disco lake la RSVP pale Mbowe Hotels na ndio kwa mara ya kwanza Marehemu Baba yake anamuachia kuiendesha ile Hotel, Disco na Guest House, huku Free akiendelea na kupeleka mananasi Uarabuni tena sasa akikodi ndege nzima, this is in the late 80s,

Mwanzoni mwa 90s, Free akaamua kuiongeza na kuwa Casino na Club, ni hii renovation ndiyo iliyompa nafasi Mkuu wangu Joe Kusaga, kuweka vyombo vyake vya nyumbani pale Motel Agip as an alternative ya kufungwa kwa matengenezo kwa Mbowe Hotels, na mpaka Joe kuhamia Leaders club na kuchana mpaka leo Clouds Prime Time, hatimaye Free kufungua tena sasa ikiwa Casino, sio Hotel tu, tena this time ikawa na Hard-Rock Cafee, sasa haya yote ameyafanya akiwa mbongo wa kwanza, hakuna urithi wala utapeli mkuu, kuna tulioshuhudia all this mkuu, na hatutasita kusema ukweli,

3. Now back to the ishu ya elimu yake, mimi ninasema kuwa it took Hitler na whatever he was, kuikomboa Germany to what Germany is today, tumekuwa na viongozi wengi wenye elimu kubwa, na ndio waliotufikisha hapa tulipo, sasa wakati umefika kwa wabongo kukaa chini na kukubali kuwa viongozi wote waliotangulia wametufikisha pabaya, pamoja na elimu zao zote kubwa,

Sasa ni wakati wa kuwapa viongozi wapya nafasi, Mtikila na elimu yake suspect ndiye aliyekwenda kusimama mahakamani na kudai wagombea Independent, Sokoine na elimu yake ya Suspect ndiye aliyetuletea Dala Dala, na yote haya sio siri kuwa ni muhimu kwa taifa letu, kulinganisha na Mkapa kujipa mgodi wa Kiwira, Tanzania tunahitaji kiongozi imara anayeweza kusimamia haki na sheria zetu za jamhuri,

Ninasema hivi waliotangulia wote wameshindwa kutuongoza, sasa sisi wananchi tufikie mahali tukubali kuwa uwezo wa kujua nani anafaa kuwa kiongozi bora au hafai, ni kwamba hatunao huo uwezo, maana tungekuwa nao, basi tusingefika hapa tulipo as a nation, sasa tutakuwa majuha kuanza kusema Freeman hafai kwa sababu ni form six,

mimi nilifikiri toka mwanzo kuwa mnajaribu kujenga an-accademic paper like, yaani kama research kujaribu kuonyesha viongozi wasomi wa bongo na viongozi wasiokuwa na elimu kubwa bongo, uzuri na madhara yao, lakini ninashangaa baadhi ya watu hapa mnaojaribu kutuonyehsa kuwa ni wasomi kwa kufikia hata kuandika na kujijibu kwa English mtu huyo huyo, lakini mnashindwa kutuelimisha tuisokuwa na elimu exactly mnachoongelea ni nini hasa? Maana ni viugmu kuelewa either mna chuki na Freeman as a person au Chadema, maana sioni a strong argument ya shule hapa so far kuhusu elimu ya Mbowe na uongozi wetu wa taifa,

Jaribuni kujipanga tena wakuu, ili mlisaidie taifa kwa kuweka elimu nzito on this ishu maana inaweza kuwa ni muhimu sana kwa taifa kuwa na ukweli wa kisayansi on this, Chadema imekuwaje juu nationally under Freeman, Freeman aliwezaje ku-secure misaada mikubwa kwa Chadema kutoka nje ya nchi kuliko viongozi wasomi waliotangulia huko Chadema? Kwa nini under Freeman Chadema imekuwa ya pili toka kwa CCM, na haikuwa hivyo before I mean toka ianzishwe?

Sasa wakuu kama kweli tunaitakia mema taifa letu basi tuwe wakweli, kuliko kujaribu kuleta character assasination, na kujaribu kuturushia kashafa na maneno yasiyofaa tunaouliza the vlidility ya hoja zenu.

Ahsante Wakuu!
 
Jaribuni kujipanga tena wakuu, ili mlisaidie taifa kwa kuweka elimu nzito on this ishu maana inaweza kuwa ni muhimu sana kwa taifa kuwa na ukweli wa kisayansi on this, Chadema imekuwaje juu nationally under Freeman, Freeman aliwezaje ku-secure misaada mikubwa kwa Chadema kutoka nje ya nchi kuliko viongozi wasomi waliotangulia huko Chadema? Kwa nini under Freeman Chadema imekuwa ya pili toka kwa CCM, na haikuwa hivyo before I mean toka ianzishwe?

FMES asante kwa maelezo yako marefu ila naomba tupitie tena kipengele cha CHADEMA kuwa chama cha pili.

Ukilinganisha na CUF, CHADEMA haina wabunge wengi zaidi, haina wanachama wengi zaidi, haijawahi kuwa na mgombea Urais aliyepata kura nyingi zaidi. Wewe umetumia kigezo gani kuona kuwa CHADEMA ndio ya pili?

Tukikamilisha swala hili kuna swala la Mbowe kuleta misaada mingi zaidi kwa CHADEMA toka nje ya nchi.
 
kuna mtu anajua namba ya wabunge wa upinzani wa Tanzania bara kwa mgawanyo wa vyama?
 
FMES asante kwa maelezo yako marefu ila naomba tupitie tena kipengele cha CHADEMA kuwa chama cha pili.

Ukilinganisha na CUF, CHADEMA haina wabunge wengi zaidi, haina wanachama wengi zaidi, haijawahi kuwa na mgombea Urais aliyepata kura nyingi zaidi. Wewe umetumia kigezo gani kuona kuwa CHADEMA ndio ya pili?

Tukikamilisha swala hili kuna swala la Mbowe kuleta misaada mingi zaidi kwa CHADEMA toka nje ya nchi.

chama cha pili,? hahaaa..... subiri nchukue bigi jii ntafune !
 
Mkuu CUF ni chama cha Visiwani, ninajua kuwa Chadema ndio inayopata ruzuku kubwa kutoka kwa serikali yetu kutoka bara, lakini hiyo sio the ishu, the ishu eilmu ya viongozi wetu wa taifa.
 
Mkuu CUF ni chama cha Visiwani, ninajua kuwa Chadema ndio inayopata ruzuku kubwa kutoka kwa serikali yetu kutoka bara, lakini hiyo sio the ishu, the ishu eilmu ya viongozi wetu wa taifa.

Nimekupata....lakini am having a hard time, kuelewa umetumia vigezo gani kudetermine chadema ndio chama cha pili...kwani chama cha kwanza ni chama kipi hicho ? ningependa kujua hivyo vigezo na mie nifaidike mzazi !

Na pia ningependa kukusahihisha kwa kutoa misleading statement, CUF SIO CHAMA CHA KISIWANI ! this is way below mzee.....(chama cha kisiwani in terms of....??)..je vipi ni vyama vya bara ? ....navyo ni vyama vya bara in terms of....?
 
Mkuu CUF ni chama cha Visiwani, ninajua kuwa Chadema ndio inayopata ruzuku kubwa kutoka kwa serikali yetu kutoka bara, lakini hiyo sio the ishu, the ishu eilmu ya viongozi wetu wa taifa.

Ngoja FMES ni muhimu tuweke records straight. CUF sio chama cha visiwani! Tangu lini kuna vyama vya visiwani na vya Bara, na CHADEMA cha wapi, bara?

CUF ndio chama cha upinzani chenye wabunge wengi zaidi na ndio chama pekee cha upinzani chenye wawakilishi Zanzibar. Na ndio chama kinachopata ruzuku kubwa zaidi.Hivyo basi iwapo tuna hamu ya kuzungumzia kuwepo kwa chama cha pili basi chama hicho kwa sasa ni CUF na si CHADEMA.

Samahani kwa kwenda nje ya mada ya shule ya viongozi. Kumekuwa na haja ya kurekebisha records kabla hatujaendelea.
 
Mkuu the ishu ni elimu ya viongozi wetu, sio ruzuku ninasema kuwa Chadema ndio chama kinachopewa hela nyingi na taifa letu kwa upande wa bara, mimi sijawahi kuihesabu CUF kuwa ni chama cha Bara, regardless lakini huo ni mtizamo wangu, lakini the ishu hapa ni elimu sio ruzuku bro!
 
Nimekupata....lakini am having a hard time, kuelewa umetumia vigezo gani kudetermine chadema ndio chama cha pili...kwani chama cha kwanza ni chama kipi hicho ? ningependa kujua hivyo vigezo na mie nifaidike mzazi !

Na pia ningependa kukusahihisha kwa kutoa misleading statement, CUF SIO CHAMA CHA KISIWANI ! this is way below mzee.....(chama cha kisiwani in terms of....??)..je vipi ni vyama vya bara ? ....navyo ni vyama vya bara in terms of....?

Of course kada hata wewe unajua kuwa chama cha kwanza ni ccm. CUF ni chama cha visiwani maana hawana mbunge yoyote bara, kwa upande wa bara kama sikosei, chadema ni wa pili baada ya ccm (sina hakika kwa hili).

Hata hao chadema ukiwaangalia ni chama cha kabila moja tu so is tlp na nccr mageuzi. upinzani kwa kweli Tanzania bado sana kama vyama vikubwa vyote ni vya watu wa kabila moja au sehemu moja ya Tanzania.
 
Ngoja FMES ni muhimu tuweke records straight. CUF sio chama cha visiwani! Tangu lini kuna vyama vya visiwani na vya Bara, na CHADEMA cha wapi, bara?

CUF ndio chama cha upinzani chenye wabunge wengi zaidi na ndio chama pekee cha upinzani chenye wawakilishi Zanzibar. Na ndio chama kinachopata ruzuku kubwa zaidi.Hivyo basi iwapo tuna hamu ya kuzungumzia kuwepo kwa chama cha pili basi chama hicho kwa sasa ni CUF na si CHADEMA.

Samahani kwa kwenda nje ya mada ya shule ya viongozi. Kumekuwa na haja ya kurekebisha records kabla hatujaendelea.

right on mzee !
 
Of course kada hata wewe unajua kuwa chama cha kwanza ni ccm. CUF ni chama cha visiwani maana hawana mbunge yoyote bara, kwa upande wa bara kama sikosei, chadema ni wa pili baada ya ccm (sina hakika kwa hili).

Hata hao chadema ukiwaangalia ni chama cha kabila moja tu so is tlp na nccr mageuzi. upinzani kwa kweli Tanzania bado sana kama vyama vikubwa vyote ni vya watu wa kabila moja au sehemu moja ya Tanzania.

nafikiri tukiamua kuanza kuweka vyama kwenye categories, kuna vyama vya visiwani, bara na vile vya ukabila ! thats if tukiamua kufanya hivyo !
 
nafikiri tukiamua kuanza kuweka vyama kwenye categories, kuna vyama vya visiwani, bara na vile vya ukabila ! thats if tukiamua kufanya hivyo !

Sawasawa unachosema maana tutaendelea na kusema kuwa UDP ni chama cha Bariadi Mashariki!!!
 
Ninarudia tena mkuu kwangu binafsi CUf inakiona kuwa chama cha visiwani, ingawa ninajua kisheria ni chama Tanzania, lakini haibadili ukweli kwamba wabunge wake karibu wote ni wa visiwani, lakini ninasema kuwa thta is not the ishu the ishu ni elimu ya viongozi wetu, kama ya Mbowe haifai ni vyema mkaweka ya viongozi waliowahji kutufaa as a nation!
 
...Mtikila na elimu yake suspect ndiye aliyekwenda kusimama mahakamani na kudai wagombea Independent, Sokoine na elimu yake ya Suspect ndiye aliyetuletea Dala Dala...

Hivi Mtikila elimu yake ni nini hasa? Kuna gazeti moja uchwara la IPP Media limeripoti siku chache za nyuma kwamba ni Mwanasheria. Lakini haijulikani amesomea wapi. Sijawahi kuona mtu ameshwalisha Elimu ya Mtikila.

Pia sikufahamu kwamba ni Sokoine ndio alituletea Dala Dala. Ni kitendo cha kijasiri mno kuruhusu ubinafsishaji wa nyanja za Uchumi za Usafirishaji wakati wa Nyerere. Ni kama vile alimwambia Nyerere, Mzee haya makampuni yako ya Ujamaa na Kujitegemea ya UDA na KAMATA yanafeli. Ruhusu watu wamiliki vyombo vya uchumi. Alichapa kibao kwenye uso wa Nyerere, na Azimio la Arusha.

Hata hivyo, kama ambavyo tunaungana mkono pale tukikubaliana, tukikosea pia tutakosoana.

Uchambuzi wako wa Adolf Hitler una mushkeli. Hakuna wachambuzi wanaoheshimika wanaosema Ujerumani ya leo ni kazi ya Hitler. Hitler aliua wasomi, isipokuwa watengeneza mabomu. Mabomu yakazaa vita, vita vyenyewe wakashindwa, na li nchi likabomolewa na washindi wa vita. Wasomi wa Kiyahudi wakaanza mbele. Ujerumani ikaanza kujengwa upya baada ya Hitler kuondoka.

Ujerumani ilijengwa tena na mifumo mipya ya Ujamaa wa Masoko ya Kiuchumi (Social Market Economy) kuanzia katikati miaka ya 40 mpaka mwishoni wa miaka ya 50. Tofauti na mifumo ya Kidekta chini ya mawazo ya Hitler, mifumo hii mipya ilihurisha uchumi wa Ujerumani, ikiwa ni pamoja na kufungua milango ya mashindano, kuruhusu masoko huria, pamoja na biashara ya nje. Hilter hasifiki kwa hayo. Kile anachosifika kwa kukijenga wakati wa utawala wake alikivunja kwa mawazo na mwamko wake wa kivita vita.

Ahsante.
 
Ninarudia tena mkuu kwangu binafsi CUf inakiona kuwa chama cha visiwani, ingawa ninajua kisheria ni chama Tanzania, lakini haibadili ukweli kwamba wabunge wake karibu wote ni wa visiwani, lakini ninasema kuwa thta is not the ishu the ishu ni elimu ya viongozi wetu, kama ya Mbowe haifai ni vyema mkaweka ya viongozi waliowahji kutufaa as a nation!

NILIYOYAELEWA:
(a) kwamba KWAKO BINAFSI cuf ni chama cha visiwani - hiyo sitopinga maana ni nafsi yako inayoona hivyo (angalau cuf inarepresent watanzania wote na sio wa visiwani tu japokuwa viongozi wake wengi wa kuteuliwa wametoka visiwani)

maadamu nimekuelewa kwa hilo, basi tunaweza kuendelea na mjadala !
 
Hata hivyo, kama ambavyo tunaungana mkono pale tukikubaliana, tukikosea pia tutakosoana.

Mkuu inaonekana wewe una msimamo wako kuhsiana na mtizamo wako on Hitler na Germany, mimi nina mtizamo wangu on Hitler na Germany, na ni clear kuwa tuna mitizamo tofauti sasa kwa nini unakimbilia neno kukosoa?

Unamkosoa mtu ambaye haelewi anachokisema, au yuko mbali na ukweli unaokubalika na dunia nzima kama ukweli, lakini humkosoi mtu mwenye mtizamo tofauti na mtizamo wako, kwa sababu kama ni vitabu kuhusu Hitler na Germany viko vingi sana mkuu sidhani kama umevisoma vyote, na hakuna mahali popote inasema kuwa ulivyosoma wewe tu ndio vina ukweli wa Hitler na Germany,

Naona hili neno linawatesa na na mimi na kukosolewa, nimesema nikikosa sihitaji kuambiwa na mtu yoyote mimi ni mtu mzima, ila siwezi kulazimishwa kukosea ili furaaha ya watu kama wewe itimilike ya kunikosoa bado mkuu, endelea kusubiri kwa hamu lakini not on this, halafu turudi kwenye topic mkuu sina mpango wa kuibadili topic!
 
Back
Top Bottom