DustBin
JF-Expert Member
- Jun 3, 2021
- 628
- 609
Wadau nawasalimu kwa jina la JMT. Kazi iendelee...!
Najikita moja kwa moja kwenye mada husika, juu ya yanayoendelea huko mashuleni (shule za msingi)
Mimi nipo haoa mkoani (nausitiri), juzi nimekutana na mtendaji mmoja wa idara ya elimu wakati tukipeana dondoo za hapa na pale ndio akaanza kunichomolea uzi huu.
Ni kwamba walimu wakuu wa shule za msingi za serikali, kuna mchezo mchafu wanaucheza kuhakikisha shule zao zinashika nafasi za juu ktk matokeo ya darasa la saba. Wengi wao hawasimamii taaluma kwa kuhakikisha walimu wanafundisha ipasavyo. Kinyume chake ikifika kipindi cha mitihani ndio hufanya njama za kuwapa majibu watahiniwa na hata kuwahonga wasimamizi kwa vijisenti ambavyo mwalimu mkuu anajua anavipata wapi.
Kwa mujibu huyu mwandamizi, akaniambia kuwa hii inatokana na baadhi ya maafisa elimu msingi (DEO's) kuhamasisha walimu wakuu wahakikishe wanafaulisha, atakaeshindwa kufaulisha basi atatenguliwa. Hivyo walimu wakuu hujipinda kwa mbinu zozote hata zisizo halali wahakikishe hawapokonywi mkate wao. Mbaya zaidi kuna baadhi ya maafida elimu wilaya (msingi) wanajua huo mchezo unaofanywa na walimu wakuu. Na hili kwa sasa limekua sugu ktk baadhi ya maeneo hapa nchini.
Mchezo huu ndio unaosababisha wakuu wa shule za sekondari kupokea wanafunzi wasiojua kusoma, kuhesabu na kuandika kwa sababu huko shule ya msingi wanabebwa na walimu wakuu wao. Lakini pia hili linakua changamoto kwa baadhi ya walimu wakuu ambao huo mchezo hawakuuzoea hasa wale ambao walihamishwa kutoka sekondari kuja msingi kwa kigezo kule sekondari walijaa na hawakua na kazi za kufanya.
Mchezo huu ukiendelea, taifa litakua linarudi nyuma badala ya kwenda mbele. Tutaendelea kulipia ada za bure (EBM) watoto mazezeta huko sekondari bila mafanikio yeyote. Nashauri wahusika wafuatilie hili, lisemwalo lipo..!!
Aidha kwa kuwa mitihani inahusisha idara mbalimbali siku hizi, kama vile Idara za elimu, Polisi, Idara ya Usalama na TAKUKURU, napendekeza yafuatayo yafanyike ili tudhibiti hili;-
(a) Wasimamizi wa mitihani wanaopangiwa kituo fulani kusimamia waondoshwe na kupelekwa kusimamia kituo kingine asubuhi mapema kabla mtihani haujaanza. Hili lifanyike pasi na wao au walima wakuu kujua
(b) Au la, msimamizi asimamie siku moja tu kwa kituo kimoja. Siku nyingine/inayofuata anapelekwa kusimamia kituo kingine. Na hii pia ifanyike bila wao kujua
(c) Walimu wakuu niwaonye tu kwamba hilo mnalolifanya mnajiharibia wenyewe na mnahatarisha ajira zenu, hao maafisa elimu mnaoona kama wanakuungeni mkono, ukikamatwa utabaki peke yako na wao watakuruka hatu 100 uje utahayari. Tekelezeni jukumu lenu la kusimamia taaluma shuleni ili kama mnafaulisha iwe kwa halali na sio figisu figisu mnazozifanya. Mkumbuke hii ni awamu nyingine.
Mwisho.
Nimesikia maafisa elimu msingi wanatangaza waziwazi kwa walio chini yao kiutendaji kwamba mwalimu mkuu atakaefelisha hata kama ktk usimamizi wa mambo mengine yupo vizuri basi atamshugulikia. Kauli kama hizi ndio zinachochea huu ubadhirifu..!! Wenyewe mnajua mnayoyafanya huko. Badilikeni, na fuatilieni ufundishaji, hakikisheni walimu wanafundisha kweli na sio kutaka tu wafaulishe..!!
Leo naishia hapa..! Mkinikera zaidi nitakuja siku nyingine...
Asubuhi njem.