Kama maombi na dua yangekuwa yanafanya kazi watu wangeikimbia siasa

Kama maombi na dua yangekuwa yanafanya kazi watu wangeikimbia siasa

SankaraBoukaka

JF-Expert Member
Joined
Jul 2, 2019
Posts
3,577
Reaction score
5,664
Kila siku, mamilioni ya watu hukusanyika kwenye nyumba za ibada wakipiga magoti na kuomba amani, ajira, afya bora, na kupungua kwa umaskini.
Maombi na Dua hutoa faraja ya kiroho na matumaini ya kesho bora. Lakini ukweli ulio wazi ni kwamba mabadiliko ya maisha hayaji juu ya madhabahu pekee, bali yanatengenezwa kwenye meza za kisiasa.

Kama Dua zingekuwa na uwezo wa moja kwa moja wa kujenga barabara, kupunguza mfumuko wa bei, au kuadhibu mafisadi, basi siasa ingekuwa taswira ya kale isiyo na maana.
Wananchi wangeacha kura na kampeni, wakiamini kuwa suluhisho la kila tatizo linapatikana kwa kuinua mikono na kutamka maneno machache ya imani.

Haki na maendeleo yangekuwa matokeo ya ibada, si ya sera.

Lakini ushahidi wa unafiki huu unaonekana wazi wakati wa kushika madaraka. .. Wanasiasa huwa wanaapa kwa kushika vitabu vitakatifu kama Biblia na Quraan, wakiahidi uadilifu.
Ndani ya mioyo yao wanajua vyema kuwa maombi hayawezi kuwazuia mara moja. Ndiyo maana wanapomaliza kuapa, au hata kabla ya kuapa huwa wanawaza kuneemeka na kusahau ahadi zao bila woga wowote wa radi ya kiungu, maana wananchi wangeamua kumshtakia Mungu kwa Maombi na Dua juu ya yanayofanywa na wanasiasa madhalimu.

Ajabu ni kwamba viongozi haohao bado huwataka wananchi wawaombee, wakitumia maombi kama ngao ya kuwaliwaza na kuwafanya wavumilie umaskini waliotengenezewa kwa makusudi.

Dunia inahitaji mikono ya binadamu, akili za kupanga, na moyo wa uwajibikaji.

Maombi yanabaki kuwa mwanga wa kiroho, lakini siasa ndiyo uhalisia unaoamua bei ya mkate na hatima ya taifa.
 
Umenena kweli mkuu,kuna mambo huwa yanafikirisha sana mkuu,
 
Back
Top Bottom