Kama Marekani itaiga inachofanya China barani Afrika, sio tu itajivunia heshima bali pia haitapata inachotaka

Kama Marekani itaiga inachofanya China barani Afrika, sio tu itajivunia heshima bali pia haitapata inachotaka

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121
VCG111405146573 (1).jpg


Siku chache baada ya waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Qin Gang kumaliza ziara yake ya mwaka mpya barani Afrika, waziri wa fedha wa Marekani na balozi wa nchi hiyo kwenye Umoja wa Mataifa walianza ziara zao barani humo mmoja baada ya mwingine. Na imeeleweka wazi kuwa lengo kuu la ziara hizo ni "kukabiliana na ushawishi wa China barani Afrika." Lakini wanaweza wasitambue kuwa kama Marekani inajaribu kuiga inachofanya China barani Afrika, sio tu inajivunjia heshima bali pia haitapata inachotaka.

Siku hizi, "nguvu ya uongozi duniani" iliyo nayo Marekani inapungua kwa kasi, hali ambayo inaweza kuonekana kwenye majibu ya upande wa Afrika. Katika siku ya pili baada ya waziri wa fedha wa Marekani Janet Yellen kuanza ziara yake barani Afrika, serikali ya Afrika Kusini ilitangaza kuwa itafanya mazoezi ya kijeshi na China na Russia katika bahari ya nchi hiyo mwezi Februari. Baadaye waziri wa mambo ya nje wa Afrika Kusini Bibi Naledi Pandor, alipokutana na Yellen alisema moja kwa moja, “tunakaribisha ziara za maofisa waandamizi kutoka Marekani, lakini tunaitumai Marekani itaondoa vikwazo vya upande mmoja dhidi ya nchi za Afrika.” Ni wazi kuwa Afrika Kusini, nchi yenye nguvu kubwa zaidi kiuchumi barani Afrika haitaki kuipa Marekani heshima yoyote. Halisi ni kuwa tangu rais Biden aingie madarakani, nchi za Afrika zimetambua wazi hila za Marekani kuharibu uhusiano kati ya China na Afrika, ambazo matokeo yake ni madogo. Hii ni kutokana na sababu tatu zifuatazo:

Kwanza, mtindo wa ushirikiano unaotolewa na China unaendana na maslahi ya maendeleo ya nchi za Afrika. Kwa muda mrefu, Marekani imekuwa ikiichukulia Afrika kama “chombo” chake, na hata mshauri wa kitaifa wa masuala ya usalama wa Marekani Bw. Jake Sullivan aliitambulisha Afrika kama "mshirika mkuu wa siasa za kijiografia", kwa mfano kwenye mgogoro kati ya Russia na Ukraine, Marekani inatumai nchi za Afrika kuilaani Russia, la sivyo zitaadhibiwa. Lakini China nayo siku zote imekuwa ikisisitiza ushirikiano wa kunufaishana kati yake na Afrika na kutoingilia mambo ya ndani ya nchi nyingine.

Pili, China inaweza kuleta manufaa halisi kwa Afrika. Kutoka Reli ya TAZARA iliyojengwa takriban nusu karne iliyopita hadi Kituo cha Afrika CDC kilichozinduliwa mwezi uliopita, "Jumuiya ya China na Afrika yenye Mustakabali wa Pamoja" haijawahi kuwa kauli mbiu ya maneno matupu. Lakini Marekani ni tofauti. Kutoka kwa mpango wa Obama wa "Power Africa" hadi mpango wa "Jenga Upya Ulimwengu Bora" wa Biden, Marekani imetoa mapendekezo mengi kuhusu Afrika, lakini utekelezaji wao ni mbaya. Kwa hiyo, nchi nyingi za Afrika zinachagua ushirikiano halisi wa China badala ya keki ambazo Marekani inaendelea kuchora.

Tatu, Marekani haina msimamo endelevu kuhusu Afrika kama ilivyo China. Tofauti na utawala wa rais aliyepita Donald Trump, serikali ya Biden sasa inasema "itaweka kila kitu barani Afrika." Lakini je, "Marekani imerejea" leo, hakuna anayejua kama Marekani itaondoka tena wakati rais ajaye wa Marekani atakapoingia madarakani. Kinyume chake, Waziri wa Mambo ya Nje wa China ametembelea Afrika katika ziara ya mwaka mpya kwa miaka 33 mfululizo, na China pia imekuwa mshirika mkubwa zaidi wa kibiashara wa Afrika kwa miaka 13 mfululizo, ambapo urari wa biashara kati ya China na Afrika unaendelea kukaribia uwiano mwaka hadi mwaka. Ni nani kati ya China na Marekani ambaye ni mwaminifu zaidi kwa Afrika, hii imejulikana kupitia vitendo halisi.

Ni jambo la kufurahisha kuona uwepo wa China barani Afrika umekuwa ni msukumo kwa Marekani kurudi barani Afrika. Lakini, waziri wa mambo ya nje wa China Qin Gang pia alisema katika ziara yake ya hivi karibuni barani Afrika kwamba Afrika haipaswi kuwa uwanja wa michezo wa nchi kubwa. Kauli hii ni kuikumbusha Marekani kwamba Marekani kuongeza ushirikiano na Afrika hakupaswi kuilenga China, la sivyo inayoumia ni Afrika.
 
......nimesoma mahali, President of Zimbabwe crocodile 🐊, amepewa mansion na President wa equatorial guinea pale malabo!!,elewa kuwa equatorial guinea pamoja na utajiri mkubwa hasa wa crude oil, raia wake wanaishi under 1usd day, Zimbabwe raia wake almost 30%wamegeuzwa kuwa wakimbizi, still Africa tunamtafuta mchawi wetu na kufanya ushabiki wa kichina/kimarekani!!,amini usiamini Africa itakapofungua macho na kusema Amen, China itakua imshaondoka na kila kitu, tuendelee kufumba macho ya kimaombi, ila binafsi sijafumba macho kabisa
 
......nimesoma mahali, President of Zimbabwe crocodile [emoji246], amepewa mansion na President wa equatorial guinea pale malabo!!,elewa kuwa equatorial guinea pamoja na utajiri mkubwa hasa wa crude oil, raia wake wanaishi under 1usd day, Zimbabwe raia wake almost 30%wamegeuzwa kuwa wakimbizi, still Africa tunamtafuta mchawi wetu na kufanya ushabiki wa kichina/kimarekani!!,amini usiamini Africa itakapofungua macho na kusema Amen, China itakua imshaondoka na kila kitu, tuendelee kufumba macho ya kimaombi, ila binafsi sijafumba macho kabisa

Hamna mjinga kama hilo linchi la Equatorial Guinea na naona hakuna jeshi kabisa!
Waafrika wengi wako macho na ndio maana nchi hazichukui mikopo kwenye nchi moja!
Usijali Mungu yupo walahi hatutafika hapo!
 
Kitu kimoja tukiweke wazi hapa,hakuna free lunch hapa duniani, China ametufanya tufumbe macho na tutakaposema Ameen, tusije tena tukaanza kumtafuta mchawi China kawekeza more than 40%ya mikopo yake Nigeria, SA,na DRC, very clever move, sisi tupo jirani na DRC bado tumelala usingizi wa pono,all major machineries za DRC,more than 45%,zinapitia Durban na Zambia anakula ushuru wake na road tolls, TI tunapigana kuwekwa viraka sio kujenga upya!
 
Sio laana ndio mwendo wa civilization hata sisi tuta fika tu maana tuliko toka ni mbali zaidi
Sio kwa mwendo huu wa konokono na wa kutokujielewa kama muanzisha uzi anavyopigia debe wachina!
 
Maelezo marefuuuuuu nimeishia hapo unaposema mtindo wa ushirikiano wa China unaendana na maslahi ya maendeleo ya Africa

Labda ni mchina ndio kaandika huu uzi

Siku Afrika ikijua nguvu na potential iliyo nayo yenyewe ndani ya yenyewe itaendelea Sana. Siku mkiacha kutafuta 'bwana' wa kumuegemea kila uchwao tutasogea sisi kama sisi.

Ni nini ambacho tunakikosa Afrika kama afrika miongoni mwetu? Labda kujitambua na kujiamini
 
Sijasoma yote hayo ila juu juu tu
Kwa kweli ushawishi wa [emoji631] ni silaha tu na hata silaha nchi nyingi zinatengeneza siku hizi

China imeshika soko kwa sababu mishahara ya wafanyakazi wao ni midogo sana ukilinganisha na America
Na bidhaa nyingi China wanaziuzia hata [emoji631]

America hawezi kuuza bidhaa zake katika soko la Africa kwa sababu hatuwezi kununua ni ghali mno
Je tunaweza kuvaa Polo ? Au kuendesha magari yao au iPhone kwa wote?

Lakini kwa mchina kila kitu kinawezekana na pia hata masikini anatumia bidhaa za [emoji630]

Tunachotaka na sisi sio kila siku kuwategemea hao hao wenye viwanda

Mchina technology nyingi ameiga kwa mataifa mengine na mengine kaboresha na mengine amebuni mwenyewe

Sisi kila kitu tuna import halafu kutwa mnatoa matokeo ya wahitimu wa sayansi ambao hawawezi kubuni au hata kuiga na kufyatua kitu chochote kama wenzetu

Je sisi ni tegemeo la kudumu?
Wenzetu mpaka kinyesi kina faida
Kusoma kuna faida gani kama hatuwezi kutengeneza chochote au elimu ni shahada tu basi
 
Back
Top Bottom