Kama masuala ya utekaji yameanza mapema hivi, kipindi cha uchaguzi hali itakuwa mbaya mno. Polisi chukueni hatua thabiti

tripof

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2024
Posts
829
Reaction score
1,120
Kimsingi suala la utekaji limeendelea kuwa suala linalotamkwa kila mahala. nimemsikia Waziri wa Mambo ya Ndani Masauni, nimemsikia Rais wa TLS bwana Mwakubusi na pengine maeneo kadhaa.

Kama ni kweli hali hii ipo Polisi chukueni tahadhari ili kulinda mali na watu ndani ya nchi. Msingi wa 4R za Rais,ni haki,utulivu na amani vinginevyo hamtamtaitendea haki falsafa hiyo. Wananchi nao toeni ushirikiano kwa vyombo vya dola.

Hofu ni kwamba kipindi cha uchaguzi inaweza kuwa mbaya ya wagombeaji kutekwa na fomu zao. ikonekana mtu kujiteka apelekwe mahakamani.
 
Unawaambia akina nani sasa? Hawa hawa polisi wetu?
 
Vipi kama ikitokea ndiyo hao hao wenyewe wanaofanya hizo mambo kutokana na maelekezo kutoka juu!!
 
Hivi Hawa watekaji wanapo kuja kukuteka hujitambulisha Kama Akina Nani?

Je! tiendelee kuwa tegemea police au dhamana za uhai wetu ziwe chini yetu wenyewe?
 
Kimsingi suala la utekaji limeendelea kuwa suala linalotamkwa kila mahala. nimemsikia Waziri wa Mambo ya Ndani Masauni, nimemsikia Rais wa TLS bwana Mwakubusi na pengine maeneo kadhaa.

Kama ni kweli hali hii ipo Polisi chukueni tahadhari ili kulinda mali na watu ndani ya nchi. Msingi wa 4R za Rais,ni haki,utulivu na amani vinginevyo hamtamtaitendea haki falsafa hiyo. Wananchi nao toeni ushirikiano kwa vyombo vya dola.

Hofu ni kwamba kipindi cha uchaguzi inaweza kuwa mbaya ya wagombeaji kutekwa na fomu zao. ikonekana mtu kujiteka apelekwe mahakamani.
Wananchi tuamke kabisa tutengeneze vikosi vya kujilinda mahali popote sio mtaani na hadi kwenye mabasi humo na kila mahali tukiwachekea hawa wanaochukua watu kwa jina la polisi tutakwisha maana polisi wameshawakana kwamba hawawajui.
 
Back
Top Bottom