Kama mbunge analipwa mshahara kama watumishi wengine kwanini mbunge akistaafu anapewa pesa zote huku watumishi wengine ni 33%?

Kama mbunge analipwa mshahara kama watumishi wengine kwanini mbunge akistaafu anapewa pesa zote huku watumishi wengine ni 33%?

40 bado kuna watu wanaanza kaz wakiwa na miaka 35 hawa wakistaafu 40 si watakuwa na vihela vidogo

Ukiona ajira yenye huitaji wa umri huo ujue ni nafasi kubwa na yenye mshahara mkubwa hvyo akistaafu na miaka 50 atakuwa ametumikia miaka 15

kuanzia miaka 50 hadi 70 mfanyakazi awe anafanya kazi kwa mikataba ya miaka 2 au 3
 
Watakubali hawa waliopo kwa dola..? Maana wapo above 60+ ila wana wekana tu kwa system
 
Wastaafu wengi wamependeza baada ya kustaafu.

Waliojipanga wakiwa kazini wanamelemeta.

Tatizo, wengi wanastaafu wakiwa na madeni, mizigo ya watoto wa kusomesha na kuwapa mitaji, hawana nyumba Wala mashamba.

Suruhisho,
Watumishi mlioko kazini zaa mtoto wa mwisho ukiwa pungufu ya miaka 45, kuwa na makazi Yako ukiwa na pungufu ya miaka 40, Fanya biashara au kilimo au ufugaji ili kujiongezea kipato.

Somesha wanao kwenye shule au vyuo unavyomudu, usikope ili mtoto akasome lakini mwanao akope heslb ili asome.

Ongeza vitega uchumi Leo.
Kujipanga ukiwa kazini, kiuhalisia haiwezekani hasa kwa mfanyakazi mwenye uadilifu. Mshahara na kipato halali ni kidogo kiadi kuwa huwezi ukafanya uwekezaji wenye tija. Ujanja ujanja, upigaji na wizi wa aina mbalimbali ndio pekee unaweza kumfanya mfanyakazi afanye uwekezaji wa aina fulani.
 
Huwa natamani kuelewa vizuri. Sijajua vizuri kama Mbunge analipwa mshahara kila mwezi kwa miaka mitano, lakini ninachofahamu ni kuwa bunge likivunjwa baada ya miaka mitano huwa wanapewa hela nyingi sana, zaidi ya milioni 200 kwamba hiki ni kiinua mgongo.

Natamni kujua ni kigezo gani kilitumika kumpa Mbunge huyu milioni zote hizo kwa miaka mitano. Kwamba yawezekana hatarudi bungeni? Kama ni hivyo kwa nini mtumishi wa umma akiacha kazi asipewe hela zake zote za hifadhi ya jamii?

Lakini pia ni kigezo gani kilitumika kwa mtumishi wa umma kupewa 33% ya fedha zake za hifadhi ya jamii na kwa nini isiwe 50%?

Wastani wa maisha ya Mtanzania ni miaka 66, ni kigezo gani kimetumika kumfanya mtumishi wa umma akae kazini mpaka miaka 60 na apewe 33% ya fedha zake za hifadhin ya jamii wakati kiuhalisi bado ana mika 6 tuu ya kuishi duniani? Hata LOWASA ameishi miaka 70 tu na siyo 72 au 82?

Serikali yetu haina budi kuliangalia swala hili kwa jicho la tatu na kuwahurumia watumishi wa umma ambao kiuhalisia wanaishi maisha magumu tofauti na mfanyabishara. Bidha zikapanda mitaani, mshahara haupandi kila mwezi.

Mtumishi wa umma ni kukamuliwa tu PAYE, NSSF (ampapo akistaafu atapewa 33%), kodi mitaani kwa kila atakachonunua. Ndiyo unakuta mtumishi wa umma anastaafu hata nyumba hana maana yeye aliishi maisha ya kukamuliwa tu!
Primary and hidden goal ya mifuko ni kumnyonya mfanyakazi kwa kisingizio cha kumjali. Wabunge wanalijua hilo, wanachukua mzigo wa maana huku wakitetewa na sisi wenyewe kuwa wao ni watunga sheria. Vyama vya wafanyakazi vinahitaji kuamka na kuamsha wafanyakazi.
 
Vyama vya wafanyakazi viongozi wake wanaingia kwa rushwa na wako upande wa serikali. Wao kupinga japo hata kutetea wenzao hawawezi
 
Mbunge sio mtumishi wa umma kwa muujibu wa public service act
 
Basi sheria ibadilishwe, wafanyakazi wasiitwe watumishi wa umma,🤣🤣🤣.
Watu wanapiga hela na kula mema ya nchi kwa kusingizia kuwa si watumishi wa umma?
 
Back
Top Bottom