Kama mimi ningekuwa Christiano Ronaldo ningefanya kulinda heshima yangu

Na ana mpango wa kupanua hotel yake Pestana CR7

Hicho kibunda anacholipwa sasa si mchezo,money is beautiful
 
Astaafu aache pesa? Pesa ndo heshima yenyewe. Ingekuwa kasajiliwa kwa pesa za kijinga hapo ungekuwa sawa.
 
Hata wedi kapu anayo
 
Hata hilo sanamu la matangazo maadamu mshiko unaingia hakuna shida
 
Hamna Heshima iliyovunjika yeye kwenda kuchota mihela kwa masheikh.

Na tafsiri yake ni kwamba wewe huwezi kuwa Ronaldo.
 
Unajua analipwa sh ngapi kwa mwezi. Hiyo heshima inamsaidia nini hajakaa uchi kaenda kwa waarabu. Acha babu astaafu na pesa yake
 
W
Ni sawa ila akitoka hapo anakuwa nani wakati kapoteza soko.

We bado hulijui soko la Cr7 lilivyo na nguvu, hapo kinachobadilika ni focus ya kibiashara huko Saudia,, waarabu wanapesa vibaya sana

Preseason za Vilabu vingi vikubwa ulaya hupenda kwenda barani Asia ili kutanua wigo wa masoko yao

Waarabu ndio kiini cha Man City kutawala Epl, na sasa wanaindea Newcastle utd

Cr7 kaangalia mpunga atakaokunja huko Al Nasr kuanzia angle ya mshahara, bonuses mpaka matangazo huko ktk nchi husika

Pesa haina kikomo cha kutafuta, ndio maana matajiri kina Bakhressa kila leo wanazidi kuongeza wigo wa biashara ilhali sisi maskini account ikisoma tumilioni kadhaa tunaanza kutembea kwa kutanua makwapa kama tuna majipu vile 😀
 
Waarabu wana pesa kuliko wazungu?
 
Well said
 
Kabla haujamshauri Ronaldo ambaye ameshafanikiwa kwa kila kitu Fanya yafuatayo
1. Jishauri kuhusu afya,elimu, mlo wako
2. Jishauri kuhusu gono,malaria, kichwa
3.Jishauri kuhusu utasaidiaje ndugu zako maskini huko vijijini
4. Jishauri kuhusu malazi na malezi Bora
5. Jishauri kuhusu utaondoaje vifo vya wajawazito, na utapiamlo etc
Thanx
 
Wanazi wakimaharibi wameumia sana Ronaldo kwenye Uarabuni, Walitaka aende MLS, wivu unawatesa sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…