Kama mkeo aliekukosea haombi msamaha na siku zaenda, waweza jisemesha mambo yaendelee?

Kama mkeo aliekukosea haombi msamaha na siku zaenda, waweza jisemesha mambo yaendelee?

Maleven

JF-Expert Member
Joined
Sep 8, 2019
Posts
783
Reaction score
3,666
Kwa mfano mmepishana kauli, mkeo akakupandishia sauti hivyo, we ukakasirika, lakini soku zaenda, mkeo haoni kama amekosea na wala haombi msamaha, anakula buyu kama wewe.

Je utajisemesha tu mambo yaendelee kama zaman?

Au utamwambia akuombe msamaha alikukosea?

Au na wewe utakausha tu hadi siku atakapoona yeye amekukosea?

naomba uzoefu wenu.
 
ACHA UJINGA MARA MOJA.

HUMO NDANI NANI KAMUOA MWENZAKE??.

ACHA KUMZINGATIA, ANZA KUA BIZE NA SIMU ,ONGEA NA SIMU UNATOKA NJE, UNACHEKAA.

Kuna mawili, aanze kushikwa na wivu Kwa kuhisi umepata Demu nje .

Au nayeye aanze kuchepuka, na kwakua ni mpumbav atafanya hivi Kwa Hasira, hivo wewe utamfuma haraka , na PAPO HAPO, UTAMPA TARAKA 3 ,aende Kwa Baba na Mama yake,akawapandishie sauti.
 
Bado hamjakua,we Kaa kimya fanya majukumu yako yanayokupasa kwa familia....kwa hela ya siku lazima umpe mkononi? Weka mezani sepa...
Ukirudi home jioni mnaweza patana,au kesho,au keshokutwa...
 
Kwa mfano mmepishana kauli, mkeo akakupandishia sauti hivyo, we ukakasirika, lakini soku zaenda, mkeo haoni kama amekosea na wala haombi msamaha, anakula buyu kama wewe.

Je utajisemesha tu mambo yaendelee kama zaman?

Au utamwambia akuombe msamaha alikukosea?

Au na wewe utakausha tu hadi siku atakapoona yeye amekukosea?

naomba uzoefu wenu.
Una chaguzi mbili tu...
1. Be a real man
2. Kuwa mwanaume halisi
 
Mkuu simama kama mwanaume halisi.

Kama haelewe somo Anza Kuja saa5 za usiku au unalala huko kabisa siku nzima na ukirudi huna habar nae
Ha ha haaa nimekumbuka kwenye ule uzi wako ukasema mwanamke akiolewa anathaminiwa na kina nani sijui😅😅😅. Kumbe mambo ndani ndo hivi,thamani hiyo vipi mkuu?
Vita ni vita mura
 
Kuna vitu vinasikitisha sana, naomba nisemehe, humo ndani mbadilishane status, yeye ndio anaonekana mtawala na wewe fuata upepo.
Kwahiyo alikukosea akakupandishia na hujui ufanye nini?
Pathetic
 
Kuna vitu vingine sio lazima uvicount, mengine mezea maisha yaende ila usiweke kinyongo, kinyongo kibaya sana kwa wanandoa......
 
We acha tu yani mwanamke ana tofauti na viongozi wakubwa wa ccm akili zao.
Ina bidi mda mwengine utumie Uchadema No reform No election.
IMG_1047.jpeg
 
Ha ha haaa nimekumbuka kwenye ule uzi wako ukasema mwanamke akiolewa anathaminiwa na kina nani sijui😅😅😅. Kumbe mambo ndani ndo hivi,thamani hiyo vipi mkuu?
Vita ni vita mura
Dawa ya jeuri ni nini kwani?
Ukitii nawewe utapewa utii wako ukikaidi utapigwa tu
 
Mwanaume hasusi wala kununa ndani ya ndoa.
Ongea naye kwa kumpa maelekezo mbalimbali na kamwe usiumize kichwa kumwomba msamaha au kusubiri yeye akuombe.
Njia ya asili kuondoa ukakasi huo ni kutaka mzigo hata kwa njia ya upole utaona maongezi yanajitokeza.
 
Back
Top Bottom