Kama Mkristu Mkatoliki Naomba Unishauri!

Asante Saana Ndugu, Ubarikiwe..
 
Nakushauri nenda parokia unayosali ukaongee na padri umueleze matatizo yako ikiwezekana uanze mafundisho ya komunio upya uombe na kubatizwa pia. Hakuna kinachoshindikana ukiwa muwazi mkuu.

Kristu..
Tumain letu, Kristu Jana..........
 
Hata kama ungekuwa hujabatizwa bado sio shida hata kidogo maana kanisa ni la watu wote...

Ukiwa parokia kama za chuo ni easy sana mchakato wa kupata vyote hauzidi mwaka mmoja
 
Umebaki mkristo jina!! Nani alikuambia ukristo ni kula komunio?
 
Ninakujibu kama Mkatoliki. Najua umeiweka hii katika public, kwa hiyo utajibiwa na watu tofauti, wengine watakuvutia kwao, wengine watakukejeli, wengine watakukatisha tamaa.

Sasa jibu ni hili. Paroko ana mamlaka makubwa katika masuala ya sakramenti ndani ya Parokia yake. Nenda kamueleze haya yote Paroko wa Parokia yako. Hakuna Paroko anayeleta mchezo mchezo kwenye sakramenti za Kikatoliki, maana hizo ndio kwa kiwango kikubwa zinazoutambulisha Ukatoliki. Nenda ofisini kwake, ataamua jambo positive kabisa kuhusu ndoto zako.
 

Tumsifu Yesu Kristu,

Haina shida, parokia yoyote ambayo ulibatizwa rekodi halisi za watu waliobatizwa hapo miaka yote hiyo parokia ipo hai zinakuwepo.

Cha kufanya, tafuta parokia uliyobatizwa, mwaka na mwezi uliobatizwa, majina ya wazazi wako na mtu aliyekusimamia ubatizo pamoja na majina yako yote ya ubatizo uende hiyo parokia na uwaeleze hilo jambo.

Hicho cheti ni muhimu sana maana hutaweza kupata sakramenti ukitoa Upako wa Wagonjwa bila hicho cheti.

Naimani kitakuwepo wewe tafuta nauli na weka nia ya kukifuatilia, Mungu anakupa changamoto ni vizuri kumuuliza ni nini kusudi lake na wewe katika hali kama hizi na si kila mmoja njia yake ya utumishi kwa Mungu inakuwa imenyooka wengine wanapata changamoto ili kuwa bora zaidi ndo maana pengine umeweza kulifahamu kanisa kwa undani wake na mambo yake.

Kila la heri

Sali Salamu Maria 3, Baba Yetu 3 na Atukuzwe Baba 3 Kabla ya kuanza safari yako.
 
Mkuu ondoa shaka, fahamu hujachelewa; cha msingi nenda ktk kanisa lililo karibu nawe, then onana na kasisi yoyote; muelezee shida yako; hapa JF hutapata msaada wowote makini.
 
Hata kama ungekuwa hujabatizwa bado sio shida hata kidogo maana kanisa ni la watu wote...

Ukiwa parokia kama za chuo ni easy sana mchakato wa kupata vyote hauzidi mwaka mmoja
Asantee saana..
 
Mkuu ondoa shaka, fahamu hujachelewa; cha msingi nenda ktk kanisa lililo karibu nawe, then onana na kasisi yoyote; muelezee shida yako; hapa JF hutapata msaada wowote makini.
Bless saana Mwana..
 
Amina sana Ndugu Ubarikiwe..
 
Milele Amina..
Daah umenigusaa Saana..
 
Mbona ni kazi rahisi sana. Najua kama ni mkatoliki utakuwa unajua maana ya Jumuiya ndogo ndogo. Hivyo kwenye Jumuiya tuna viongozi wetu ikiwemo M/Kiti. Natumai majibu yote ya matatizo yako yangepata majibu kwa wakati. Ushauri wangu naomba ujiunge na Jumuiya ndg ndg popote ulipo na baada ya hayo haya yote uliyoyandika yawasilishe kwa viongozi wa Jumuiya husika. Natumai utapata msada wa kupata Sakremeti ya Komonio ya kwanza, Kipaimara na hata Ndoa. Nakutakia kila la Kheri.
 
Nakushauri ukafuatilie cheti chako kule wazazi wako walipokiacha na uanze mafundiaho ya wakatekumeni utapewa hizo Sacrament.
Pole sana kwa mfarakano wa kifamilia uliokukosesha masakrament.
 
Nakushauri ukafuatilie cheti chako kule wazazi wako walipokiacha na uanze mafundiaho ya wakatekumeni utapewa hizo Sacrament.
Pole sana kwa mfarakano wa kifamilia uliokukosesha masakrament.
Asaante Saana..
 
Uko wapi, bado sana kuna nafasi kubwa na uwezo wa kuwa padri mpk sasa! Hizo scrament unaweza pata tu.

Kikubwa naomba kujua uko wapi na unafanya nini kuanzia hapo I will help you to follow your dream to be a priest/padri.

Cha msingi usiwe umeoa au kuwa na mtoto, binafsi nina 34 kasoro but still nawaza kurudi nikawe padri wito ni kitu cha ajabu mno. Nitafute pm.
 

Milele Amina!

Kama unaikumbuka Parokia yako uliyobatizwa basi nenda hapo ukiwa na taarifa zako sahihi kwa maana ya jina lako la Ubatizo, Jina la Baba na la Mama. Pia kama hukumbuki mwaka exactly unaweza wapa range, watacheki kwenye register na wakikupata watakupa Cheti kipya cha Ubatizo kikiwa na details zote!
Sasa ukiisha kipata hicho cheti cha Ubatizo rudi kwenye Parokia yako ya sasa na uongee na uongozi kujua ni kipindi gani mafundisho ya Wakatukumeni yataendeshwa, jiunge nayo na utapatiwa Komunyo ya kwanza na Kipaimara!

Angalizo:
Utafute na Jumuiya mahalia unapoishi ili uwe unasali pamoja na wana jumuiya wenzako, hii itakusaidia sana kwenye process za Masakramenti hayo na hata Ndoa muda ukifika!

Kila la heri na Mungu akuongoze!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…