Tumsifu Yesu Kristu,
Haina shida, parokia yoyote ambayo ulibatizwa rekodi halisi za watu waliobatizwa hapo miaka yote hiyo parokia ipo hai zinakuwepo.
Cha kufanya, tafuta parokia uliyobatizwa, mwaka na mwezi uliobatizwa, majina ya wazazi wako na mtu aliyekusimamia ubatizo pamoja na majina yako yote ya ubatizo uende hiyo parokia na uwaeleze hilo jambo.
Hicho cheti ni muhimu sana maana hutaweza kupata sakramenti ukitoa Upako wa Wagonjwa bila hicho cheti.
Naimani kitakuwepo wewe tafuta nauli na weka nia ya kukifuatilia, Mungu anakupa changamoto ni vizuri kumuuliza ni nini kusudi lake na wewe katika hali kama hizi na si kila mmoja njia yake ya utumishi kwa Mungu inakuwa imenyooka wengine wanapata changamoto ili kuwa bora zaidi ndo maana pengine umeweza kulifahamu kanisa kwa undani wake na mambo yake.
Kila la heri
Sali Salamu Maria 3, Baba Yetu 3 na Atukuzwe Baba 3 Kabla ya kuanza safari yako.