Kama Mkristu Mkatoliki Naomba Unishauri!

Kama Mkristu Mkatoliki Naomba Unishauri!

Ryzen

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2012
Posts
7,301
Reaction score
8,706
Tumsifu Yesu Kristu!

Nina Jambo Nataka Kuwashirikisha Ndugu Zangu!
Naandika Maneno Haya nikiwa na Huzuni Kubwa Moyoni...Huzuni inayosababishwa na Kutotimiza Ndoto yangu Kubwa ya Utotoni Niliyonayo.. (Tuendelee)..

Mimi ni Kijana wa Miaka 23, Mkatoliki ambaye sijapata Sakramenti za Kikatoliki Pamoja na ya Kwamba Naujua Ukatoliki Vizuri saana!

Nilikuwa na Ndoto Nyingi sana ndani ya Ukatoliki wangu Kubwa hasa ilikuwa Kutaka Kuwa Padre..Bahati Mbaya sana Ndoto zangu Hizi zikawa za Abunuasi...Yaani Hazikufanikiwa na Sina Matumaini Tena Kama zitafanikiwa... sababu Kubwa sijawahi kupata sakramenti ya Komunio na Kipaimara (Na Mpaka sasa Sijapata)

Kwanini Sijapata Sakramenti?
Nilibatizwa Katika Jimbo ambalo baadaye Wazazi wangu Walihama..After Then wakaacha cheti changu cha ubatizo katika hilo Jambo..
Baada ya kuanza shule ya Msingi nikawa Nahudhuria Kanisani kama kawaida Yangu mpaka nilipoanza mafundisho yangu ya Komunio!
Siku Tunaungama ili Tupate Rasmi komunio Ndio siku Najua kumbe sina Cheti Cha Ubatizo, Na Kwa bahati mbaya sana wakati Huo Baba na Mama walikuwa Hawaelewani kwahio hata cheti hakikuweza kufuatiliwa..

Nilikosa Komunio, siku hio naona wenzangu niliofanya nao Mafundisho kwa Miaka Miwili wanapata Komunio NILILIA SANA.. iliniuma Kufanya Mafundisho kwa Muda Mrefu nikiwa na Great Expectations na nilichokuwa nakitaka Nakikosa....Nilikuwa Darasa la 5 wakati Huo..Ikafika Mahala Mama akiniambia niende Kanisani Nakataa.. sitaki Kwenda Kanisani.. Akinilazimisha Kwenda Basi Nitaondoka na Kuishia Mtaani Kuangalia Movies Vibanda Umiza Mpaka Muda wa Kutoka church ufike ndo Nirudi Home..

Nikakata tamaa ya Kwenda Kanisani na Sikuwahi Kupata Motivation ya Kwenda Church Mpaka nafika University.. (Imagine Darasa la 5 Mpaka University).. Ikumbukwe Hapo Nilikuwa Nasoma Makala zote za Kikatoliki Mitandaoni na Kufuatilia Kila kitu Kuhusu Kanisa kuanzia Historia, tamaduni na Mapokeo ya Kanisa + Mitaguso yote ya Kanisa... But still sikuwa na motivation ya Kuhudhuria Kanisani Maana i feel kitu mimi kama sio Complete Catholic Mimi..

Najiwa na Mawazo Mengi Labda ya Kubadili Dhehebu Either Niende Madhehebu Mengine ya kikristu au Nihame Dini Kabisa Niwe Muislamu au dini Nyinginezo Pia... Nafanya Hivi kwa Kuamini Mungu Yupo na Anaishi..

Sasa Hivi Nimebaki Mkristu Jina tu.. Sina Nilipokaa Complete Maana siamini kama im a Complete Catholic Kama Sijapata Hizo Sakramenti..

Sasa kwa Utu Uzima wangu Nataka Tushauriane.. Je Naweza Kufatilia Nikapata? Na kwa wakatoliki Wabobezi itachukua Muda Gani Hasa wa Mtu kama Mimi Ambaye Najua Mafundisho ya Kanisa Katoliki na ya Ukristu kwa Undani kabisa.. Kupata Hizo Sakramenti..??

Halafu Kingine Najiuliza Kwanini Haya Yanitokee?? Au Ndio Mungu Hakutaka Niwe Padre??

Kingine Cha Mwisho Je itakuwa Jambo la Busara Nikibadili Dhehebu au Dini..??

(Nimeandika Haya Kwa Machungu Sana.. Maana nilienda Kanisani Mara Moja Mwaka Jana Nikaona Karibia Watu Wote Niliokaa Nao wamenyanyuka Kupata Komunio Nikabaki Mimi Nimeketi)..

Mwenyezi Mungu Awaongoze Katika Ushauri Wenu Mtakaonipa....Mbarikiwe...!

Tumsifu Yesu Kristu!
 
Mwamini Yesu na umpokee naye atakata kiu yako.
 
wewe nenda mbele padre akisema mwili wa kristo unaitikia Amina inakula...
mambo mengine kujipa presha tu.

Uwe padre umewahi kuwa na mwanamke?
 
wewe nenda mbele padre akisema mwili wa kristo unaitikia Amina inakula...
mambo mengine kujipa presha tu.

Uwe padre umewahi kuwa na mwanamke?
Asante saana.. Sijaoa..
 
Hii story mbona kama ni C&P halafu kama inerudiwa hivi??

Anyways nashindwa kutoa jibu la moja kwa moja kutokana na avatar yako na Huo u' catholic' wako


NB: Imani yako itakuponya
 
Hii story mbona kama ni C&P halafu kama inerudiwa hivi??

Anyways nashindwa kutoa jibu la moja kwa moja kutokana na avatar yako na Huo u' catholic' wako


NB: Imani yako itakuponya
BIG NO.. This is My Own Story Tafadhali Kaka Tusiharibiane... Tafuta hio yako uweke hapa kama zinafanana!
 
Nenda ambako cheti ulikiacha wape full details cheti ni haki yko utapewa tu. Pili mafundisho hayana umri watu wanafundishwa na kupokea hizo sacrament wakiwa na miaka 50+
 
Nenda ambako cheti ulikiacha wape full details cheti ni haki yko utapewa tu. Pili mafundisho hayana umri watu wanafundishwa na kupokea hizo sacrament wakiwa na miaka 50+
Daah toka 1996??
 
Nakushauri nenda parokia unayosali ukaongee na padri umueleze matatizo yako ikiwezekana uanze mafundisho ya komunio upya uombe na kubatizwa pia. Hakuna kinachoshindikana ukiwa muwazi mkuu.

Kristu..
Asantee sanaa...

Tumaini.. Letu..
 
Wewe muongo eti unamiaka 23 umezaliwa 96 duuu watu mnajua kutunga
 
Back
Top Bottom