Kama Mkristu Mkatoliki Naomba Unishauri!

Kama Mkristu Mkatoliki Naomba Unishauri!

Yaani hili ni tatizo kweli la kuleta hapa!?? Ina maana humjui hata baba yako wa kiroho ambae ndo mwenye msaada mkubwa sana kwa mambo hayo.

Lkn kwa kukusaidia,kanisa katoliki ndo baba sayansi,baba historia,baba wa kila kitu unachokiona leo. Hao ndiyo mabingwa wa kutunza kumbukumbu. Ukibatizwa ndani ya kanisa katoliki,taarifa zako hazipotei kamwe! Dada yangu alikuwa anafunga ndoa hapa dar mwaka 2015. Alibatizwa mwaka 1967,akiwa mchanga wa mwaka 1,miaka 14 baadae akapata komunio na kipaimara. Alipewa cheti lkn harakati za maisha akapoteza,hakujali mpaka alipotaka kufunga ndoa ndo akaambiwa afuate cheti Cha ubatizo. Alibatizwa kijijini kabisa parokia moja inaitwa Ibhoja ipo wilaya ya KAHAMA.

Nilitumwa me mwenyewe kukifuata,yaani ni kazi ya dakika 10. Nilikichukua nikakipiga picha nikatuma whatsap wakati me najipanga kurejea dar taratibu zikaendelea. Nenda ulikobatizwa kachukue...!! Wala siyo issue kabisa hiyo....
 
Baki na imani ya kanisa katoriki ndugu achana na propaganda zao hao watu maana hata hao wanaodai wamelowea katika madhehebu mengine wametoka na chimbuko la kanisa mama kanisa katoriki.
Amina saana Boss.... Sijawahi Kuwa na Dhehebu Lingine na Sitoikana imani Yangu Katoliki....Nitaipigania na Kuilinda...
 
Yaani hili ni tatizo kweli la kuleta hapa!?? Ina maana humjui hata baba yako wa kiroho ambae ndo mwenye msaada mkubwa sana kwa mambo hayo.

Lkn kwa kukusaidia,kanisa katoliki ndo baba sayansi,baba historia,baba wa kila kitu unachokiona leo. Hao ndiyo mabingwa wa kutunza kumbukumbu. Ukibatizwa ndani ya kanisa katoliki,taarifa zako hazipotei kamwe! Dada yangu alikuwa anafunga ndoa hapa dar mwaka 2015. Alibatizwa mwaka 1967,akiwa mchanga wa mwaka 1,miaka 14 baadae akapata komunio na kipaimara. Alipewa cheti lkn harakati za maisha akapoteza,hakujali mpaka alipotaka kufunga ndoa ndo akaambiwa afuate cheti Cha ubatizo. Alibatizwa kijijini kabisa parokia moja inaitwa Ibhoja ipo wilaya ya KAHAMA.

Nilitumwa me mwenyewe kukifuata,yaani ni kazi ya dakika 10. Nilikichukua nikakipiga picha nikatuma whatsap wakati me najipanga kurejea dar taratibu zikaendelea. Nenda ulikobatizwa kachukue...!! Wala siyo issue kabisa hiyo....
Asaante saana kaka mimi 96 tu
 
Mtume Paulo alisema kama huwezi useja acha ila wanajiingiza kimagumashi. Yesu wa Nazareth hatujui kwani injili za ukweli kumhusu zilifichwa
 
Nenda katika parokia iliyopo karibu nawe..kaonane na katekista..hapo utaambiwa usome mafundisho ya ukatakumeni nahisi hua ni miezi mitatu hivi sina uhakika sana...baada ya kumaliza mafundisho utapokea ivyo unavyovihitaji

Au kama vipi okoka kabisa nenda kabatizwe upya kwenye maji mengi..kule hakuna komunio wala kipaimara

Sikushauri kuhama dini

Huyu hana haja ya mafundisho ya ukatukumeni, ni mkatoliko kwani alibatizwa.
Aende kwa paroko wa parokia anayoishi atampa muongozo!
Anaweza kuamua kumpa mtihani kupima uelewa wake, kisha akampa hizo sakramenti kwa muda mfupi tu.

Cheti chake cha ubatizo atapata kwa kutaja tarehe ya ubatizo, jina na parokia tu.
 
Asante saana Kaka..
 
Tumsifu Yesu Kristu!

Nina Jambo Nataka Kuwashirikisha Ndugu Zangu!
Naandika Maneno Haya nikiwa na Huzuni Kubwa Moyoni...Huzuni inayosababishwa na Kutotimiza Ndoto yangu Kubwa ya Utotoni Niliyonayo.. (Tuendelee)..

Mimi ni Kijana wa Miaka 23, Mkatoliki ambaye sijapata Sakramenti za Kikatoliki Pamoja na ya Kwamba Naujua Ukatoliki Vizuri saana!

Nilikuwa na Ndoto Nyingi sana ndani ya Ukatoliki wangu Kubwa hasa ilikuwa Kutaka Kuwa Padre..Bahati Mbaya sana Ndoto zangu Hizi zikawa za Abunuasi...Yaani Hazikufanikiwa na Sina Matumaini Tena Kama zitafanikiwa... sababu Kubwa sijawahi kupata sakramenti ya Komunio na Kipaimara (Na Mpaka sasa Sijapata)

Kwanini Sijapata Sakramenti?
Nilibatizwa Katika Jimbo ambalo baadaye Wazazi wangu Walihama..After Then wakaacha cheti changu cha ubatizo katika hilo Jambo..
Baada ya kuanza shule ya Msingi nikawa Nahudhuria Kanisani kama kawaida Yangu mpaka nilipoanza mafundisho yangu ya Komunio!
Siku Tunaungama ili Tupate Rasmi komunio Ndio siku Najua kumbe sina Cheti Cha Ubatizo, Na Kwa bahati mbaya sana wakati Huo Baba na Mama walikuwa Hawaelewani kwahio hata cheti hakikuweza kufuatiliwa..

Nilikosa Komunio, siku hio naona wenzangu niliofanya nao Mafundisho kwa Miaka Miwili wanapata Komunio NILILIA SANA.. iliniuma Kufanya Mafundisho kwa Muda Mrefu nikiwa na Great Expectations na nilichokuwa nakitaka Nakikosa....Nilikuwa Darasa la 5 wakati Huo..Ikafika Mahala Mama akiniambia niende Kanisani Nakataa.. sitaki Kwenda Kanisani.. Akinilazimisha Kwenda Basi Nitaondoka na Kuishia Mtaani Kuangalia Movies Vibanda Umiza Mpaka Muda wa Kutoka church ufike ndo Nirudi Home..

Nikakata tamaa ya Kwenda Kanisani na Sikuwahi Kupata Motivation ya Kwenda Church Mpaka nafika University.. (Imagine Darasa la 5 Mpaka University).. Ikumbukwe Hapo Nilikuwa Nasoma Makala zote za Kikatoliki Mitandaoni na Kufuatilia Kila kitu Kuhusu Kanisa kuanzia Historia, tamaduni na Mapokeo ya Kanisa + Mitaguso yote ya Kanisa... But still sikuwa na motivation ya Kuhudhuria Kanisani Maana i feel kitu mimi kama sio Complete Catholic Mimi..

Najiwa na Mawazo Mengi Labda ya Kubadili Dhehebu Either Niende Madhehebu Mengine ya kikristu au Nihame Dini Kabisa Niwe Muislamu au dini Nyinginezo Pia... Nafanya Hivi kwa Kuamini Mungu Yupo na Anaishi..

Sasa Hivi Nimebaki Mkristu Jina tu.. Sina Nilipokaa Complete Maana siamini kama im a Complete Catholic Kama Sijapata Hizo Sakramenti..

Sasa kwa Utu Uzima wangu Nataka Tushauriane.. Je Naweza Kufatilia Nikapata? Na kwa wakatoliki Wabobezi itachukua Muda Gani Hasa wa Mtu kama Mimi Ambaye Najua Mafundisho ya Kanisa Katoliki na ya Ukristu kwa Undani kabisa.. Kupata Hizo Sakramenti..??

Halafu Kingine Najiuliza Kwanini Haya Yanitokee?? Au Ndio Mungu Hakutaka Niwe Padre??

Kingine Cha Mwisho Je itakuwa Jambo la Busara Nikibadili Dhehebu au Dini..??

(Nimeandika Haya Kwa Machungu Sana.. Maana nilienda Kanisani Mara Moja Mwaka Jana Nikaona Karibia Watu Wote Niliokaa Nao wamenyanyuka Kupata Komunio Nikabaki Mimi Nimeketi)..

Mwenyezi Mungu Awaongoze Katika Ushauri Wenu Mtakaonipa....Mbarikiwe...!

Tumsifu Yesu Kristu!
Umewahi kumshirikisha hili jambo padre au mwalimu yoyote wa dini?!
 
Back
Top Bottom