Ndugu zangu Watanzania,
Kwa hakika CCM ina mamilioni ya wanachama,ina washabiki wa kutosha ,ina wafuasi wengi sana ,ina aminika sana ,ina kubalika sana ,inapokeleka na kupokewa na mamilioni ya watanzania kila ipitapo,ina nafasi katika mioyo ya watanzania. Ukiona mkutano wa ndani tu watu wana jaa na kufurika kiasi hiki ,basi ni lazima ufahamu ya kuwa chama hiki kipo mioyoni mwa watu na kimebeba matumaini yao.
Hawa unaowaona pichani ni Sehemu tu ya maelfu ya wengine ambao wanakuwa wamebakia nje kwa kukosa nafasi ya kukaa ndani. Hata uchukue ukumbi wenye ukubwa wa aina ipi , CCM inauwezo wa kuujaza ndani ya dakika moja na wengine kubakia nje ya ukumbi.CCM ina uwezo wa kuujaza uwanja wa Taifa na ukabakia uking'aa kwa rangi za kijani na njano tu.
Kwa hakika hiki chama ni mpango wa Mungu mwenyewe.huwezi ukashindana nacho hata kidogo.iwe ni jukwaani au katika sanduku la kura.
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.