Kama mshahara ni chini ya Tsh 150,000/= kwa mwezi bora useme unatangaza nafasi za utumwa kuliko useme ni nafasi za kazi

Kama mshahara ni chini ya Tsh 150,000/= kwa mwezi bora useme unatangaza nafasi za utumwa kuliko useme ni nafasi za kazi

Mkuu kuna watu hawana huruma au alitaka aonekane ametoa ajira, ujue hata mm nimefikiria sana, kwa mshahara wa 2,000.00/day mtoto wa mtu apande daladala kutoka anakoishi mpaka kibaruani kwake na kurudi kwao, anunue sabuni ya kufulia nguo zake maana jamaa kasema awe msafi, kweli?????.

Bado muda wa kazi anaanza saa 1:00 asubuhi mpaka saa 4 usiku hii inamaanisha awe anaamka saa kumi alfajiri na kulala saa sita usiku, kama anakoishi ni mbali na foleni za DSM hii sijui itakuwaje

Vinginevyo utakuta anawalaza watoto wa watu stoo ya vyakula. Zaidi sana hawa mabinti itabudi wajiuze kwa wateja wao chakula ili waweze kumudu maisha.

Ninatambua tunateswa na ufukara na wahitaji wa kazi hii ni wengi, lakini jaribuni kuwaonea watoto wa watu huruma. Alienda mbali akasema kuwa atawahudumia chakula. ukweli ni kwamba hawa watu mara nyingi huwalisha wafanyakazi wao
''UKOKO au MABAKI ya chakula pamoja na michuzi.'' mfanyakazi akitaka ale vizuri inabidi akubali akatwe hela kwenye malipo yake.

Sawa hali ni ngumu lakini tuoneane huruma. Pia asilinganishe kazi ya mgahawa na kazi za ndani.
Inahuzunisha sana
 
Kama ungekuwa na hiyo quality ya kulipwa 9Million usingeiomba hiyo kazi.Kutengeneza ajira Siyo jambo jepesi hata nchi ikitaka kuajiri lazima wajipange!

Tuboreshe mazingira ya biashara halafu mapato yakiwa mazuri automatically mishahara itapanda vinginevyo biashara zitafilisika
Hata yangeboreshwa vipi kama mtu kashazoea ukandamizaji ataendelea kuwakandamiza huku yeye na familia yake wakiishi kama peponi.
 
Hata yangeboreshwa vipi kama mtu kashazoea ukandamizaji ataendelea kuwakandamiza huku yeye na familia yake wakiishi kama peponi.
Hujui shida wanazopata wafanyabiashara, akitoka TRA, wanakuja JIJI, wakitoka kuna utitiri wa taasisi zingine, Kama 150,000 ndogo fungua ofisi yako lipa watu 3M Halafu lete mrejesho baada ya mwaka
 
Hujui shida wanazopata wafanyabiashara, akitoka TRA, wanakuja JIJI, wakitoka kuna utitiri wa taasisi zingine, Kama 150,000 ndogo fungua ofisi yako lipa watu 3M Halafu lete mrejesho baada ya mwaka
Mkuu hapo kwenye mgahawa/genge usitake kupotosha. TRA wanafikaje
 
Leo nimesikitika sana baada ya kusoma uzi wa jamaa anayetaka wahudumu wa mgahawani kwa mshahara wa Tsh 2000/= kwa siku kwa hoja kwamba watakula bure mgahawani. Watu wengi kwenye ule uzi wamempinga vikali mleta mada. Mimi pia niliandika comments za kupinga huo ujinga.

Ninawasihi waajiri binafsi watoe ujira ambao mtu anaweza hata kulipa nauli ya daladala na kubakiwa hata na Tsh 2000/= kila siku badala ya huu utumwa wanaoutangaza. Kama biashara yako haina mzunguko mzuri ni bora ukakomaa kivyako na familia yako hadi pale utakapoweza kuajiri mtu mwingine. Au akijitokeza mtu wa kujitolea ndo umlipe hizo posho kuliko kusema eti ni nafasi za kazi wakati ni utumwa mtupu.

Hata wafanyabiashara wakubwa wenye viwanda wanatuhumiwa kulipa mishahara ya chini ya Tsh 5000/= huku watu wakipigika hatari. Utetezi wao ni kwamba wakipandisha mishahara watashindwa kuendesha viwanda. Huu ni uongo mtupu. Hao matajiri ni wabinafsi wasio na utu. Kama kwenye net profit kwa mwaka tajiri anaweza kujinunulia V8 la anasa au kujijengea hekalu anawezaje kusema gharama za ku-run ni kubwa? Pia kusema kodi ni tatizo ninapinga. TRA wanachukua kodi baada ya kuangalia gharama zako za uendeshaji. Ina maana kiasi kidogo utachoongeza kama posho kwa wafanyakazi kitajumuishwa kwenye matumizi ya kampuni na kupelekwa TRA.

Watanzania tupendane na tuache kukandamizana. Kama sisi wa chini tunakandamizana kamwe hatuwezi kuwa kitu kimoja na kukataa ukandamizaji wa baadhi ya viongozi.
Wee jamaa ni hovyo tu.Ni rahisi kuwa mkosoaji kama hivi lakini sio kazi rahisi kuanzisha biashara ambayo utapata pesa ya kulipa wafanyakazi na bado wewe upate faida na biashara iendelee.Hebu jaribu kuanza biashara na uajiri watu,halafu leta mrejeaho hapa kwamba wewe umelipa mashara mnono kama unavyoeleza hapa.
 
Hujui shida wanazopata wafanyabiashara, akitoka TRA, wanakuja JIJI, wakitoka kuna utitiri wa taasisi zingine, Kama 150,000 ndogo fungua ofisi yako lipa watu 3M Halafu lete mrejesho baada ya mwaka
Acha kutetea unyonyaji. Hakuna mtu aliyesema ulipe 3m kwa mwezi. Nimesema mshahara angalau anaoweza kumudu nauli ya daladala na kujibakizia 2000. Hujaelewa nini hapo? Kama huwezi hata kulipa 150k si ufanye hizo kazi mwenyewe au na familia yako? Kuna haja gani ya kulazimisha kuajiri watu huku huwezi kuwalipa?
 
Wee jamaa ni hovyo tu.Ni rahisi kuwa mkosoaji kama hivi lakini sio kazi rahisi kuanzisha biashara ambayo utapata pesa ya kulipa wafanyakazi na bado wewe upate faida na biashara iendelee.Hebu jaribu kuanza biashara na uajiri watu,halafu leta mrejeaho hapa kwamba wewe umelipa mashara mnono kama unavyoeleza hapa.
Wewe mpumbavu nimeanza biashara tangu 2011 hadi leo. Kuanzia 2016 nilianza kuajiri na hakuna mtu niliyewahi kumlipa chini ya 150k tangu mwaka huo. Na kwa sasa hakuna anayepata chini ya 250k. Usidhani nimeandika tu bila kujua ninachoandika.
 
Huwezi kumlipa mtu kiasi kikubwa ili hali faida ni ndogo. Tunagawana gawana kidogo kinachopatikana.

Wapo watu wanalipwa 1500 kwa kutwa na maisha yanaenda.
 
Ningekuwa ni mtunga sera ningehakikisha mishara ya watu hasa wahudumu wa baa na viwandani inapanda. Kuna mishahara ya baadhi ya viwanda ni midogo mno na kazi zina risk kubwa yaani inakuta mmiliki wa kiwanda au baa ana ukwasi mkubwa kwa kunyonya watumishi wake. Ningehakikisha wanaajiri watu wachache ila wanapata maslahi mazuri ili na wao waajiri wengine mashambani au kwenye biashara zao.
 
Huna njaa wewe na hujui unachokiongea. Businesses zina mambo mengi interconnected na calculated alafu wewe unaongea superficially.
 
Mbona unajiita mama samia we ni mwanamke kweli wahuni tukukamie?
 
Back
Top Bottom