Kama mshahara ni chini ya Tsh 150,000/= kwa mwezi bora useme unatangaza nafasi za utumwa kuliko useme ni nafasi za kazi

Kama mshahara ni chini ya Tsh 150,000/= kwa mwezi bora useme unatangaza nafasi za utumwa kuliko useme ni nafasi za kazi

Fikiri.

House girl analipwa 50,000 kwa mwezi, kulala bure, kula bire, umeme bure, sabuni kuanzia ya kufulia mpaka kukogea bure, matibabu bure, kwa ugfupi kila kitu bure. Na mutu anayelipwa 200,000 ambae kila kitu anajilipia mwenyewe, kuanzia kodi ya nyumba na kila mahitaji yake binafsi.

Ipi bora hapo?
Hakuna bora.
 
Kwanza ukipata kazi unashauriwa kukaa karibu na kazi, wahindi wanapesa lakini hawapandi daladala wewe unakaa chamazi halafu kazi mwenge??? Mwisho wa siku hakuna pesa ndogo, Kama unabisha ajiri watu watano kila mmoja alambe Milioni kwa mwezi 😀😀😀bado TRA na marejesho!!!
Una akili timamu?
 
Create jobs,don't criticise people's who create jobs,unajua faida na uwekezaji wake? Unajua analipa kiasi Gani Kodi ya pango,umeme,taka,Ulinzi,service levy,mapato,simu,Zima moto,leseni?
Acha kutetea upumbavu. Kama kampuni haiingizi hela afanye yeye na familia yake.
 
Kama ungekuwa na hiyo quality ya kulipwa 9Million usingeiomba hiyo kazi.Kutengeneza ajira Siyo jambo jepesi hata nchi ikitaka kuajiri lazima wajipange!

Tuboreshe mazingira ya biashara halafu mapato yakiwa mazuri automatically mishahara itapanda vinginevyo biashara zitafilisika
Ndo 2000 bila shaka wewe ni miongoni mwa mafedhuri
 
Leo nimesikitika sana baada ya kusoma uzi wa jamaa anayetaka wahudumu wa mgahawani kwa mshahara wa Tsh 2000/= kwa siku kwa hoja kwamba watakula bure mgahawani. Watu wengi kwenye ule uzi wamempinga vikali mleta mada. Mimi pia niliandika comments za kupinga huo ujinga.

Ninawasihi waajiri binafsi watoe ujira ambao mtu anaweza hata kulipa nauli ya daladala na kubakiwa hata na Tsh 2000/= kila siku badala ya huu utumwa wanaoutangaza. Kama biashara yako haina mzunguko mzuri ni bora ukakomaa kivyako na familia yako hadi pale utakapoweza kuajiri mtu mwingine. Au akijitokeza mtu wa kujitolea ndo umlipe hizo posho kuliko kusema eti ni nafasi za kazi wakati ni utumwa mtupu.

Hata wafanyabiashara wakubwa wenye viwanda wanatuhumiwa kulipa mishahara ya chini ya Tsh 5000/= huku watu wakipigika hatari. Utetezi wao ni kwamba wakipandisha mishahara watashindwa kuendesha viwanda. Huu ni uongo mtupu. Hao matajiri ni wabinafsi wasio na utu. Kama kwenye net profit kwa mwaka tajiri anaweza kujinunulia V8 la anasa au kujijengea hekalu anawezaje kusema gharama za ku-run ni kubwa? Pia kusema kodi ni tatizo ninapinga. TRA wanachukua kodi baada ya kuangalia gharama zako za uendeshaji. Ina maana kiasi kidogo utachoongeza kama posho kwa wafanyakazi kitajumuishwa kwenye matumizi ya kampuni na kupelekwa TRA.

Watanzania tupendane na tuache kukandamizana. Kama sisi wa chini tunakandamizana kamwe hatuwezi kuwa kitu kimoja na kukataa ukandamizaji wa baadhi ya viongozi.

Ndiyo maana wanasema ni watumishi wa umma. Siyo wafanyakazi.
 
Hujui shida wanazopata wafanyabiashara, akitoka TRA, wanakuja JIJI, wakitoka kuna utitiri wa taasisi zingine, Kama 150,000 ndogo fungua ofisi yako lipa watu 3M Halafu lete mrejesho baada ya mwaka
Hajasema analipa hela zake ila mapato yaendane na matumizi ikiwamo mishahara.
 
Ukisoma comments za wengi hapa ni kama wanaupenda umaskini na kuwatetea wanyonyaji. Kimsingi watu wengi hawajui wanataka nini kwenye haya maisha.
Sio wanatetea wengi wao ndo wale mafedhuri waliojaa humu kuna watu humu wanatabia za ajabu sana kueni makini na waajiri wa humu ndani ni machoko tu humu wamekaa kama watu kumbe inreality machoko ofisini kwao uozo tu na utapeli
 
Kwanza ukipata kazi unashauriwa kukaa karibu na kazi, wahindi wanapesa lakini hawapandi daladala wewe unakaa chamazi halafu kazi mwenge??? Mwisho wa siku hakuna pesa ndogo, Kama unabisha ajiri watu watano kila mmoja alambe Milioni kwa mwezi 😀😀😀bado TRA na marejesho!!!
Chenye unaongea sidhani hata kama unaelewa au simu imejitype sasa umeongea nn hapo?
 
Create jobs,don't criticise people's who create jobs,unajua faida na uwekezaji wake? Unajua analipa kiasi Gani Kodi ya pango,umeme,taka,Ulinzi,service levy,mapato,simu,Zima moto,leseni?
So kuweza kulipa vyote hvo kwanini asipunguze na kustandardize mishahara wewe ni walewale 😂
 
Back
Top Bottom