Kama Msola ni Simba, basi Utopolo mmekwisha

Kama Msola ni Simba, basi Utopolo mmekwisha

kibaravumba

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2012
Posts
6,634
Reaction score
7,015
Nimesikia mahojiano na mpenzi wa utopolo aliyekuwa kama amechanganyikiwa, muasisi wa jina la "utopolo" akidai Dr Mshindo Msola ana kadi ya Simba.

Kama wanayanga wana akili za jinsi hii, basi iko siku nayo si mbali GSM anatimuliwa. Maana naye ni Simba. Hawa utopolo wanapenda sana kuchanga elfu moja moja.

Awali mlilaumu waamuzi mara TFF,mara bodi ya ligi.Sasa baada ya kupewa penalty,goli a kuotea,na kubebwa kama watoto,mmehamishia vita yenu kwa viongozi wenu.Poleni sana
 
Siyo GSM hata baadhi ya wachezaji wao mioyo yao iko simba kama yule goalkeeper na defender mmoja...😁
 
Wachezaji wa uto wote wanatamani kwenda Simba hata wakawe ball boys bahati mbaya kwao hakuna nafasi, hata mashabiki wao nao wanaona aibu tu lakini kimoyomoyo ni mashabiki wa mnyama.
 
Kama wanayanga wana akili za jinsi hii,basi iko siku nayo si mbali GSM anatimuliwa.Maana naye ni Simba.
Nafikiri mambo ya upenzi yaishie kwenye ngazi ya uongozi tu, kwenye udhamini na ufadhili kusiwepo kuangalia nani ana kadi gani. Kama wadhamini wataanza kuchunguzwa, vilabu vitapoteza udhamini mwingi tu. Hersi wangemtoa kwenye kamati zao ila wamuache awepo kibiashara tu kama mdhamini kupitia GSM
 
Kuna kipindi Yanga ilikuwa na magolikipa wazuri watatu; Dida, Bartez na Kaseja. Kati ya hao, Bartez na Kaseja walijulikana waziwazi kuwa ni wekundu ila Dida hakujulikana, na hata wakikaa golini dhidi ya Simba mashabiki wa Yanga wanakuwa na wasiwasi kama mtu anayechemsha maziwa
 
Mwisho hii yanga itakuwa Mali ya Simba,maana hata uchebe wanafikiria kumleta ni mwanachama wa Simba.
Kama wakimleta tu,na akafungwa,habari itabadilika.
 
Wachezaji wa uto wote wanatamani kwenda Simba hata wakawe ball boys bahati mbaya kwao hakuna nafasi, hata mashabiki wao nao wanaona aibu tu lakini kimoyomoyo ni mashabiki wa mnyama.
Hata washabiki wa upotolo wanatamani kuhamia Simba ila tumewakataa kwani hatupendi vurugu
 
Back
Top Bottom