Hizi nadharia zimewahi kukusaidia kwenye maisha yako? Umewahi kukutana nazo kwenye shughuli za kila siku za maisha yako?
Hata waliokimbia Kemia shuleni unawakuta kwenye viti virefu na meza za mashua wana dilute K-VANT na MO-Energy utadhani ni Mkemia wa serikali!!!
Ni Geometry ndiyo unakutana nazo kwenye maisha hata kabla hujaanza shule chekechea lakini utafanya Geometry kwa kutengeneza nyumba na gari za udongo, gari za mabua, miti, mbao na katani.
Hii uliyoileta hapa na zingine zinazofanana nayo ni matokeo ya Knowledge Based Curriculum KBC na siyo Competency Based Curriculum CBC ambayo dunia ndiyo sasa inaikimbilia kuiasili kama mtaala unaofaa kuendana na kasi na agenda ya sayari.
CBC walianza Malaysia Kenya wakawahi kuiasili na kuitekeleza na sisi Tz ndiyo tumeianza japo hatuna bajeti ya kutosha kuitekeleza 100% mfano siyo Walimu wote wamefunzwa CBC na pia vitabu vya kiada na ziada havijaandikwa vya kutosha na weledi bado una mashaka kwa maana kwamba vitabu vingi vina kasoro kwamba kumbe hata waandishi wa vitabu nao walipaswa kupewa mafunzo kabla ya kuandika.
Sent from my SM-A260F using
JamiiForums mobile app