Kama muda ukirudi nyuma na ukapewa nafasi ya kubadili future yako, kwa upande wako utafanya nini?

Kama muda ukirudi nyuma na ukapewa nafasi ya kubadili future yako, kwa upande wako utafanya nini?

Rayamikhal

Senior Member
Joined
Sep 14, 2026
Posts
110
Reaction score
207
WanaJf ni muda sasa wakuwekana wazi siku ya leo. Kila nafsi ya mtu moyoni amejaza Siri nyingi sana na yenye kuumiza moyo, wengine majuto🙁 wengine vilio🙁 wengine mikosi 🙁

Wanasaikolojia walifika tamati na kusema maisha ya binadamu yoyote huchukua mabadiliko na kuanza kuandaa future kwenye miaka ya 10's yaani kwanzia umri wa miaka 10 ndio kila mtu huchukua aina yake ya maisha, mtindo wake wa mavazi, namna ya kuongea ubaya kwa uzuri. Na pia katika miaka ya 10's hatima ya mtoto huwa Mara zote chini ya wazazi, Hivyo basi wazazi ndio wanachangia kwa asilimia kubwa sana kwenye kuyatengeneza na kuyaharibu maisha ya watoto wao.

Kwanini mzazi kutakiwi kumsema mwenza wako mbele ya mtoto? Kwanini mzazi hamtakiwi kugombana, kuachana au kuonesha sintofahamu yoyote mbele ya mtoto? Sababu huwa ni moja huenda mkawa watuhumiwa wakuu katika uharibifu wa mtoto huyo.

Mfano mzuri kilamzazi na malezi yake ndio tabia za mtoto hasa wakiwa shule kipindi Cha darasa la 4 hadi 6 watoto huonesha tabia ambazo nizaajabu na takwimu inathibitisha kuwa hayo yote huwa ni matokeo ya tabia za wazazi wao majumbani.

Matokeo mengi sana hivi karibu yamekuwa ni ya watoto kujinyonga, wanandoa kuuwana kila Kona habari ni hizohizo kwanini?

Mimi pia ni muhanga kwenye hili kadili ninavyosoma vitabu vya philosophy zaidi ninavyogundua niliharibu personality yangu around 10. Guys! Hakuna Jambo gumu maishani kama kubadilika,, Mara nyingi unasema nataka kubadilika, nataka kubadilika lakini haubadiliki kwanini? Sio kwasababu hutaki au unashindwa shida ni kwamba kubadilika ndio kazi kubwa zaidi kwenye maisha ya mwanadamu hasa anapokuwa amevuka umri wa 10's na 20's hapo kubadilika no forever "no" ndio maana wengine huishia kujikubadili namna walivyo kwasababu walijaribu kubadilika na kuona wanakuwa watu tofauti na wanavyojifahamu.

Hitimisho la kubadilika ni Nini? Malezi! Huenda vijana wengi wanajiua kwasababu ya malezi, umasikini umezidi kwasababu ya malezi, ugonjwa wa akili umezidi sababu ni malezi hivyo basi kwanini usibadilishe mfumo wako wa malezi ili kuboresha kesho ya mtoto wako.

Muda mwingine tuache kufuata kauli za kijinga kwamba namna ya kumtrain mtoto ni kwa kumpiga kilawakati, kumtukana matusi kilamuda, kutishia maisha, na kumnyima haki zake za msingi,,, vijana, wazee na wazazi ingieni mjifunze malezi ya watoto wenu.... Wengine mpaka leo tumeshindwa kusahau matendo mabaya tuliotendewa na wazazi wetu wenyewe na tumebaki kujutia hilo kilasiku kwanini usibadili kesho ya mwanao kwa kusahau yaliyopita na kumlea vizuri zaidi ya alivyofanya baba au mama yako.

Wengine hawakupata bahati kabisa ya kulelewa na wazazi wao maana walifariki, kwa heshima kubwa wapumzike kwa amani na huenda ombi lao la kilasiku ni kutamani wangerudisha nyuma muda at least wafurahie muda mzuri na wazazi wao au waepushe vifo ambavyo huenda vingetokea.

Kesho ya kila mmoja ipo mikononi mwetu, kuibadilisha ni kazi yetu kama tumeshindwa kujibadilisha sisi na kuwa watu wazuri tena basi tunaweza kubadili maisha ya watoto wajao... Kwenye haya maisha hakuna mtu Yuko pekeyake basi kama sio Leo au Jana ni kwa ajili ya familia itakayokuwa nayo baadae.

Tujaribu kufanya Mambo kwa usahihi sana hasa malezi.

Basi wewe niambie,,kama muda ungerudi nyuma ungebadilisha nini?

~rayamikhal
 

Attachments

  • Screenshot_20261012-161659.jpeg
    Screenshot_20261012-161659.jpeg
    31 KB · Views: 7
Sema muandiko wako

Ila kuwa chochote ni kuwa mwenyewe

Ili kama kariba yako ni u hayawani tukuemineti mapema
 
That's beauty of life ,Kama Kila mtu angefanya mambo yake namna inatakiwa Kuna mambo mengi yasingetokea ,Kuna maamuzi yasiyo sahihi unafanya lakini yanakusaidia baadae kukujenga kuwa imara zaidi ,Kuna experience unapitia zitakusaidia uwasaidie wengine wasipitie uliyopitia , Maisha ni funzo katikati Kila hatua ndio maana mwanadamu huacha kujifunza pale tu anapoacha kupumua.
 
Back
Top Bottom