Kama muda wa kuandika Katiba mpya hautoshi, mbona wa kuuza Bandari na kufukuza wamasai ulitosha?

NAMBA MOJA AJAYE NCHINI

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2019
Posts
9,863
Reaction score
20,806
Ninawasanua makada wenzangu wa chama chetu CCM, hebu tujaribu kulijibu hilo swali kimantiki!!

Hoja za lissu tumeshindwa kujibu na hilo swali tunaweza kulijibu?

Ifikie hatua tuache kujibu mipasho masuala mtambuka ya kitaifa na nchi yetu Kwa ujumla.

Mzee Warioba ni mwanaccm na anaitaka Katiba mpya wewe hutaki katiba unasema eti katiba haileti ugali mezani. Sasa mkataba wa bandari umeleta ugali wa nani mezani? wamasai kufukuzwa ngorongoro kumesaidia ugali wa nani mezani?

Wanaccm hasa kizazi hiki chetu tuache kujizima data,vkatiba kwasasa inatakiwa sio tu na watanzania hata wanyamapori, majani, mawe, mchanga, maji bahari na vyote vinaitaka katiba mpya!!

Kama tuna akili timamu hatuwezi enda kwenye uchaguzi bila katiba mpya.

Tuendelee kushupaza shingo kwa uchawa usio na maana lakini kampeni zikianza tutaulizwa maswali hayo hapo juu na tukishindwa kuyajibu basi andaeni vyombo vya dola kushindisha chama awamu ijayo.

Nimewasanua sanukeni kama vipi!
 
nikieendelea kusubiri makada wa ccm mdaa huu waje
 
Mtanzania yeyote yule, bila ya kujali chama, alimradi ana akili timamu na anaipenda Tanzania, anaunga mkono hoja za Lisu, anaunga mkono kazi kubwa ya kutukuka iliyofanywa na Tume ya Warioba.

Hakuna mwanaCCM mwenye akili timamu utakayemsikia kupinga hoja za Lisu. Ni wale wajingawajinga wanafiki ndio utawasikia wakipiga kelele bila hoja.

WanaCCM wanaofahamika kuwa na akili na uzalendo kwa nchi kama Jaji Warioba, Butiku, Prof. Shivji, au Prof. Tibaijuka hutawasikia wakiilalamikia hoja ya Lisu kuhusiana na Muungano. Ni hawa wapuuzi wanafiki wanaojiita machawa ndio utawasikia wanapiga kelele.
 
Wanajua mafuriko nchini yanaashiria nini kiroho lakini wanapuuza!!

Msimu mpya umeingia,

Tusubiri.
 
Ninawasanua makada wenzangu wa chama chetu CCM, hebu tujaribu kulijibu hilo swali kimantiki!!

Hoja za lissu tumeshindwa kujibu na hilo swali tunaweza kulijibu?

Ifikie hatua tuache kujibu mipasho masuala mtambuka ya kitaifa na nchi yetu Kwa ujumla.

Mzee Warioba ni mwanaccm na anaitaka Katiba mpya wewe hutaki katiba unasema eti katiba haileti ugali mezani. Sasa mkataba wa bandari umeleta ugali wa nani mezani? wamasai kufukuzwa ngorongoro kumesaidia ugali wa nani mezani?

Wanaccm hasa kizazi hiki chetu tuache kujizima data,vkatiba kwasasa inatakiwa sio tu na watanzania hata wanyamapori, majani, mawe, mchanga, maji bahari na vyote vinaitaka katiba mpya!!

Kama tuna akili timamu hatuwezi enda kwenye uchaguzi bila katiba mpya.

Tuendelee kushupaza shingo kwa uchawa usio na maana lakini kampeni zikianza tutaulizwa maswali hayo hapo juu na tukishindwa kuyajibu basi andaeni vyombo vya dola kushindisha chama awamu ijayo.

Nimewasanua sanukeni kama vipi!
MAFISADI WA CCM HAWAITAKI KATIBA MPYA ITAVURUGA WIZI WAO
 
Back
Top Bottom