Kama Mungu hayupo, binadamu katokea wapi?

Kama Mungu hayupo, binadamu katokea wapi?

Kwahiyo ukimchukua mke/mume wako mkaenda ivory cost mkazaa mtoto atakuwa na mwili mkubwa?
Au mkaenda uingereza atakuwa mweupe sababu ya tabia ya nchi husika?

Mkizaa mtt kule akakulia kule akala vyakula vya kule hali ya hewa ya kule atakua Giant tu.
 
Kwahiyo huyo Mungu ameshindwa kumdhibiti huyo Shetani na mabaya yake ili ulimwengu uwe peace?

kwanini ulimwengu uwe peace na usiwe na maovu?kipimo cha kumdhibiti unakifahamu wewe?unampangiaje yeye ilhali hata wewe hujijui?halafu nachoshangaa huyo unayemzungumzia unamjua au ?na unataka umjue ili iweje ?ilhali umekiri hayupo?au unaogopa
 
This is too low for broda REALITY ,unajua karne hii ya 21 ni ajabu sana kukutana na MTU mwenye mawazo kama Hays .Kama mabaya ni ya shetani sasa nani aliyepanga kwamba mabaya yawe ya shetani,,je shetani ana mamlaka zaidi ya mungu wako?,Je nikisema ili mungu awepo lazima na shetani awepo nitakuwa wrong?

tatizo we unadhani life is a circular movement ,life is an infinity rail with puzzles each to be solved in every stage it reaches on a rail,shetani alikuwa malaika na ni mdhaifu ndo maana alitokea kinywani mwa mungu i mean kutajwa lakini alipewa mamlaka makuu na uhuru ,tatizo Mungu kutuumba sisi wa mwisho yule malaika akaona wivu why them GOD atumie all effort to them ,akasema why sisi tusiwe na thamani hivyo na tu karibu ?na ndo hapo akahasi akijua ana uwezo mkubwa wa kushindana na aliyemleta kwa kuwa anauhuru,nguvu na sifa za malaika,kuwepo Mungu si lazima shetani awepo period
 
Last edited by a moderator:
Nani kamuumba huyo shetani? Kama ni mungu, inamaanisha hakujuwa kama atakuwa mleta maovu duniani huyu shetani?na kwanini asimdhibiti ili tuwe salama?

Mungu kaumba malaika ila yule malaika kahasi na kuwa kinyume na muumba wake ndo kuwa shetani,kuhusu mleta maovu ni sawa ila mlaumu hawa sio aliyewaumba maana waliambiwa msile tunda la mema na mabaya mkila mtajionea na mtakufa ,hapo nani alaumiwe?ukitaka kuwa salama kuwa salama si unayo akili na maarifa
 
Mkizaa mtt kule akakulia kule akala vyakula vya kule hali ya hewa ya kule atakua Giant tu.

Mbona waafrica walioko marekani hawajawa weupe miaka yote?

Au makaburu walioko south Africa hawajawa weusi?
 
Mungu kaumba malaika ila yule malaika kahasi na kuwa kinyume na muumba wake ndo kuwa shetani,kuhusu mleta maovu ni sawa ila mlaumu hawa sio aliyewaumba maana waliambiwa msile tunda la mema na mabaya mkila mtajionea na mtakufa ,hapo nani alaumiwe?ukitaka kuwa salama kuwa salama si unayo akili na maarifa

Nakuuliza, je mungu hakujuwa kama shetani ata hasi nakusababisha madhara yote?
Ww unayoongelea maovu unaongekea kuhusu moral evils kuna evils zaina nyingi kama metaphysical evils mfano Earth Quake, deformed creatures, Animal sufferings,hizi zote ni evils ambazo kwa namna youote binadamu hausika.
 
kwanini ulimwengu uwe peace na usiwe na maovu?kipimo cha kumdhibiti unakifahamu wewe?unampangiaje yeye ilhali hata wewe hujijui?halafu nachoshangaa huyo unayemzungumzia unamjua au ?na unataka umjue ili iweje ?ilhali umekiri hayupo?au unaogopa

Sihitaji kujua kipimo cha kumdhiti shetani. Ulisema mabaya sio ya Mungu ni ya shetani nikakuuliza kwahiyo huyo Mungu ameshindwa shetani? We badala ya kujibu umekuja na hekaya.
Sina haja ya hadithi kama huna jibu kaa kimya tu

Unavyodhani kuna sababu yoyote ya kuogopa kitu kisicho kuwepo?
 
Jaribuni Kusoma hapa baadhi ya madhaifu katika biblia ambayo mnasema ni kitabu cha mungu.

THE BIBLICAL ACCOUNT
OF CREATION
A Young Earth?
Genesis 1:16 God made two great lights?the
greater light to govern the day and the lesser
light to govern the night. He also made the
stars. God set them in the expanse of the sky
to give light on the earth.
The stars gave light to the earth immediately,
although the closest star, Alpha Centauri, is 4.3
light years away. So the very first star light
would have taken 4.3 years to reach earth. The
light we see from the Andromeda Galaxy takes
2.2 million years to reach earth, which also
debunks the argument that the earth is only
6,000-10,000 years old.
The Order of Creation
Genesis 1:11-12 and 1:26-27 Trees came
before Adam.
Genesis 2:4-9 Trees came after Adam.
Genesis 1:20-21 and 26-27 Birds were created
before Adam.
Genesis 2:7 and 2:19 Birds were created after
Adam.
Genesis 1:24-27 Animals were created before
Adam.
Genesis 2:7 and 2:19 Animals were created
after Adam.
Genesis 1:26-27 Adam and Eve were created
at the same time.
Genesis 2:7 and 2:21-22 Adam was created
first, woman sometime later .
Back to top ↑
Other Issues in the Garden
Genesis 1:31 God was pleased with his
creation.
Genesis 6:5-6 God was not pleased with his
creation.
Which raises the question, how can an
omnipotent, omniscient God create something
he?s not pleased with?
Genesis 2:3 Then God blessed the seventh
day and made it holy, because on it he rested
from all the work of creating that he had
done.
An omnipotent being required?rest?
Genesis 2:16-17 And the Lord God
commanded the man, "You are free to eat
from any tree in the garden; but you must not
eat from the tree of the knowledge of good
and evil, for when you eat of it you will surely
die."
God placed temptation in the direct path of his
two na?ve children and allowed them to be
tempted by the serpent (Genesis 3: 1-7),
resulting in a single mistake that would
contaminate hundreds of billions with a sin
nature worthy of eternal torture?
Genesis 3:1 Now the serpent was more crafty
than any of the wild animals the LORD God
had made. He said to the woman, "Did God
really say, ?You must not eat from any tree in
the garden??"
A talking snake. Enough said.

Ngoja nipitie moja moja mkuu
 
Sihitaji kujua kipimo cha kumdhiti shetani. Ulisema mabaya sio ya Mungu ni ya shetani nikakuuliza kwahiyo huyo Mungu ameshindwa shetani? We badala ya kujibu umekuja na hekaya.
Sina haja ya hadithi kama huna jibu kaa kimya tu

Unavyodhani kuna sababu yoyote ya kuogopa kitu kisicho kuwepo?

sibadili hata moja nililoandika period
 
Kwa muda mrefu nimekua nikisikia watu wengi wakikanusha uwepo wa Mungu na wakatoa evidence nyingi tu katika ukanushaji huo especially Jamii inteligence.Sasa kwenye hili bandiko mi nataka kufaham kama Mungu hayupo huyu binadamu aliyemuumba ni nani? au kajileta mwenyewe hapa duniani. Unajua hata ukiliona gari barabani yupo aliyeunda gari hilo. Wanasayansi wanaopinga uwepo wa mungu wamejitahidi kueleza sana asili ya dunia na vitu vingine vingi. Naomba izingatiwe kwamba nataka kufahamu asili ya mwanadam sio mungu. ni kweli mungu anaweza akawa hayupo je binadamu wa kwanza alimuumba nani? uje na lengo la kuelimishana. nawasilisha.

Dr. Aluta

Swali lako ni gumu kulijibu kwa ufupi. Kadri ninavyofahamu mimi wanasayansi wanazungumza mada mbili moja ni uwepo wa Mungu na mada nyingine ni kuhusu Mungu huyu kuwa chanzo cha viumbe vyote. Ukitaka kuelewa dhana yote kama wanavyoielezea kwa kweli utatakiwa kuvitafuta vitabu walivyoviandika. Vipo vitabu vingi sana ambavyo vimeelezea asili ya viumba na binadamu. Kwa ufupi wanasema viumbe vyote vimetokana na viumbe vya awali vilivyozuka miaka zaidi ya bilioni 3 iliyopita. Katika miaka yote hiyo viumbe vya awali vilipitia mabadiliko (evolution) yaliyosababishwa na mazingira ya mahali ambapo viumbe hivyo vilijikuta vipo katika uso wa dunia hii. Wanaendelea kusema mwanadamu wa sasa anatokana na kiumbe aliyekuwapo hapo kale ambaye hakuwa na uwezo wa akili tulio nao. Kwa maana nyingine mwanadamu, sokwe na sokwe mtu ni mabinamu. Wanasema miaka zaidi ya milioni 2 iliyopita alikuwepo kiumbe ambaye ni chanzo cha hawa watatu. Kwamba viumbe wa sasa wanatokana na viumbe wa kale sana walioishi baharini inathibitishwa na ukweli kwamba viumbe vyote iwe mimea au bacteria au wanyama au fungi wanajirithisha kwa kutumia DNA yenye molekyuli 4 ( Guanine, Adenine, Cytosine na Thymine). Hivyo wanasayansi hawa wanasema binadamu anatokana na kiumbe wa awali ambaye yumkini huko nyuma kama ingewezekana kumwona pengine angefanana na sokwe wa sasa. Wanasema mabadiliko (evolution) hutokea taratibu sana pengine miaka zaidi ya 250,000 kwa tukio moja hivyo sisi wenye maswali mengi hatuwezi kuyaona kwani wengi wetu tunaishi si zaidi ya miaka 85.

Ukitaka kufahamu zaidi soma vitabu vifuatavyo: The Greatest Show on Earth na The Ancestors Tale vilivyoandikwa na Richard Dawkins. Pia soma kitabu cha Charles Darwin cha On the Origin of Speies. Vitabu hivi havitakata kiu yako juu ya maswali yako lakini naamini vitaenda mbali sana kupanua uelewa wako juu cha asili ya viumbe.
 
Mungu kaumba malaika ila yule malaika kahasi na kuwa kinyume na muumba wake ndo kuwa shetani,kuhusu mleta maovu ni sawa ila mlaumu hawa sio aliyewaumba maana waliambiwa msile tunda la mema na mabaya mkila mtajionea na mtakufa ,hapo nani alaumiwe?ukitaka kuwa salama kuwa salama si unayo akili na maarifa

Ndugu REALITY unachoandika hapa hakina mashiko,Unaweza kunambia yule malaika aliyeasi na kwenda kinyume na mungu alitoa wapi lile wazo la kuasi wakati hakukuwa na shetani mwingine?.,Maana ikiwa mungu ni mwema na kila alichokiumba kilikuwa chema ilikuwaje malaika akapata wazo ovu?

Habri za kula tunda LA mti hazina uhalisia ni hadthi za kutunga kwa kuwahazimfanyi huyo mungu kuwa all knowing,. Maana ikiwa alijua kabisa kwamba Adam na hawa watakula tunda kwa nini awahukumu kwa kitu alichopanga yeye?,
Lakini pia mungu wao anaonekana muongo kwa kuwa alisema wakila watakufa badala yake shetani anaonekana mkweli kwamba wakila watajitambua ,,
.........karibu katika ulimwengu Huru....
 
Last edited by a moderator:
Dr. Aluta

Swali lako ni gumu kulijibu kwa ufupi. Kadri ninavyofahamu mimi wanasayansi wanazungumza mada mbili moja ni uwepo wa Mungu na mada nyingine ni kuhusu Mungu huyu kuwa chanzo cha viumbe vyote. Ukitaka kuelewa dhana yote kama wanavyoielezea kwa kweli utatakiwa kuvitafuta vitabu walivyoviandika. Vipo vitabu vingi sana ambavyo vimeelezea asili ya viumba na binadamu. Kwa ufupi wanasema viumbe vyote vimetokana na viumbe vya awali vilivyozuka miaka zaidi ya bilioni 3 iliyopita. Katika miaka yote hiyo viumbe vya awali vilipitia mabadiliko (evolution) yaliyosababishwa na mazingira ya mahali ambapo viumbe hivyo vilijikuta vipo katika uso wa dunia hii. Wanaendelea kusema mwanadamu wa sasa anatokana na kiumbe aliyekuwapo hapo kale ambaye hakuwa na uwezo wa akili tulio nao. Kwa maana nyingine mwanadamu, sokwe na sokwe mtu ni mabinamu. Wanasema miaka zaidi ya milioni 2 iliyopita alikuwepo kiumbe ambaye ni chanzo cha hawa watatu. Kwamba viumbe wa sasa wanatokana na viumbe wa kale sana walioishi baharini inathibitishwa na ukweli kwamba viumbe vyote iwe mimea au bacteria au wanyama au fungi wanajirithisha kwa kutumia DNA yenye molekyuli 4 ( Guanine, Adenine, Cytosine na Thymine). Hivyo wanasayansi hawa wanasema binadamu anatokana na kiumbe wa awali ambaye yumkini huko nyuma kama ingewezekana kumwona pengine angefanana na sokwe wa sasa. Wanasema mabadiliko (evolution) hutokea taratibu sana pengine miaka zaidi ya 250,000 kwa tukio moja hivyo sisi wenye maswali mengi hatuwezi kuyaona kwani wengi wetu tunaishi si zaidi ya miaka 85.

Ukitaka kufahamu zaidi soma vitabu vifuatavyo: The Greatest Show on Earth na The Ancestors Tale vilivyoandikwa na Richard Dawkins. Pia soma kitabu cha Charles Darwin cha On the Origin of Speies. Vitabu hivi havitakata kiu yako juu ya maswali yako lakini naamini vitaenda mbali sana kupanua uelewa wako juu cha asili ya viumbe.

Mkuu haya ndo majibu tuliyokua tunayatafuta toka mada ianze!! Hongera sana na ubarikiwe
 
Mungu hakuanza alikuwepo tangu awali, kwa Mungu hakuna kitu kinaitwa muda.
 
Mungu hakuanza alikuwepo tangu awali, kwa Mungu hakuna kitu kinaitwa muda.

Kumbe zile hadithi za kwenye vitabu fulani za mungu kutumia muda wa siku 6 kuumba na ya 7 akapunzika ni uongo walioutunga kina Musa sio?
 
umeuliza swali a binadamu wa kwanza. kwani huyo binadamu aliumbwa wapi? mbona kuna wakorea,wachina,waafrika,wazungu? mbona wa ivory cost wana miili mikubwa kuliko watz? kama walitokana na binadamu wa kwanza kwa nini watofautiane.
jambo dogo sana kwa aliye umba minaadamu wanyama na malaika.
 
Kwa muda mrefu nimekua nikisikia watu wengi wakikanusha uwepo wa Mungu na wakatoa evidence nyingi tu katika ukanushaji huo especially Jamii inteligence.Sasa kwenye hili bandiko mi nataka kufaham kama Mungu hayupo huyu binadamu aliyemuumba ni nani? au kajileta mwenyewe hapa duniani. Unajua hata ukiliona gari barabani yupo aliyeunda gari hilo. Wanasayansi wanaopinga uwepo wa mungu wamejitahidi kueleza sana asili ya dunia na vitu vingine vingi. Naomba izingatiwe kwamba nataka kufahamu asili ya mwanadam sio mungu. ni kweli mungu anaweza akawa hayupo je binadamu wa kwanza alimuumba nani? uje na lengo la kuelimishana. nawasilisha.
kunaishara nyingi zinazoonesha mungu yupo.. Angalia solar system sayari zinazunguka bila kugongana yaani ipo kama system flani iliyo tengezwa kwa upande wa mwanadamu angalia biochemistry yake anatomy yake utaona kweli huu ni mfumo ulioumwa na aliyetuumba.. Binaadamu na viumbe vingine vinamfumo wa kula kunywa kupumzika kulala kuzaana na kufa.. Ingetokea kunampishano kwa maana pangekuwa na binaadamu hali au hanywi na tofauti zingine basi tungesema tumetokea kbahati mbaya au bahati nasibu.. Lakini ukiangalia compexity ya maumbile ya binaadamu baaas unapata jibu kuwa hii complex structure haijajiumba yenyewe kwa nyungunyungu kama wasemavyo wale scientist wa zamani..SASA KAMA HAJAUBWA ALITOKEA TUU MBONA SASAHIVI HATOKEI TUU.. NATAKA NISIKIE MTU AMETOKEA KWENYE MTARO AU JALALANI NTAAMINI KWELI BINAADAMU HAJAUBWA..
 
kunaishara nyingi zinazoonesha mungu yupo.. Angalia solar system sayari zinazunguka bila kugongana yaani ipo kama system flani iliyo tengezwa kwa upande wa mwanadamu angalia biochemistry yake anatomy yake utaona kweli huu ni mfumo ulioumwa na aliyetuumba..
Solar system inaelezeka kwa nini iko vile na sio maajabu San kuwa vile,sijui kama unauelewa was physics.

Binaadamu na viumbe vingine vinamfumo wa kula kunywa kupumzika kulala kuzaana na kufa.. Ingetokea kunampishano kwa maana pangekuwa na binaadamu hali au hanywi na tofauti zingine basi tungesema tumetokea kbahati mbaya au bahati nasibu.. Lakini ukiangalia compexity ya maumbile ya binaadamu baaas unapata jibu kuwa hii complex structure haijajiumba yenyewe kwa nyungunyungu kama wasemavyo wale scientist wa zamani..SASA KAMA HAJAUBWA ALITOKEA TUU MBONA SASAHIVI HATOKEI TUU.. NATAKA NISIKIE MTU AMETOKEA KWENYE MTARO AU JALALANI NTAAMINI KWELI BINAADAMU HAJAUBWA..

Mfumo wa kula na kunywa sijui na vitu gani inaelezeka pia,
Hoja ya kwamba"" Ingetokea kunampishano kwa maana pangekuwa na binaadamu hali au hanywi na tofauti zingine basi tungesema tumetokea kbahati mbaya au bahati nasibu."" Haina mashiko kwa kuwa kuna wanyama ,wadudu n.k na tuko tofauti kimfumo
Lakini pia inasemekana katika ulimwengu kuna uwezekano was kuwepo viumne wengu katika safari ama Galax za mbali we unaonaje hilo?.Lakini pia juz tu NASA wamegundua uwezekano wa maisha sayat ya Mars sasa anzeni kuandaa biblia na Koran za kupeleka huko kisha mseme mungu(kama yupo)aliumba dunia na mars kisha.

Karibu katika ulimwengu huru
.........Free ideas......
 
Mungu hakuanza alikuwepo tangu awali, kwa Mungu hakuna kitu kinaitwa muda.

Who told you?,umeyajuaje haya ?,tushirikishe na sisi basis ndugu?Siri zake unazitoa wapi?,Sio nyie mnaosema god is beyond our thinking capacity?
 
Back
Top Bottom