First thing first, sitaki kuamini. Nataka kujua.
Kuamini unaruhusiwa kuamini chochote. Amini the earth is flat. Amini Santa Claus lives on the North Pole. Amini Che Guevara yupo msukule Dodoma anaishi.
Unaruhusiwa. Kuna maazimo ya Umoja wa Mataifa yanayotetea haki yako ya kuamini, ilimradi huvunji sheria. Katiba ya Tanzania inatetea haki yako ya kuamini unachotaka, mradi huvunji sheria. Mimi mwenyewe natetea uhuru wako wa kuamini unachotaka, mradi huvunji sheria.
Lakini tukija kwenye ujuzi katika framework ya logical thinking, ukitaka kuanza kusema mungu yupo, lazima utoe sababu, ushahidi na uhakiki wa kueleweka.
So far hakuna aliyeweza kuonesha mungu yupo kwa minajili hiyo.