Kuamini Mungu yupo wakati hamna chochote kuna athari nyingi sana:
1.Kwanza unaishi kwa hofu ukihofia kwamba una uwezekano wa kwenda motoni siku ya mwisho ili hali hamna aliyewahi kuona huo moto.
2.Unapoteza muda kumwomba Mungu ili hali kupata kitu ni probability...ukichunguza utagundua kusali ni kama kurusha jiwe gizani, unaweza kulenga target au kukosa...Hata wewe mwenyewe ni shahidi, siyo kila ulichoomba ulipata.Ila baada ya kukosa ulijipa visababu mf. haukuwa mpango wa Mungu mimi kupata kitu flani.
3.Ukiamini kwa Mungu una postpone maisha.Badala ya kuishi na kufurahia maisha ya duniani unatumia muda na gharama nyingi kuanda maisha ya baadae...eti unaanda maisha ya uzima wa milele, mbona hukujiandalia maisha ya kuja kuishi hapa duniani kabla haujazaliwa???
4.Kumwamini Mungu ni kuleta chuki, mf sehemu nyingi wakristo na waislam hawapatani, waislam na waislam hawapatani, wakristo kwa wakristo hawapatani wana madhehebu zaidi ya 35000 na kila mmoja anadai dhehebu lake ni bora zaidi.Unafikiri chanzo cha huo ugomvi ni nini kama siyo Mungu??? kama watu wasingekuwa na dini, vita vya kidini vingetoka wapi???
5.Kumwamini Mungu unapoteza resources muhimu kama muda na pesa.Yaani badala ya kutumia muda wako ukifanya mambo ya faida kwako na kwa vizazi vijavyo, wewe unashinda na kukesha kwenye nyumba za ibada.Pesa unayotafuta kwa jasho na kuichokea unaambiwa uitoe kiurahisi tu eti utaongezewa mara mia...kwanini wao wasitoe ili waongezewe mara mia??? wananyonya pesa za waumini wakiziita fungu la kumi. sadaka au michango ya ibada. Kama unajisikia kutoa kitu, wape ombaomba na siyo hao mamwinyi wanaomiliki dini
Kuamini kwa Mungu au kwa Shetani kuna hasara zisizo na idadi.