Naomba nitumie mfano mwingine kueleza jambo(dhana ya uwepo au kutokuwepo)Mungu:
1.Leo mtu anaunda gari kule Japan kwa mfano.Ili wewe ujue au ulione hilo gari Tanzania ni lazima lifike Tanzania.Sasa tujiulize maswali yafuatayo:
1.Kama usingeweza ona gari hilo Tanzania kunaondoa ukweli kuwa kumekuwa na gari kama hilo kule Japani?
2. Je kunaondoa ukweli kuwa kuna mtu alitengeneza gari huko Japan? Nina maana kuwa kunaondoa ukweli kuwa Mjapani ndiye Essence (kiini/mwanzo) ya gari hilo?
3. Je, kunaondoa ukweli kuwa mtu huyo Mjapani atakuwa aliona "picha ya gari" (alivuviwa) hilo toka sehemu nyingine na ndio maana akaweza kutengeneza kama linavyoonekana?
3.Je chanzo cha uvuvio wa picha ya gari(namna gari linavyopaswa kuwa) unaweza kukithibitisha wewe au hata Mjapani mwenyewe?Je kushindwa kuthibitisha kunaondoa Essence yake?
Kwa hiyo tunaosema Mungu hayupo tunamaanisha nini?Tunataka au tulitegemea awepo wapi? Mlitaka exist kama Sold,Liquid or gas? Mnasema juu ya "WEMA na UOVU".Kama kuthibitisha ndio njia pekee ya kulifanya jambo liwepo je:
1.Tunaweza kuthibitisha kuwa ukweli au uovu una-exist? Je, tulicho nacho kama uthibitisho ni tabia za ukweli/uovu au Ukweli au Uovu?Je tukiona nguo unazovaa ndiyo tuhitimishe kuwa nguo hizo ndio wewe mwenyewe?
Gari si mfano mzuri. Kwa sababu gari lipo, tunalijua, tunaliendesha kila siku. Halina contradiction.
Mungu si kama gari. Gari linaonekana kwa macho.
Mungu ana contradiction.Ni kama pembetatu duara katika Euclidean geometry. Pembetatu haiwezi kuwa duara na duara haliwezi kuwa pembetatu.
Ukiona pembetatu ambayo ni duara wakati huo huo, njoo unioneshe haraka sana. Siku hiyo hiyo nitakubali mungu yupo.
Kwa nini?
Kuwepo kwa pembetatu ambalo I duara pia hapo hapo ni sawa sawa na kuwepo kwa mungu huyu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote.
Vyote viwili, pembetatu ambayo ni duara na mungu muweza yote, mjuzi wa yote na mwenye mapenzi yote ambaye kaumba ulimwengu huu wenye maovu, vina contradiction.
Pembetatu haiwezi kuwa duara, duara haiwezi kuwa pembetatu. Not in the framework of Euclidean geometry. Pembetatu duara ni contradiction.
Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, kwa nini kaumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana wakati alikuwa na uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani?
Mungu huyo kuumba ulimwengu kama huu ni contradiction.
Majibu mengi yametolewa.
Moja ni kwamba mungu alitaka tuwe na freewill.
Jibu hili linashindwa kujua au kukubali kwamba hatuna freewill anyway. Kwa mfano, hatuwezi kurudi nyuma katika muda.
Jibu linguine ni kwamba mungu alitaka dunia isiwe na maovu, lakini shetani ndiye chanzo cha maovu. Aliasi na kusababisha uovu.
Jibu hili linajibu swali tofauti na swali langu. Linajibu swali la "kwa nini kuna maovu duniani?" wakati mimi nauliza swali la "Kwa nini mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote kaumba ulimwengu ambao maovu yanaweza kutokea wakati aliweza kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani bila kupoteza lolote?".
Sijapata jibu la kueleweka la swali hili.