Kama mwanaume: Jitahidi mazingira yako ya nyumbani yawe bora kuliko mazingira ya nyumbani kwa mke wako

Mkuu ndio hapo sasa. Mke anakuwa alikubali kuolewa na wewe kwa sababu ya mapenzi japo hali yao kwao ni ya juu kuliko ya kwako. Sasa katika maisha yenu ya ndoa na watoto hizi changamoto haziepukiki. Fikiria unaenda nyumbani kwao unakuta shemeji zako wamekuja na Premio au IST zao, na baba yake amepaki Ford Ranger yake hapo nyumbani, wewe, mkeo na watoto mnaingia kwa basi. Mbona utaanza kukataa kwenda kwao kusalimia!
 
Kuna watu huwa wanatafuta sifa ukweni.
Mkuu, kujaribu ku-impress ukweni ni natural phenomenon, sio kutafuta sifa! Lazima uonyeshe kuwa nyumbani kwako mtoto wao kwako anabembea juu kwa juu tu!

By the way, halafu tukiwa ukweni tunamwonyesha mke mapenzi zaidi, touch touch na kiss za hewani nyiiiingi, mara umemchumia ua nk, kumbe mkirudi nyumbani kwako shubiri! Basi tu, kuwatia nyongo kaka zake kama wanagombana na wake zao!
 
Mi kwangu kama mke ni wangu kweli Kwa mpango wa Mungu, hili halina shida, mwanamke nikimpenda anasahau kama ana kwao au wazazi wake maana mimi naziba gape, ndiomana huwa sipendi hovyo walau siku hizi nafanya kumhitajia mwanamke tu kupenda nimepunguza
Hujaoa wewe!
 
Kumbe baba mkwe anakupiga tafu kiasi hicho sasa hapo tatizo liko wapi? Sio inategemea mwanamke, sema inategemea baba mkwe!

Huenda hata waliwapa mchuma Range Rover Vogue kama zawadi ya harusi na hizo nyumba na viwanja wamewapiga tafu pia!

Ndio maana nilisema, ikibidi, omba mkwe akupige tafu!
 
Theoretically you are right
 
kwakua cna hela labda,ila ukweni siwezi kujenga.
 
Duh
Duh! Mkuu wewe Mungu alikudondoshea zali la mentali aisee! Bila Shaka wewe Ni Mmoja Kati ya wanaume wachache wenye bahati.
 
Umeongea kinadharia sana, mtoa mada na mchangiaji wa kwanza wamezungumza mambo ‘practical’
 
Bora mi na mama chanja tuliokotana uko jalalani.......
Sie wetu dagaa nyama tamaa, life mdondo....
 
Umeongea kinadharia sana, mtoa mada na mchangiaji wa kwanza wamezungumza mambo ‘practical’

Hakuna cha unadharia, ni aidha una Dini na unaamini katika Mafundisho yake au hauna na hauamini, kuna watu wengi tu wanaamini na kufwata mafundisho ya kidini hupata mwenza wa aina yao, hivyo inategemea, na ndio maana kuna msemo Mke mwema hutoka kwa Mungu, maana yake ni kwamba ukitfuta na kuomba pia utapata unachokitaka, na ukitaka pia Mwanamke asiye na malezi ya kidini wala asiyefwata mafundisho yake utampata pia.

Maishani mwangu nimeshuhudia watu wenye furaha ya Maisha ni wale wenye familia bora inayofwata mafundisho ya kidini, na wapo wengi tu.

Put God First!
 
Sawa.
 
Mke mwema hutoka kwa Mungu, maana yake ni kwamba ukitfuta na kuomba pia utapata unachokitaka

Maishani mwangu nimeshuhudia watu wenye furaha ya Maisha ni wale wenye familia bora inayofwata mafundisho ya kidini, na wapo wengi tu.

Put God First!
Sawa, mtu anaetafuta na kuomba hekima ya Mungu ili kupata mke, ataepuka kuoa mke ambae anamwacha mbali sana katika level ya maisha maana busara ya Mungu itamwambia sio jambo la hekima kuoa katika familia ya namna hiyo iliyo katika uthamini wa fedha wakati wewe huna uwezo. Ni sawa na Solomon kuoa Wamoabi badala ya Waisrael. Mke wa namna hiyo wala sio Mungu amekuonyesha, ndio maana Jakobu alienda mbali sana ili kupata mke wa aina yake, mchunga ngamia kama yeye!

Sasa wewe oa katika familia ya matajiri useme umeomba Mungu amekuonyesha uone itakavyokula kwako!
 
Dem niliyemuoa alinikuta nikiwa "kapuku kapukutika" na kwa wazee nako hakueleweki. Kwao yeye aaah uongo ...mambo safi.

Alipotaka kuleta hizo za mtoa mada nilimhangaisha kisaikolojia hadi alichanganyikiwa akawa anakonda hovyo na nuru usoni ikapotea.

Wazazi wake waligundua kua binti yao kaolewa ila hajakubali maisha ya ufukara na bado kichwani anawaza "kwao". Siku moja nilimdunda kweli kweli binti akaamua kurudi huko kwao.....baba yake aliporudi na kumkuta nyumbani amepuzika na utosi umevimba akamuuliza binti akadai kapigwa na amerud kwao mume hamtaki tena.

Mzee alimtoa baru pale sebleni binti akafukuzwa arudi "kwake" kakimbilia kwa shangazi mtu nae akamtoa mkuku akaenda kulala lodge (ya baba yake). Kesho yake kapanda costa tena kwa kuomba maana nauli ilipungua buku 2 kaja moro kapiga magoti kesi ikaisha.

Baada ya wiki babaake kaja. Lake lilikua moja tu. Kasema hajaja kusuluhisha ugomvi kwasababu anaamini tulishayamaliza. Kilichomleta ni kumhakikishia binti kwamba pale kwetu kama baba yake alivokua mgeni ndivyo binti nae amekua mgeni akienda kwa baba yake.
 
Ndugu.una roho ngumu sana....bila shaka kutakuwa na vingi hujawekawazi pia.Unalipiwa ada ya watoto waziwazi na baba mkwe..then uko comfortable kabisa.....???Hauko serious wewe....pambana...hao watoto wapelekeni shule mnayoiweza......

Pambana aisee au kuwa na kiasi, ishi maisha yako na Mungu atakuinua kivyakovyako na familia yako..acha huo unyonge kabisa..hakuna adabu na furaha kwa mwanaume kusaidiwa majukumu yake tena na watu wa karibu kama baba mkwe..

KAMA mkeo kwao wanaukwasi na wanaeleweka...kaa chini..andika proposal yako...nenda kwa huyo mzee mfanye biashara..omba mkopo wa riba nafuu, chakarika....mrudishie amount yake, songa mbele..hapo utakuwa mwamba....hayo ya kusaidia yataaibisha hata watoto wako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…