Mkuu,una maoni gani kitalaam hapo kwenye kuoa au kuolewa na maskini?Ndoa ni kutafuta wa kufanana Naye.
Neno "mfano" Lina maana kubwa Sana na ndio ndoa yenyewe.
Huwezi olewa au oa mtu Tajiri alafu ukategemea uishi Kwa Furaha na Amani ilhali wewe ni kapuku au kwenu ni kapuku.
Hiyo haijawahi kutokea na kamwe haitotokea.
Mkuu i never took a penny kutoka kwa huyo mzee. Kwa kipindi chote amekua ankinishawishi nikamsaidie majukumu ktk moja ya shughuli zake nimekua nikimkatalia sababu i know consequencies.Ndugu.una roho ngumu sana....bila shaka kutakuwa na vingi hujawekawazi pia.Unalipiwa ada ya watoto waziwazi na baba mkwe..then uko comfortable kabisa.....???Hauko serious wewe....pambana...hao watoto wapelekeni shule mnayoiweza......
Pambana aisee au kuwa na kiasi, ishi maisha yako na Mungu atakuinua kivyakovyako na familia yako..acha huo unyonge kabisa..hakuna adabu na furaha kwa mwanaume kusaidiwa majukumu yake tena na watu wa karibu kama baba mkwe..
KAMA mkeo kwao wanaukwasi na wanaeleweka...kaa chini..andika proposal yako...nenda kwa huyo mzee mfanye biashara..omba mkopo wa riba nafuu, chakarika....mrudishie amount yake, songa mbele..hapo utakuwa mwamba....hayo ya kusaidia yataaibisha hata watoto wako
Mkuu,una maoni gani kitalaam hapo kwenye kuoa au kuolewa na maskini?
Sawamtaalamu,Mimi nitakata hiyo number 4.Inategemeana na Akili ya huyo muolewaji/muoaji.
Mimi vigezo vya kuoa ni Kama ifuatavyo
1. Upendo
2. Akili.
3. Tabia njema
4. Uzuri.
Pesa tutatafuta.
Ila hayo manne hapo juu huwezi kuyatafuta
Sawamtaalamu,Mimi nitakata hiyo number 4.
Mkuu mkweo wewe ni kama mkwe wangu mimi,nashukuru Mungu yule mzee hana tabu kabisa.Maoni yangu ktk hili swala kupitia ushuhuda wangu bjnafsi.
Mimi na mke wangu tulikutana chuoni miaka 11 iliyopita, mimi natokea familia ya kipato cha chini ila yeye kwao wanamaisha mazuri hasa, yaani unaweza sema familia yao yote wapo vyema kuanzia baba, baba wa dogo nk. Ni wafanyabiashara wa kubwa wa usafirishaji, real estate na sasa wameingia ktk mashule.
Binti alikubali nimuoe kwa mahari ya sawa na bure mpaka kwetu wakashangaa akaulizwa mara tatu tatu mwisho akaishia kuipunguza zaidi. Kwa ufupi alikubali nimuoe kwa hali yangu yoyote, tulianza maisha ktk chumba kimoja, tukahamia viwili na sasa tuna nyumba zetu 2 na viwanja kadhaa na tupo mid thirties.
Nalotaka kusema ni hivi, inategemea na mwanamke mwenyewe na hulka zake na familia yake, unaweza ukanyanyaswa kupita maelezo na pia unaweza kupewa confort kuliko unavyotegemea. La msingi kuwa mwanaume, sababu ushamuoa basi hakikisha unaishi kutokana na uwezo na mipango yako uwezo wake na familia yake usiwe sehemu ya maisha yenu.
Binafsi hupitia kipindi nafulia mpaka msosi ndani hakuna na watoto wanasimamishwa shule lakini napambana of which am sure akipiga simu kwa mzee wake just one call muamala wa kutosha tu unaingia.
Ninachoshukuru mzee wake ananipa sana ushauri wa maisha hasa ktk utafutaji na anapenda niwe karibu nae, may be kwa sababu ya prosperity ya mwanae na wajukuu zake.