Maoni yangu ktk hili swala kupitia ushuhuda wangu bjnafsi.
Mimi na mke wangu tulikutana chuoni miaka 11 iliyopita, mimi natokea familia ya kipato cha chini ila yeye kwao wanamaisha mazuri hasa, yaani unaweza sema familia yao yote wapo vyema kuanzia baba, baba wa dogo nk. Ni wafanyabiashara wa kubwa wa usafirishaji, real estate na sasa wameingia ktk mashule.
Binti alikubali nimuoe kwa mahari ya sawa na bure mpaka kwetu wakashangaa akaulizwa mara tatu tatu mwisho akaishia kuipunguza zaidi. Kwa ufupi alikubali nimuoe kwa hali yangu yoyote, tulianza maisha ktk chumba kimoja, tukahamia viwili na sasa tuna nyumba zetu 2 na viwanja kadhaa na tupo mid thirties.
Nalotaka kusema ni hivi, inategemea na mwanamke mwenyewe na hulka zake na familia yake, unaweza ukanyanyaswa kupita maelezo na pia unaweza kupewa confort kuliko unavyotegemea. La msingi kuwa mwanaume, sababu ushamuoa basi hakikisha unaishi kutokana na uwezo na mipango yako uwezo wake na familia yake usiwe sehemu ya maisha yenu.
Binafsi hupitia kipindi nafulia mpaka msosi ndani hakuna na watoto wanasimamishwa shule lakini napambana of which am sure akipiga simu kwa mzee wake just one call muamala wa kutosha tu unaingia.
Ninachoshukuru mzee wake ananipa sana ushauri wa maisha hasa ktk utafutaji na anapenda niwe karibu nae, may be kwa sababu ya prosperity ya mwanae na wajukuu zake.