Mkuu, haukosoma ujumbe wa niliyemQuote
Yeye alisema, jambo hili linalomhusu M/kiti wa Chadema lingetokea akamatwe katika kipindi cha JPM tena kwa suala hilihili la ugaidi, Ile lugha ya JPM anachukia Wachaga na ile dhana ya sukuma gang, chuki yake ingeongezeka mara elfu, na pengine kungelihitajika mtu wa kuzipatanisha hizi pande mbili,
Bahati mbaya yanatokea haya, JPM hayupo, na ndiyo maana nilitaka kusema,
Kwa Tanzania yetu mahali ilipo na kwa misingi bora iliyowekwa, sisi hatuna ukabila, na ukiona kuna kelele za ukabila, chunguza, na ukichunguza kwa umakini ndio utaweza kuona kama haya ya tuhuma za Mbowe
Kwa wenye kujisemea, mtu anaweza kusema..! kumbe ile chuki iliyokuwa ikifukuta chinichini ya Sukuma gang kuchukiana na Watanzania wenzao Wachaga, kulikuwa na namna iliyokuwa inaundwa kitaalamu, kwamba ikitokea Mbowe amedakwa kwa tuhuma hizo, iwe ni suala la mtu kuamini moja kwa moja kuwa, Msukuma JPM anachuki na wachaga,
Sasa yanatokea haya JPM msukuma hayupo,
Tuacheni sasa siasa zisiwe zinatuchonganisha, na kila mwenye kutenda kosa, awajibishwe kisawasawa na mtu mwingine yeyote na kusiwepo kusema sijui kwa sababu ya kabla lake, hapana!