Kama Mwenyekiti wa Chama atajihusisha na Ugaidi na chama hakifutwi, kosa gani linaweza kusababisha chama kufutwa?

Kama Mwenyekiti wa Chama atajihusisha na Ugaidi na chama hakifutwi, kosa gani linaweza kusababisha chama kufutwa?

Mkuu, haukosoma ujumbe wa niliyemQuote

Yeye alisema, jambo hili linalomhusu M/kiti wa Chadema lingetokea akamatwe katika kipindi cha JPM tena kwa suala hilihili la ugaidi, Ile lugha ya JPM anachukia Wachaga na ile dhana ya sukuma gang, chuki yake ingeongezeka mara elfu, na pengine kungelihitajika mtu wa kuzipatanisha hizi pande mbili,

Bahati mbaya yanatokea haya, JPM hayupo, na ndiyo maana nilitaka kusema,

Kwa Tanzania yetu mahali ilipo na kwa misingi bora iliyowekwa, sisi hatuna ukabila, na ukiona kuna kelele za ukabila, chunguza, na ukichunguza kwa umakini ndio utaweza kuona kama haya ya tuhuma za Mbowe

Kwa wenye kujisemea, mtu anaweza kusema..! kumbe ile chuki iliyokuwa ikifukuta chinichini ya Sukuma gang kuchukiana na Watanzania wenzao Wachaga, kulikuwa na namna iliyokuwa inaundwa kitaalamu, kwamba ikitokea Mbowe amedakwa kwa tuhuma hizo, iwe ni suala la mtu kuamini moja kwa moja kuwa, Msukuma JPM anachuki na wachaga,

Sasa yanatokea haya JPM msukuma hayupo,

Tuacheni sasa siasa zisiwe zinatuchonganisha, na kila mwenye kutenda kosa, awajibishwe kisawasawa na mtu mwingine yeyote na kusiwepo kusema sijui kwa sababu ya kabla lake, hapana!
Mbowe kaponzwa na kufukuza wale wa dada, walikuwa wanatembea na siri za chadema.Chezea kina Delila, muulize I Somson
 
Kwanza naomba nieleweke kwamba, Huu uzi hauongelei chama chochote, isipokuwa unaangazia makosa ambayo yakifanyika ndani ya chama chochote, na nani ndani ya chama endapo atafanya makosa yanayopita uwezo wa kustiliwa hadi kupelekea kufutwa kwa Chama,

Kama M/kiti wa chama husika, anajihusisha na mambo ya kigaidi na bado chama hakuwezi kufutwa, Je, ni kosa lipi lingine ambalo linaweza kupelekea chama cha siasa kufutwa?

Kama kosa doogo kabisa la mgombea Urais kuanza kampeni kabla ya kipyenga rasimi kupulizwa, anaweza kuondolewa kwenye nafasi ya ugombea Uraisi au kuadhibiwa vikali.

Je, Ili chama kifutwe, ni makosa gani ambayo yakitendeka ndani ya chama, yanayompa nafasi Msajili wa vyama kukifuta chama hiko kupitia sheria na kanuni za usajili nchini!

Karibuni wadau na wajuzi wa mambo ili hata likitokea, wote tunakuwa tunafahamu
Huyo ni Mbowe bhana! Kiongozi wa chama kwani umeambiwa CDM inashabikia ugaidi? Yaani baba wa familia ukiwa jambazi ukafungwa, familia nzima ifungwe?
 
Wanaouliza kwa nini Mbowe amekamatwa sasa na si vinginevyo wanasahau kuwa Mbowe, Lema, Meya wa zamani Ubungo Boniface walikamatwa mara baada ya matokeo ya uchaguzi mkuu kutangazwa na kabla Rais hajaapishwa kwa kuchochea maandamano yasiyo na kikomo kupinga matokeo. Mambosasa alihojiwa na vituo vya ITV na TBC na kutoa madai hayo hayo ya ugaidi.
 
Back
Top Bottom