Akiwa waziri wa Mambo ya Ndani wakati wa uraisi wa Magufuli, nilidhani Mwigulu ni mtu makini mwenye msimamo sana, msomi wa degree ya first class ya economics, masters na PhD.
Mara tu baada ya Tundu Lissu kupigwa risasi, Magufuli alimwamuru Mwigulu atoe tamko kwamba serikali haihusiki na jaribio la kumuua Lissu. Mwigulu alikataa na Magufuli akamkasirikia sana.
Lakini sasa sijui kawa mtu wa namna gani. Anaongea vitu vya ajabu sana. Mtu mwenye PhD na first class degree ya uchumi unawezaje kuongea kwa kujidhalilisha hivyo ili tu kumfurahisha mtu wa form four na certificate ya siasa za jamii? Kwa nini usikae kimya ukajikita kwenye kuongelea mambo ya msingi? Wewe ni Waziri Mkuu. Ujinga wa kipropaganda waachie makatibu wenezi na wengine kama wao. Acha kupayuka kama vuvuzela mikononi mwa mtu asie na akili sawasawa. Haikusaidii kisiasa, inakumaliza.