Kama mzaha hoja ya Mbunge Shabibi inaweza kutungiwa Sheria kuongeza maumivu kwa wananchi

Kukatwa buku 2 haina shida mkuu tatizo hizo hela zinaenda kweli kufanya lililokusudiwa? Ama kuna wacenge wachache fedha zikifika hazina watagawana billion 60/60 za michango na kwenda kujenga maghorofa mbweni na kununulia mabasi na malori?
Hapa umenena maana check tu mfano WA hili la NHIF malalamiko ya private sector ni ucheleweshaji wa malipo.
So tutumie mbinu gani wenzetu wasife kwa kukosa matibabu maana mbongo nae mgumu kuchanga we check kwa mfano kanisa katoliki lina bima unalipa kidogo kwa mwanachama lakini still muitikio ni mdogo.Ila visivyo na tija tupo mbele
 
Basi Bora kampuni za simu zifanye hivyo kwa kila mmiliki wa laini Yao ya simu tuungwe kwa lazima,hiii ya shabiby tunaenda nufaisha mafisadi.
Maana wazo ni zuri shida ni accountability,pana watu wanawaza kuongeza mabus na malori TU
 
Tupeni mbadala,yale ni mawazo yake ya hesabu na zile ni data zake,elfu 2000 kwa mwezi na nchi nzimabtutibiwe bure we inakuuma.
Utibiwe bure wapi, waongo hao itaenda kwenye matumbo yao, kwani wanaposema umeme vijijini nguzo sh 27,000 ni kweli? kama hauna laki 5 na kuendelea haujafunga umeme.
 
Wabongo kwa ulalamishi nini elf 2 kuokoa milioni 2 za matibabu
Tatizo sio 2000 bali ni pale mtu anaugua lkn unaambiwa bima haitoshi, mfanyakazi anakatwa hela kila mwezi na kwa muda wa miaka 10 lkn anaugua ugonjwa unataka 3mln ili apone anaambiwa bima haitoshi, swali ni je wale wote wanaokatwa bima huugua? Kama sio je pesa yao uenda wapi?
 
Tutumie njia gani kuukataa mkuu? Wanaopaswa kutusaidia wanasema wao wanalinda katiba (wanalinda majizi).

Njia moja ya kuwakataa hawa heartless jambazis kwa mfano ni kumpiga chini huyu Shabiby uchaguzi ujao. Tuwe serious na mambo yanayohusu uhai wetu Watanzania, tuamke!

Na pia tuache kuitukuza serikali kwenye kila nyanja ya maisha yetu. Siku Kuu ya Pasaka inaweza kunoga bila kumwita Majaliwa akae kiti cha mbele. Na siku tukifa tunaweza kusalishana wenyewe bila kumuita Mkuu wa Mkoa "kuongoza mazishi." Wana serikali wameshajua tunawatukuza kama miungu mtu, wanafanya lolote, tukatae hizi mentality za kijima hizi.

Na hiyo bima ikija tudai iseme ni marufuku serikali kumtibu mtu kwa cash nje ya mfumo wa bima, iwe ndani au nje ya nchi. Hata Joe Biden akiugua anatumia BIMA, serikali ya USA haitoi cash kumtibu rais, iwe ndani au nje ya Marekani, its just impossibly expensive. Hakuna mtu, au bilionea, kampuni, serikali, duniani inatibu watu kwa cash, except here in the meat-headed third world!
 
Wa-Tanzania Mutaisoma namba mpaka mtajuta kuzaliwa Tanzania pasipo na kupinga mutaonewa kila siku na Serikali ya SISI EMU OYEEE .Kidumu Chama Cha Mapinduizi Zidumu Fikra mbovu za Wabunge wa CCM.
 
Wame mismanage michango ya watu mpaka Hali imefika hapa. Tena michango iongezwe Tena wakatapanye!!
 
Hawa wabunge wa awamu hii waondolewe wote, tubadili katiba wabunge wataje viwango vya mishahara wanavyotaka kulipwa wanapoomba kazi majukwaani ili tuachane na hawa wakujitajirisha, kuna vijana wengi tu wapo tayari kuwa wabunge kwa malipo ya mil 5, ifike wakati tuwe na wabunge wenye akili

Kwa akili zake anadhani kila raia ana simu? Kila raia anaweka salio kwenye simu? Hajui wafanyakazi wanakatwa bima mshaharani?
 
Moja ya kosa kubwa alilofanya Mwalimu na baadae likaongezewa nguvu zaidi na The Late Magu ni kutufanya tuwe waoga!System imejipenyeza kila idara na kwa bahati mbaya inatumika kwa manufaa yao,its sad.Mahakama ipo kama paper tiger,huku chini mwananchi huwez kuanzisha vuguvugu hata la kuwataka wabunge waisimamie Serikali ukijaribu wew na wenzio kutembea na mabango kuelekea pale bungeni ujue your days are numbered!What a country🤣
 
 
Na inawezekana ikapita kabisa!
Cha kusikitisha hawaongelei maelekezo ya CAG kuhusu ubadhirifu wa fedha za umma na kubana matumizi yasiyo ya lazma!
Hata makisio ya Shabiby ya kukusanya trillion 2 bado zitapigwa tu,koz hamna uwajibikaji serikalini!
 
Asipougua yeye ataugua ndugu yake
 
YESU NA MARIA!!!!!!!!!Kwa hiyo nikatwe hela yangu ili niwachangie wahuni wavuta bangi,walevi ,wazinzi,wafiraji kisa tu wapate bima kwa wote? huu sasa ni ujinga uliyopitiliza.navunja laini zote
 
Kwa upande wangu hoja Yake sio mbaya ikiwa kweli itaenda kufanyiwa kazi inavyopaswa
Hii ni sawa na tunavyokatwa kodi ya majengo kwenye umeme na si lazima.iwe kwenye simu
Inaweza kuwa hata kwenye petroli
Inaweza kuwa hata kwenye kitambulisho cha taifa ikaja sheria kwamba kila Aliyefikisha miaka kumina minane awe nakitambulisho cha taifa na atakilipia elfu 15 au ishirini kwa mwaka na kitambulisho hicho kitamuwezesha kupata bima ya Afya

Shida iko wapi shida ni pale utakapolipia elfu mbili yako kwenye simu kisha huduma hakuna lakini ikiwa utalipia na huduma unapata miki sina pingamizi watu wanateseka sana huko hospitalini inahitajika njia ya kuwapa uhakika wa matibabu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…