Kama mzazi, binti yako ndio amekuja kukuambia kuwa amepata mchumba, ni swali gani la kwanza utamuuliza binti yako?

Karibu mzazi wa mwanamali na mzazi wa mwanamali mtarajiwa.
Je, unamfahamu vizuri mchumba wako yaani mumeo au mkeo mtarajiwa ni mtu wa aina gani? akueleze strenght and weakness za mwenza wake. Kisha maswali mengine yatafuta hapo kwenye S-W zake ili kuhakikisha kama anaweza kuishi nae kwa kuzitatua au kuwa mvumilivu.
2. Mchumba wako amekuzwa katika mazingira yapi? Baba, Mama au single parent? kwenye dini ipi?
3. Anajishughulisha na nini?
4. Je, unafahamu strenght na weakness zako wewe mwenyewe? utazishughulikiaje?
 
Namba 3. Huwa inajibiwaje au inapimwaje sorry
Nafikiri baba anataka kujua kama boyfriend wa mwanae ana kiwango gani maadili katika jamii.

So binti yeye anapaswa kujibu namna gani tabia, mwenendo wa boyfriend wake kama una tiki box la maadili mema ambayo jamii inayomzunguka inakuwa affected positively na jinsi alivyo.
 
Genious mshua wako.
 
She loves me and i love her , smart upstairs, figure 8 ,she is humble and have respect , age 23
How many say this about herπŸ˜΅β€πŸ’«πŸ˜΅β€πŸ’«πŸ˜΅β€πŸ’«πŸ˜΅β€πŸ’«
 
1. Anaitwa nani majina yake yote matatu.
2. Anatokea wapi
3. Baba yake ni nani na familia yake ni ya akina nani.
4. Baba yake anajishughulisha na jambo gani au shughuli zake za kiuchumi.
5. Kwao wapo watoto wangapi na yeye ni mtoto wa ngapi.
6. Mlikutana wapi na lini
7. Umefanya nae chochote hadi sasa kimwili
8. Amekupa mipango gani kuhusu maisha yake binafsi yaani kalenga kujishughulisha na jambo gani maishani na wewe unaingia kama nani katika hayo maisha yake.
9. Umekwenda kwao,mara ngapi
10. Nani anakufahamu kwao au nani wa upande wa kwao mnamawasiliano ya karibu.
11. Nani ambaye kati yenu alimfuata mwenzake na ni nani hadi sasa anaendelea kushawishi huu uhusiano uwepo
12. Wewe kama binti ambaye unakaribia kuingia mahusiano ya kudumu unaingia kimahusiano na huyu kijana kwa malengo gani
13. Unayafahamu majukumu anayokuitia mkafanye nayo mahusiano au unakwenda kuyajulia mbele ya safari
14. MUNGU ana nafasi gani katika uhusiano wenu
15. Mpo tayari kufuata maagizo ya MUNGU katika uhusiano wenu
16. Unakwenda kuanza mahusiano na huyu kijana mlishakaa na kupanga mnakwenda kuanza mahusiano ya namna gani
17. Umepima afya yako na yake
18. Unazifahamu changamoto za huyu kijana na tabia zake ambazo zinaweza kinzana na wewe yaani madhaifu yake kama mwanadamu
 
Nimependa maswali sita ya mwanzo!
 
Japo kwa maswali haya nadhani baba mkwe mtarajiwa atakuwa Muhaya tena mziba !
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…