Eneo la malezi kwa watoto ni pana sana chief,hapo unaweza kuta mzazi hajui kama mtoto hayupo nyumbani.
Karne hii watoto wanajua kila kitu kinachoendelea duniani, kwahiyo mzazi ukishindwa namna ya kumzibiti mtoto matokeo ndio kama haya. Anakwambia yupo tayari kwenda na msanii popote,ina maana anayajua mengi. Lakini pia kama vile wazazi tunaona haina haja tena kuwafuatilia watoto na kuwajenga katika misingi bora,tukiwapeleka shule tunadhani imetosha.
Turudi enzi zetu,nadhani mnakumbuka malezi tuliopewa,namna tulivyoonywa,tukazane mapema kuokoa hiki kizazi maana tukishindwa kuwalea vizuri matokeo yatakuwa mabaya zaidi.
Tusinyoosheane vidole,unaweza kumsaidia mwingine fanya,kama wao hawatathamini MUNGU anathamini mchango wako