GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 7,645
- 10,867
Simlaumu, ila nahisi amechangia pakubwa mtatiziko wa kisiasa uliopo nchini kwa sasa. CHADEMA wameamua kususia uchaguzi kwa sababu ya mapungufu yaliyopo kwenye mfumo mzima wa uchaguzi.
Inaaminika kuwa Katiba ya Wananchi ingeweza kutibu mtatiziko huo. Kwa bahati mbaya, ingawa mzee Kikwete aliuanzisha mchakato wa Katiba mpya, hakuweza kuukamilisha. Maslahi ya Wananchi na ya Chama chake yalikinzana.
Mzee Warioba alikuwa radhi kuwapa Wananchi walichohitaji. Lakini kwa kuwa Mzee Kikwete hakukubali kukisaliti Chama chake, alilitupilia mbali suala hilo.
Na tokea kipindi hicho mpaka sasa, Wananchi hawajaacha kuidai Katiba yao.
Laiti mzee Kikwete angeuvaa ujasiri wake wa kijeshi kipindi hicho na kuwapa Wananchi haki yao stahiki...!