Kama mzee Makamba alirekebishwa kauli, kwanini kauli nzito ya Zitto dhidi ya TISS imebarikiwa?

Kama mzee Makamba alirekebishwa kauli, kwanini kauli nzito ya Zitto dhidi ya TISS imebarikiwa?

Msanii

Platinum Member
Joined
Jul 4, 2007
Posts
25,252
Reaction score
36,513
Jana katika ibada ya kumuaga mpendwa wetu Bernard Kamilius Membe pale Karimjee, watu mbakimbali walipata fursa ya kutoa maneno ya rambirambi kwa familia na jamaa wa Marehemu Membe.

Kiongozi wa ACT Wazalendo alipata fursa ya kutoa rambirambi zake. Lakini ndani ya content aliyoisoma pale aliituhumu idara kuhusika nankuruhusu rasilimali zake kutumika kumchafua Membe na watu wengine.

Kauli hii, inazua sintofahamu ya ujasiri na kusudio la Zitto dhidi ya TISS. Ikumbukwe kwamba kuidhalilisha hadharani TISS ni kuidhalilisha nchi. Na bahati mbaya hawa jamaa huwa hawana msemaji wa kujibu hoja za kisiasa wanazotuhumiwa nao.

Mzee Makamba alimnanga Magufuli kwa kusema Wazuri hawafi mapema na aliposimama Capo akamrekebisha kuwa mzee aliteleza ulimi. Lakini jana mbele ya CIC zimetolewa tuhuma nzito dhidi ya taasisi nyeti nchini na hakuna kanusho wala rekebisho dhidi ya udhalilishaji huo.

Mtu kama Zitto siyo asset wa kuaminiwa kwenye nafasi yeyote nchini kwa sababu anaonesha wazi hana mahaba na Nchi yetu
 
Jana katika ibada ya kumuaga mpendwa wetu Bernard Kamilius Membe pale Karimjee, watu mbakimbali walipata fursa ya kutoa maneno ya rambirambi kwa familia na jamaa wa Marehemu Membe...
Kauli ya ZZK ni DIRA yetu, inabeba maudhui mazito sana kwa Taifa letu kwenye kipindi hiki, kwa hiyo haiwezi okabadilishwa.

Magufuli alikuwa kama Nebuchadnezzar wa kwenye Biblia, ALINAJISI vitendea kazi vya Ikulu kwa kuvutumia HOVYO. Kutofuata Katiba, kuliendesha Bunge lwa remote na kuotishia Mahakama ni vitendo viovu sana katika historia ya nchi yetu. Namna alivyoitumia TISS kwa ajili ya masilahi yake binafsi na kuunda kikundi haramu cha WASIOJULIKANA lazima kikemewe kisijejirudia tena kwenye nchi yetu.

Nashauri ZZK aongeze kupaza sauti ili hata watanzania wajinga wapatao 89%ya population waelewe kuwa Magu hakuwa mtu sahihi kutawala nchi yetu
 
Tiss ndio takataka gani,kualibu pesa za walipa Kodi,hakuna shida Katiba yenyewe imeweka watu chini ya ulinzi hakuna maana yoyote kupoteza pesa.
 
Tiss ndio takataka gani,kualibu pesa za walipa Kodi,hakuna shida Katiba yenyewe imeweka watu chini ya ulinzi hakuna maana yoyote kupoteza pesa.
TISS ni takataka inayokuwezesha wewe kupata usingizi na kuamka salama na kwenda kijiweni kupiga soga bila kuporwa wala tishio la usalama.

Ni taasisi yetu lazima tuienzi na kuisitiri sambamba na kuiboresha penye mapungufu
 
Kauli ya ZZK ni DIRA yetu, inabeba maudhui mazito sana kwa Taifa letu kwenye kipindi hiki, kwa hiyo haiwezi okabadilishwa...
Kuna Professor moja wa afya alikuwa anajisifu sana kwamba watu wenye akili kama sisi hatufi haraka,bahati mbaya sana kumbe wanafunzi walikuwa wanamuona kama punguani flani tu.
 
Hata usoni anaonesha wazi kuwa anakerwa na utulivu na amani yetu.
Sijawahi kumuamini hata chembe na utaona anapambania zaidi maslahi ya wanaomtumia.
 
Ilitakiwa MC ajitolee aseme tu, jamani tumsamehe bwana Zitto uzee unamnyemelea na stress za kukosa mambo mazito.
 
Back
Top Bottom