Kama Na Wewe Ni Mzalendo Halisi, Hebu Tujadili Hili Kwa Pamoja Na Tuishauri Serikali

Kama Na Wewe Ni Mzalendo Halisi, Hebu Tujadili Hili Kwa Pamoja Na Tuishauri Serikali

Dialogist

JF-Expert Member
Joined
Apr 14, 2014
Posts
1,167
Reaction score
1,872
Wanabodi, Salaam..

Nimewiwa kuja na bandiko hili usiku wa leo kutokana na changamoto nilizokutana nazo barabarani.

Kila mtu anafahamu kwa sasa nchi yetu imepiga hatua kwa namna fulani katika kukaribisha uwekezaji wa nje (foreign investment) ukilinganisha na miaka kadhaa nyuma. Lakini kwa ufuatiliaji wa karibu hawa wawekezaji wote au kwa wingi wao hakuna mwenye nia ya dhati ya kuisaidia Tanzania, kila anayekuja nia ni kuchuma fedha na kupeleka kwenye nchi zao na kujikuta hakuna faida kubwa tunayobaki nayo hapa.

Mfano, ni majengo machache sana Tanzania yanayomilikiwa na wageni iwe kwa kujenga au kununua, wengi wamekodi kwa muda mfupi ili miradi yao ikiisha waondoke na mabegi na pesa au rasilimali lakini waache fixed assets kama walivyozikuta. Majengo mengi yaliyopo hapa nchini ni ama yamejengwa na serikali na taasisi zake, au na watanzania binafsi au PPP kama anavyofanya TOSHI CARGO Kariakoo.

Hata ukiwafatilia wachina ambao ndio wengi na wajanja wajanja tu, kwenye viwanda vyao hawana majengo ya kudumu, ni mabox box au mabati vitu ambavyo ni movable. So tangible benefits kutoka kwao ni ngumu kuonekana.

Katika muktadha huo, hamuoni kuna umuhimu sasa wa serikali hata kama itapunguza kodi au namna gani, iwape upendeleo wazawa kuendesha baadhi ya miradi ili pesa ibaki nchini???

Kutokana na tetesi ninazosikia, (zisizo na uthibitisho ila mwishoni itajulikana tu) kuna sababu gani ya kuwapa wageni kuendesha mwendokasi wakati ABOOD yupo, SHABIBY yupo, ABC/ABS yupo? Kuna umuhimu gani wa serikali kuendelea kuendesha feri ya Kigamboni pamoja na kufeli kwake, wakati BAKHRESA yupo? Kuna siri gani hapo?? Au ndio kweli ni mambo ya 10% yanayotufelisha watanzania??

Haya mambo yanaturudisha sana nyuma sisi wenyewe katika maendeleo ya kudumu ya mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.
 
Back
Top Bottom