Kama nchi tumefeli kwenye Ufunguzi wa African Football League

Caf wanamjua ali kiba?
Kwa nn ile nafasi ya alikiba kutumbuiza wasingewapa team za academy
Hakuna ufunguzi niliowahi kuona hizo content unazosemea, Ila ni wazo nzuri sana hapo Kwa alikiba Pana ukakasi inawezekana viongozi wa Simba walipewa nafasi ya kupendekeza jina la mtumbuizaji wao wakaona kiba anafaa
 
Kudhamini mechi kinahitaji hela ndefu. Visit Rwanda inayoonekana kwenye jezi ya Arsenal kagame anatoa £10m kwa mwaka Sawa na hela ya Samia Tzs 30b/=
 
Habari za wakati huu wakuu,

Jana ilikuwa siku muhimu sana katika Historia ya Soka la Tanzania na Africa kwa ujumla baada ya Ufunguzi wa African Football League katika Uwanja wa Benjamin william Mkapa mechi ambayo iliisha kwa sare ya goli mbili.

Wadhamini wakubwa wa mashindano haya ni Saudia na Rwanda, ambapo wakati mechi inaendelea maneno kama Visit Rwanda na Visit Saudia yalionekana, ambayo kiuhalisia hiyo nafasi ilitakiwa iwe yetu.

Inamaana kuanzia zanzibar na Tanzania bara hawakuona umuhimu wa kutafuta kitu cha kututangaza kama nchi mpaka Rwanda na Saudia wanachangamkia fursa sisi tupo tumelala usingizi wa pono! Hapo kama nchi tumefeli.

Kwa tukio la jana ambalo watu maarufu na viongozi mbalimbali wa mpira Duniani walikuwa uwanjani akiwemo Rais wa FIFA na aliyekuwa Kocha wa zamani wa Arsenal, Mzee Arsene Wenger ilikuwa fursa adhimu ya kuonyesha vipaji mbalimbali tulivyonavyo katika nchi yetu.

Hivyo nilitegemea wachezaji wa Timu ya Wanawake ya Simba na wachezaji vijana wa Simba kucheza mechi za ufunguzi kabla ya mechi rasmi, kwasababu jana kulikuwa na football agents kutoka sehemu mbalimbali duniani.

Kweli mtu amuangalie Kibu Denis na Saido Ntibazonkiza hata kama ni wachezaji wazuri atawapeleka wapi kwa umri wao? Kosa kama hilo tulifanya walivyokuja Sevilla kutoka Spain, walisema wachezaji wa Simba ni wazuri ila umri ndio ilikuwa tatizo.

Wenzetu hutumia fursa kama hizi kama njia ya kuonyesha vipaji walivyonavyo na kuonyesha uwezo wa wachezaji wadogo kama njia na fursa ya kusakata kabumbu nje ya Bara la Afrika na Tanzania kiujumla, ila na hapo pia tumefeli kama nchi na kama club.

Simba kwa kushirikiana na serikali walitakiwa waingie makubaluano katika mashindano haya makubwa kwa ngazi ya vilabu Barani Africa, nilishangaa kuona M-Bet badala ya Visit Tanzanka kwenye kifua wakati mkataba wa M-Bet ulikuwa ni CAF Champions League kwa Level za Kimataifa na Mashindano yote ya ndani, nilishangaa kuona na hili pia linatupita kama nchi tumefeli kwenye hili tena.

Kuteleza si kuanguka, ila wakati mwingine tutumie haya mashindano kibiashara zaidi kuliko kuangulia tu matokea. Bado hatujachelewa, tujipange tena kwenye Maandalizi ya AFCON, tusichezee fursa wakati zipo mlangoni mpaka majirani wanazichangamkia.

Tatizo tunaangalia kila kitu kisiasa na kiushabiki, ndio maana kila siku tunakumbuka shuka kumekucha! Tuamke wazee, Dunia ya 1980 sio ya leo 2023, next time tujipange.

Alamsik.
Yale mashindano yapo chini ya CAF sio Tanzania. Wadhamini wana-submit ofa zao mwenye kisu kikali ndie atakaekula nyama.
 
Visit Tanzania alitakiwa kuweka bid nayeye, zile ni hela zimewekwa pale,
 
No vijana wangecheza hata vijana wenzao kwa mfano wangecheza fountain gates academy na simba ila vijana na wanawake kabla ya mechi husika that's was my point mkuu.
Ili iweje sasa, hii ni kitu mpya
 
Hapana sidhani kama mkataba wa team husika unaingiliana na wadhamini wakuu ndio maana bakhresa anatangaza mo energy licha ya kuwa mpinzani wake kwenye AZAM energy.
Bro unakumbuka case ya Yanga mwaka Jana ya sport pesa sijui na 1bet kule Confederation Cup Mkuu? Poa hata Simba ya Mbet na hiyo kampuni iliyodhamino Champion Leagu ya mwaka jana? Nilichukulia nadharia ile nikairelate na game ya jana ya Simba na Visit Tanzania Mkuu.
 
Habari za wakati huu wakuu,

Jana ilikuwa siku muhimu sana katika Historia ya Soka la Tanzania na Africa kwa ujumla baada ya Ufunguzi wa African Football League katika Uwanja wa Benjamin william Mkapa mechi ambayo iliisha kwa sare ya goli mbili.

Wadhamini wakubwa wa mashindano haya ni Saudia na Rwanda, ambapo wakati mechi inaendelea maneno kama Visit Rwanda na Visit Saudia yalionekana, ambayo kiuhalisia hiyo nafasi ilitakiwa iwe yetu.

Inamaana kuanzia zanzibar na Tanzania bara hawakuona umuhimu wa kutafuta kitu cha kututangaza kama nchi mpaka Rwanda na Saudia wanachangamkia fursa sisi tupo tumelala usingizi wa pono! Hapo kama nchi tumefeli.

Kwa tukio la jana ambalo watu maarufu na viongozi mbalimbali wa mpira Duniani walikuwa uwanjani akiwemo Rais wa FIFA na aliyekuwa Kocha wa zamani wa Arsenal, Mzee Arsene Wenger ilikuwa fursa adhimu ya kuonyesha vipaji mbalimbali tulivyonavyo katika nchi yetu.

Hivyo nilitegemea wachezaji wa Timu ya Wanawake ya Simba na wachezaji vijana wa Simba kucheza mechi za ufunguzi kabla ya mechi rasmi, kwasababu jana kulikuwa na football agents kutoka sehemu mbalimbali duniani.

Kweli mtu amuangalie Kibu Denis na Saido Ntibazonkiza hata kama ni wachezaji wazuri atawapeleka wapi kwa umri wao? Kosa kama hilo tulifanya walivyokuja Sevilla kutoka Spain, walisema wachezaji wa Simba ni wazuri ila umri ndio ilikuwa tatizo.

Wenzetu hutumia fursa kama hizi kama njia ya kuonyesha vipaji walivyonavyo na kuonyesha uwezo wa wachezaji wadogo kama njia na fursa ya kusakata kabumbu nje ya Bara la Afrika na Tanzania kiujumla, ila na hapo pia tumefeli kama nchi na kama club.

Simba kwa kushirikiana na serikali walitakiwa waingie makubaluano katika mashindano haya makubwa kwa ngazi ya vilabu Barani Africa, nilishangaa kuona M-Bet badala ya Visit Tanzanka kwenye kifua wakati mkataba wa M-Bet ulikuwa ni CAF Champions League kwa Level za Kimataifa na Mashindano yote ya ndani, nilishangaa kuona na hili pia linatupita kama nchi tumefeli kwenye hili tena.

Kuteleza si kuanguka, ila wakati mwingine tutumie haya mashindano kibiashara zaidi kuliko kuangulia tu matokea. Bado hatujachelewa, tujipange tena kwenye Maandalizi ya AFCON, tusichezee fursa wakati zipo mlangoni mpaka majirani wanazichangamkia.

Tatizo tunaangalia kila kitu kisiasa na kiushabiki, ndio maana kila siku tunakumbuka shuka kumekucha! Tuamke wazee, Dunia ya 1980 sio ya leo 2023, next time tujipange.

Alamsik.
Umepuyanga. Usiniulize kwanini. Wataeleza wengine.
 
Yes hili ni kweli kabisa Mimi iliniudhi sana mpka kwenye information zone pale Red carpet pia Visit Rwanda kwani hakukuwa na Tanzania...
Ni muhimu saa kuangalia Mikataba tunayoungia isije ikatufnya kuwa watumwa kama Jana
Watu mnachekesha sana Simba anahusikaje pale kwenye uo unauita mkataba ? Mashindano ni ya CAF na FIFA wao ndio waamuzi na wasimamizi ,ulitakiwa kusema sisi kama nchi ilipaswa tuzamini mashindano haya ili kutangaza utalii wetu ..
 
Kudhamini mechi kinahitaji hela ndefu. Visit Rwanda inayoonekana kwenye jezi ya Arsenal kagame anatoa £10m kwa mwaka Sawa na hela ya Samia Tzs 30b/=
Alaf Rwanda ni kama kamkoa kamoj tu ka TZ ama kama sio wilaya moja aseee
 
Umepuyanga. Usiniulize kwanini. Wataeleza wengine.
Umenikumbusha mbali mkuu [emoji1787][emoji1787] kama job ndugai anadai aliambiwa na mzee malecela ajiuzulu na asiulize kwa nini na akafanya kama alivyoambiwa kipindi kile watu wanamuandama.
 
Bro unakumbuka case ya Yanga mwaka Jana ya sport pesa sijui na 1bet kule Confederation Cup Mkuu? Poa hata Simba ya Mbet na hiyo kampuni iliyodhamino Champion Leagu ya mwaka jana? Nilichukulia nadharia ile nikairelate na game ya jana ya Simba na Visit Tanzania Mkuu.
Hapana mkuu its totally difference unaweza ukashangaa raisi wa FIFA na arsene Wenger hakupata hata proposals kutoka kwa watanzania zaidi ya kuomba picha mtu kama yule anatakiwa aondoke na document nyingi alizopewa na watanzania on how to develop African football ili watupe support ila kila mtu kaomba picha tu.
 
Hakuna ufunguzi niliowahi kuona hizo content unazosemea, Ila ni wazo nzuri sana hapo Kwa alikiba Pana ukakasi inawezekana viongozi wa Simba walipewa nafasi ya kupendekeza jina la mtumbuizaji wao wakaona kiba anafaa
Ni kweli mkuu ila nazungumzia hali yetu ya mpira ilivyo kwa sasa na aina ya watu waliokuja hilo lingewezekana kufanyika
 
Hapana mkuu its totally difference unaweza ukashangaa raisi wa FIFA na arsene Wenger hakupata hata proposals kutoka kwa watanzania zaidi ya kuomba picha mtu kama yule anatakiwa aondoke na document nyingi alizopewa na watanzania on how to develop African football ili watupe support ila kila mtu kaomba picha tu.
Kongole kwako umeongea kitu kikubwa sana mkuu.
 
Back
Top Bottom