B51
JF-Expert Member
- Jan 1, 2019
- 582
- 798
Kutumia Agent ipo kimataifa sio tu Tanzania, hili ni sawa coz kuna taratibu za kiforodha lazima zifuatwe.Habari,
Ninaandika huu uzi nikiwa na masikitiko makubwa mno yanayozidi kiasi; natamani kuukana uzalendo kabisa
Nilienda kupokea mzigo wangu pale airport kg 63 personal effect ambao ulichukua siku nne mpaka kuutoa pale ndani
Kwa ufupi airport cargo kuna mapungufu makubwa mno na gharama ambazo si za msingi
1. Ili upate mzigo lazima uwe na agent ambaye unatakiwa umlipe sijui kwa. Nini wameweka huu mfumo?
2. Mzigo unakagulia na taasisi kama tano hivi na zote unatakiwa ulipie TRA, TBS, hearth care, TFDA n.k
Hizo taasisi utakuta kuna agent mmoja mmoja ambae anakagua mizigo na kuingiza data
Nimesikitishwa kuona TBS wana fees kubwa kuliko TRA nililipa TRA 41,000/- TBS 180,000/- (personal effect )
Gharama za storage zipo juu ya mteja japo uzembe wa kutoa mzigo ni wa mamlaka husika
Mwisho
Rafiki yangu alituma mzigo kupia Kenya mpaka Tanzania alilipa laki mbili mpaka kuupata mimi nimemaliza laki saba
Mamlaka husika boresheni huduma za Airport mnakosa mapato mengi kizembe
Mzigo kukaguliwa na taasisi zaidi ya moja inataegemea na HS CODE ya mzigo/items. Ila TRA na TBS lazima wakague. Hao TFDA, HEALTH CARE, TBS nk wapo hapo coz HS CODE ya mzigo zimewahitaji kwenye system.
TBS wamekuchaji 180,000 kwa sababu ni DI(destination inspection) ambayo lazima wachukue sample wakapime then wakupe permit. Ila ingekuwa COC usingechajiwa hivyo au ingekuwa ni physical tu ungechajiwa 30000. Kwa person effects lazima kuna items zilihitaji sample..
Yes, storage lazima ulipe kwasababu mtunza mzigo hausiki na hizo taratibu zenu agent wako anapaswa kukimbiziana na muda kuokoa hiyo storage charges. kwa airport una cku4 free zakutoa mzigo wako bila storage,. Kwa seaport ni siku7(inahesabiwa container inaposhuka kwenye meli).
Hivyo agent wako lazima aassess mapema coz system zenyewe(TANCIS/TeSWs) zinazinguaga sometimes.