Kama ni adhabu ya kutoa mzigo pale airport ni hii, poleni wafanyabiashara

Kutumia Agent ipo kimataifa sio tu Tanzania, hili ni sawa coz kuna taratibu za kiforodha lazima zifuatwe.
Mzigo kukaguliwa na taasisi zaidi ya moja inataegemea na HS CODE ya mzigo/items. Ila TRA na TBS lazima wakague. Hao TFDA, HEALTH CARE, TBS nk wapo hapo coz HS CODE ya mzigo zimewahitaji kwenye system.

TBS wamekuchaji 180,000 kwa sababu ni DI(destination inspection) ambayo lazima wachukue sample wakapime then wakupe permit. Ila ingekuwa COC usingechajiwa hivyo au ingekuwa ni physical tu ungechajiwa 30000. Kwa person effects lazima kuna items zilihitaji sample..


Yes, storage lazima ulipe kwasababu mtunza mzigo hausiki na hizo taratibu zenu agent wako anapaswa kukimbiziana na muda kuokoa hiyo storage charges. kwa airport una cku4 free zakutoa mzigo wako bila storage,. Kwa seaport ni siku7(inahesabiwa container inaposhuka kwenye meli).
Hivyo agent wako lazima aassess mapema coz system zenyewe(TANCIS/TeSWs) zinazinguaga sometimes.
 
Hatari sana, sijui hii chuki aliyeipandikiza ni nani

Nimetafakari sana mimi nikaja kugundua nyuma ya yote haya ni CCm wanafikiri wakitufanya Mafukara watatuwala kwa urahisi
 
Nilikuwa na kilo 63 tu mkuu
Duh wewe hukuingia front. Mimi yule agent nlikua nakula nae sahani moja ananiingiza mpk kwa mabosi nalia kama mtoto
Nlikua na kilo mara 3 ya za kwako. finally nkalipa tu laki tano something. Washenz Sana.
ujinga ni kua personal effects ukipita nazo ukisafiri nazo no free lkn ukizileta km cargo msala.
 
Tanzania kuna usumbufu sana yaani wanaonekana wapo kukwamisha watu wasipate bidhaa kutoka nje ya Nchi wakati wapo kwenye mlango wa Dunia mbaya sana kwa kweli...
 
Nchi ngumu sana hii na Adui wa Mtanzania ni Mtanzania mwenzake
Nikipata hela ya kununua apartment nje around 2.4B TZS hii nchi nawaachia yaani kuwa na gari ni anasa jamani.
Nchi ambayo ukiwa na bilioni zako kadhaa benki zinakombwa.
Lake zone wahujumu uchumi walikuwa ni kabila fulani tu.
Kuna mzee alichukuliwa 20Bn mpaka akapata stroke.yaani naogopa Sana jamani kumiliki bilions of money
 
Maccm yatabisha
 

Hakuna sample imechukuliwa ya kitu chochote kwenda kupima mzigo umefunguliwa ukakaguliwa na kufungwa

Then mamlaka husika yaangalie namna ya wakaguzi watarahisisha maana ukaguzi unachukua mpaka masaa matano, mtu mmoja anakagua anaingiza data anazituma data kwa nini wasweke mkaguzi then anapeleka file kwa muingiza data kuna vitu haviko sawa pale
 
Sawa, tutalifanyia kazi
 

Umejibu ki TAFFA zaidi, ma HS code, ma physical verificiation, DI, safi tunawaacha watu kwenye flyover ubungo. Nikusaidie kdogo Kwenye hiyo 180,000 ya TBS huwa ni mzigo wa ambao HS CODE yake IPO REGULATED na TBS ambapo hufanyika physical verification tu hakuna kuchukua sampo, ikichukuliwa sampo itazidi hiyo kulingana na test fee ya sampo hiyo / hizo na 30,000 huwa ni mizigo ya PVoC exempted ambayo mteja huchajiwa service fee tu au mizigo ya Non Regulated lakn mteja anakua am lodge kwa matakwa ya ulazima kwa TeSWS ila kwa TANCIS sio lazma alodge
 
Hivi kwanini hao healthcare na tfda wasiwe maafisa walioajiriwa ndani ya tbs ili kuokoa muda?

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…