Kama ni kurogwa Watanganyika wamerogwa na mchawi kafariki katuachia msala huu

Kazi ya watanzania ni kufuatilia ujinga ujinga tu..Na hii Simba na Yanga ni kichaka Cha kuendeleza ujinga, Ujinga kabisa huu.. Tuanze maombi makali ya kufutilia mbali huu ushabiki maandazi wa Simba na Yanga.
Na hawa bongo fleva na bongo movies ndio matakataka kabisa
 
Mwenye changamoto ni wewe mwenye uelewa kuhusu siasa na athari zake za moja kwa moja kwenye maisha ya mtanzania.

Unafahamu fika watu wengi nchini hawana uelewa mkubwa wa maswala ya kisiasa na hii inasababishwa na mifumo yetu ya maisha, sasa wewe mwenye uelewa kuhusu siasa instead of kuwaelimisha hawa wasioelewa unaanza kuwalaumu.

Kama utaendelea kuwalaumu mimi nitasema wewe ndiye umerogwa kwasababu hautumii vyema maarifa uliyonayo kwa jamii.

Toa elimu, toa elimu, toa elimu, Next time ukirudi hapa tueleze umefanikisha kushare maarifa uliyonayo kwa jamii kwa kiwango kipi na output ni ipi nasio kuwalalamikia watu wambao hawana maarifa.
 
Ulianza vyema lkn 8 umekengeuka.
 
Unamwelewesha mbunge au waziri na ana kuteka na kukuua. Hembu kaa kwa kutulia na waza tena. Hawa wakuelewesha ndio machawa kabisa na sifu na kuabudu mtu mmoja. Nchi ina wahitimu wa vyuo ila haina wasomi wa kulikomboa taifa
 
Ujumbe wako ni mzuri ila umetumia hasira sana na chuki kutufikisha...acha tabia za kibaguzi basi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…