Kama ni kweli, basi comrade Kinana amepuuzwa!

Kama ni kweli, basi comrade Kinana amepuuzwa!

JERUSALEMU

JF-Expert Member
Joined
Sep 19, 2012
Posts
3,114
Reaction score
3,541
Habari wanajamvi!

Sijaamini maneno ya msemaji wa chama cha Mapinduzi labda nitaaminishwa baadae. Kwa maneno yake Katibu mwenezi anasema ni kweli mwanasiasa nguli na Katibu Mkuu wa chama cha mapinduzi comrade Alhajji Abdulrahman Kinana alikuwa anaumwa, na alipelekwa nje ya Nchi kwaajili ya matibabu,lakini kwa sasa amerudi yupo Nchini anapumzika nyumbani kwake! Hajafafanua kama ni Dar es salaam au Arusha. Nikajiuliza maswali yafuatayo;

- Hivi inawezekana kweli Katibu Mkuu wa chama arudi kutoka kwenye matibabu halafu asipokelewe na Mtu yeyote pale Airport? Hata ndugu zake hawakwenda kumlaki? Yaani asionekane na mwandishi wa habari hata mmoja?

- Tuseme yupo nyumbani kweli anaendelea kupumzika baada ya matibabu na huenda ana ED za miezi miwili au mitatu, lakini hakuna hata mtu mmoja alie kwenda kumpa pole? Yaani hata katibu mwenezi Naibu katibu mkuu hawajaenda kumpa pole!

- Yaani hata viongozi wote wanao julikana kwa uungwana wao wa asili kama Mbowe, Maalimu Seif, n.k Hawajaenda kumjulia hali? Nini kimetokea?

Ndio maana nikaishia kusema kama ni kweli kuwa Comrade Alhajji Abdulrahmani Kinana amerudi yuko nyumbani na hakuna mtu hasa wanao penda kuonekana kwenye vyombo vya habari, basi ni dhahiri ndugu yetu amedharauliwa na kupuuzwa.

Binafsi naomba wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari kampeni pole kwa niaba yangu.
IMG-20170506-WA0006.jpg
 
Mbona sioni tatizo lolote....

Mmeumbuka kwenye ndege na huyo mpiga picha wenu sasa mmeibuka na non issue kuhusu mzee Kinana....

Bado nacheka kuhusu mpiga picha Woody....😀
Jibu hoja ni kawaida kwa kiongozi wa ngazi ya juu kama KATIBU MKUU wa chama kurudi kimyakimya? Imeanza lini? Au nako ni kubana matumizi?
 
Kunataarifa zinasambaa kaamba tarehe 6/5/2017 atakutana na kuzungumza na baadhi ya wanachama wa jumuiya ya ccm ya vyuo vikuu nyumbani kwake. Waandishi wa habari nao wamealikwa.
 
Jibu hoja ni kawaida kwa kiongozi wa ngazi ya juu kama KATIBU MKUU wa chama kurudi kimyakimya? Imeanza lini? Au nako ni kubana matumizi?
Alikuaga wakati anaondoka?

Alikuwa anakutaarifu yanayojiri huko alipokuwepo?

Katibu mkuu wa CHADEMA huwa anakuaga wakati akisafiri na huwa anakutaarifu anaporejea?

Kama Kinana alikuwa huko alikokuwa kama mtu binafsi na si kama katibu mkuu wa chama wewe inakuhusu nini kujua kama karejea au la?

Yaani mnatafuta kila aina ya vijisababu tu ili mumseme rais Magufuli.....


Btw, mpiga picha Woody hajatoa tu tweet ingine?[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Hana hoja huyu nadhani anaisoma number bado. Mtapoteana uwanjani chenga zimewalevya
 
Kunataarifa zinasambaa kaamba tarehe 6/5/2017 atakutana na kuzungumza na baadhi ya wanachama wa jumuiya ya ccm ya vyuo vikuu nyumbani kwake. Waandishi wa habari nao wamealikwa.
Zenda ameshakana hiyo taarifa sio ya kweli.
 
Labda nae katekwa..[emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125]
 
Back
Top Bottom