Kwahiyo mnatumia ruzuku ya Tundu Lisu?
Bure kabisa wewe kijana wa Robert Amsterdam!
MAKUNDI YA RUZUKU ZA VYAMA.
ruzuku za vyama zipo katima makundi mawili.
1.Ruzuku inayotokana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania(JMT).
hii inaelezwa katika sheria ya vyama vya siasa sura namba 258 ya mwaka 2002 iliyotungwa na Bunge la JMT.
2.Ruzuku inayotokana na Serikal ya Mapinduzi ya Zanzibar(SMZ).
hii inaelezwa katika sheria namba 6 ya vyama vya siasa ya mwaka 1997 pamoja na marekebisho namba 1 ya mwaka 2013 iliyotungwa na Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
UFAFANUZI ZAIDI.
(A) RUZUKU INAYOTOKA JMT.
Ruzuku hii ipo katika sehemu tatu.
(1).Serikali itatenga fedha si zaidi ya asimilia mbili ya bajeti yake ya mwaka kwa ajili ya ruzuku ya vyama vya siasa.
Ruzuku hii naipa jina la RUZUKU X.
(2) Ruzuku inayotengwa kulingana na uwiano wa madiwani kwenye halmashauri za wilaya au miji.
ruzuku hii naipa jina la RUZUKU Y.
(3) Ruzuku inayotengwa kwa kuangalia uwiano wa kura za wagombea Urais.
ruzuku hii naipa jina la RUZUKU Z.
# RUZUKU X:ruzuku inayotengwa isiyozidi asilimia 2 ya bajeti yote ya serikali.
mgawanyo na masharti yake.
(a): asilimia 50 ya pesa iliyotengwa itagawanywa kwa vyama vya siasa katika uwiano wa idadi ya wabunge wa kuchaguliwa kwa kila chama.
kama chama hakina mbunge hakitapata mgawo huu.
kama mgombea ubunge alipita bila kupingwa basi itachukuliwa asilimia 51 ya wapiga kura wote katika jimbo husika na kuhesabiwa kuwa hizo ndizo kura alizopata mbunge huyo ili zitumike kuamua ruzuku hii.
wanufaika hapa watakuwa CCM, wakifatiwa na CUF,CHADEMA na kwa pamoja NCCR na ACT vyenye mbunge mmoja kila chama.
vyama vingine havitapata kitu katika pesa hizi kwa kuwa havijashinda ubunge.
(b): asilimia 50 ya pesa iliyobakia itagawiwa katika vyama vya siasa vilivyofikisha asilimia 5 ya kura zote za wagombea wake wa ubunge kwa kulinganisha na kura zote halali zilizopigwa nchi nzima kwa wagombea ubunge wote bila kujali walishindwa ama walishinda.
vyama vitakavyonufaika na mgao huu ni vitatu. CCM ikifatiwa na CHADEMA na mwisho CUF.
vyama vingine vyote havitapata kitu kwa kuwa havikufikisha asilimia 5 ya kura zote halali za wagombea ubunge.
# RUZUKU Y:ruzuku inayotengwa kwa uwiano wa madiwani wa kila chama katika halmashauri ya wilaya au mji.
ruzuku hii itaamuliwa wa waziri kwa namna atakavyokadiria ama kuamua.
ili chama kipate ruzuku hii ni sharti kiwe kimeshiriki uchaguzi wa hivi karibuni na mgombea wake wa ubunge akashinda au mgombea wake wa udiwani akashinda.
kwa faida tu ya kila msomaji ni kwamba mbunge ni diwani kwa mujibu wa sheria za mamlaka za miji na tawala za mikoa.
Hivyo isionekane ni kosa kwa sharti hili kumujumuisha mbunge pia.
kwa hiyo vyama vitakavyonufaika na mgao huu vitaongozwa na CCM, CHADEMA,CUF, NCCR na ACT. kwa kuwa vimepata madiwani au wabunge. sina taarifa za uthibitisho kama kuna chama kingine kimeshinda udiwani nje ya vyama hivi. kama kipo nacho kitapata mgao huu.
# RUZUKU Z: ruzuku inayotokana na kura za mgombea Urais.
nimejaribu bila mafanikio kupata sheria inayoelezea mgawanyo wa fedha hii lakini sikufanikiwa.
lakini kwa kiasi chake nafahamu kuwa ili chama kipate ruzuku hii ni sharti kura za mgombea wake wa Urais ziwe zimefika asilimia 5 ya kura zote halali zilizopigwa kwa wagombea wote wa urais.
kwa mkutadha huu vyama vitakavyonufaika hapa ni vyama viwili tu. CCM na CHADEMA kwa kuwa ndivyo vyama pekee vilivyoweza kufikisha asilimia 5 ya kura zote za Rais(wa jamhuri). ACT na vyama vingine havikufanikiwa kufikisha idadi ya kura zinazotakiwa hivyo havitapata hata mia katika kundi hili la ruzuku.
(B): RUZUKU INAYOTOKA SMZ.
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inaruhusiwa kutenga kiasi cha pesa ambacho si zaidi ya asilimia 1 ya bajeti ya serikali ya Mapinduzi kwa ajili ya ruzuku kwa vyama vya siasa.
ikumbukwe kuwa ile pesa ya JMT si zaidi ya asilimia 2 ya bajeti.
MGAWANYO WA PESA HII.
(a) asilimia 25 ya pesa iliyotengwa itagawiwa kwa chama kilichoshinda Urais(Urais wa SMZ).
kwa hali ilivyo Zanzibar mpaka sasa haijafahamika nani ni Rais ya serikali ya Mapinduzi ya Zanzibara baada ya Jecha kufuta uchaguzi kinyume cha sheria na kinyume cha katiba.
lakini kwa vyovyote vile mnufaika wa pesa hizi ama atakuwa CUF ama CCM kwa kuwa hivi vyama ndivyo vinapewa nafasi kubwa kati ya vyama vilivyosimamisha wagombea urais.
CHADEMA kwa vyovyote vile haiwezi kupata mgao huu kwa kuwa haikusimamisha mgombea Urais SMZ.
(b) asilimia 50 ya pesa iliyotengwa itagawiwa kwa vyama ambavyo vimenyakua viti vya baraza la wawakilishi( vimeshinda majimbo ya uwakilishi).
kwa namna ilivyokuwa kabla ya matokeo kufutwa CUF ilikuwa katika nafasi nzuri zaidi ya kupata sehemu kubwa ya mgao huu ikifatiwa na CCM kulingana na majimbo ambayo yalikuwa tayari yametangazwa washindi wake.
katika mgao huu vyama vingine havitapata kitu kutokana na kutopata ushindi katika maeneo vilivyogombea kabla ya kufutwa kwa matokeo.
(c) asilimia 25 itagawanywa kwa vyama vile tu ambavyo vilishinda ama vimeshinda kata kwa mujibu wa sheria inayofafanua. ieleweke kuwa kwa upande wa Zanzibar SHEHIA ndio kama kata kwa huku bara. kwa hiyo shehia zipo chini ya mamlaka za mji za na tawala za mikoa.
hapa wanufaika wakuu watakuwa CCM na CUF kwa kuwa hivi ndivyo vyama vinavyopewa nafasi kubwa, hata matokeo ya uchaguzi wa October 25 vyama hivi ndivyo vilionekana kupata viti vingi zaidi.
NB:
1.Malipo ya ruzuku hizi yanalipwa kutokana na serikali itakavyoamua ama ilipe kwa mkupuo ama kila baada ya muda fulani. mara nyingi ruzuku inatolewa kila mwe.
UCHAMBUZI HUU UMEANDIKWA NA: Joseph Mshinga.