Li ngunda ngali
JF-Expert Member
- Jun 22, 2023
- 707
- 2,572
Watanzania wenzangu hatima ya ustawi wa Taifa letu upo mikononi mwetu. Ni wajibu wetu kama Watanzania tujizuie kwa namna yeyote ima kununuliwa ama kushawishiwa kwa namna yeyote ile ilmradi tuligawe Taifa na rasilimali zetu.
Safari za namna hiyo za watu maarufu na wasanii wetu kwenda huko Dubai kwa nyakati za SINTOFAHAMU kubwa ihusuyo bandari yetu na wao badala ya kueleweka hakika zinaongeza maswali mengi mno kwa wenzetu wenye mashaka na mradi wetu pendwa tarajiwa.
Nakemea kwa nguvu zote, njia za aina yeyote zifananazo na hiyo ya ushawishi kwa jamii yetu kuhusu hilo!
Vilevile, siamini hao wasanii na watu maarufu wanatumia pesa zao kutoka mfukoni kuhimili gharama za hoteli za aina hiyo ya hapo juu kwa zaidi ya siku nne!
JE, KAMA HAWA WASANII WANATUNZWA KIFALME HIVYO (kama ni kweli) ILIKUWAJE KWA WAWAKILISHI WETU WALE 30?!
NAANZA KUHOFIA PENGINE TUPO KWENYE HATARI TARAJIWA!
Chama changu CCM naomba kama kikombe hicho kinaweza kutuepuka kwa kuzingatia MASLAHI MAPANA kwa Taifa letu tulipendalo na tukiepuke!
Kidumu Chama cha Mapinduzi.